Jikomboe Kiuchumi Hatua #2 - Lipa Madeni Yako [The Snowball Method]

Apr 5, 2024
78
106
Habari wanaJF,
Natumaini mnaendelea vizuri. Leo ni February 13, na nimejikuta nimevaa polo nyekundu (mke wangu aliamua kufua nguo zote leo, so hi ndo ilibaki kabatini. Tupo wanaume kama 4 hivi wenye shati nyekundu hapa mzigoni, kitu ambacho sio kawaida). 14/02/2024 (mwaka jana) nilivaa polo hii hii (sitanii, na sio maksudi).

Sasa, jana tulizungumzia mada fulani kuhusu hatua 7 za kujikomboa kiuchumi. Uzi huu hapa.

Hatua saba hizo ni:
1️⃣ Kujiwekea akiba ya mwanzo (emergency starter fund) (angalau laki 1, mshahara wa mwezi 1, au $1,000+ kwa wafanyabiashara).
2️⃣ Kulipa madeni yote (tofauti na yale ya maendeleo ya ujenzi).
3️⃣ Kujiwekea akiba pana ya dharura ya miezi 3-6 ya matumizi yako ya mwezi (itakusaidia maisha yakikupa TKO).
4️⃣ Kuwekeza 15% ya kipato chako katika kikokotoo binafsi.
5️⃣ Kuweka akiba kwa ajili ya elimu ya watoto wako.
6️⃣ Fedha na mpango wa kujenga na kuhamia kwako.
7️⃣ Kukuza mali yako na kutoa msaada kwa wengine (ukarimu kwa jumla).

Leo naomba kuzungumzia hatua ya pili.

_____________________________​

Uhalisia Kuhusu Madeni​

Madeni hutujia kwa namna mbalimbali:
Mikopo ya simu (MPAWA, SONGESHA, NIPIGE TAFU nk). Unapoteza 20% ya pesa zako hapa.
Kausha damu (mtaani kwetu kuna wakopaji binafsi wanachukua hadi 30% riba. Kuna mtu aliweka bondi nyumba. Kwa laki 5. Akashindwa kulipa...)
Mikopo ya Benki AKA Topup (inakuwa changamoto kama ulichukua mkopo kwa ajili ya chakula cha kila siku, au kununua vitu vya ndani, au nguo)
Mkopo wa chuo/Boom (Hili limewakwaza wengi. Tutakuja kulizungumzia kwa undani baadaye)
Madeni ya ndugu na marafiki (usipolipa kwa wakati, utakosana na watu. Imewahi kunitokea)

Umuhimu wa hatua hii​

  • Madeni hukuibia mapato ya kesho. Ukiwa na madeni, kila unapopata pesa, unahudumia wadeni wako badala ya kukabiliana na njozi zako za kiuchumi.
  • Madeni humkwamisha mtu. Huwezi kukua au kuwekeza endapo pesa zako zote zinatumika katika kulipa tu.
  • Dharura hugeuka kuwa janga. Ukipoteza kazi au kukutana na hali ya ngumu ghafla, madeni hubaki palepale.

_____________________________​

The Snowball Method (Lipa kwa Kujenga Kasi)​

Sasa hapa Tanzania hatuna uzoefu na theluji. Kwa hiyo ntatumia mfano ufuatao kukuelezea mbinu hii ya kulipa deni kwa kujenga kasi ya malipo.

Njia hii ni rahisi: unapanga madeni yako kuanzia lile dogo zaidi hadi kubwa zaidi, halafu unalipa kidogo kidogo huku ukiongeza kasi unapomaliza deni moja.

Mfano wa kawaida:

Mama Asha, mfanyabiashara mdogo jijini Dar es Salaam, ana mapato ya TZS 500,000 kwa mwezi lakini anadaiwa madeni yafuatayo:

💵 Mkopo wa simu (MPAWA) – TZS 20,000
💵 Deni la Mama Mwajuma– TZS 80,000
💵 Mkopo wa Kikoba – TZS 100,000
💵 Deni ya Yakobo Mangi (Mkopaji binafsi) – TZS 1,500,000

Atalipa deni lake kwa kuchukua hatua zifuatazo:

1️⃣ Anaanza na deni dogo zaidi – Mkopo wa MPAWA(TZS 20,000). Anaweka bidii kulipa haraka, labda kwa TZS 2,000 kila wiki.
2️⃣ Baada ya kumaliza hilo deni, anaongeza pesa aliyokuwa akilipa kwenye deni linalofuata – Deni linalofuata ni la mama Mwajuma. Huyo mama alisisitiza kuwa anataka hela zake zote kwa pamoja.

Mama Asha akaamua kuweka akiba kidogo kidogo mpaka kufika tarehe ya malipo, awe ametimiza lengo. Labda alidhamiria kuhifadhi 10,000 kila wiki. Sasa, mara tu baada ya kukamilisha deni la MPAWA, ataweka 12,000, badala ya 10,000 kumalizia deni hii.

3️⃣ Anafanya hivyo kwa kila deni linalofuata – Mkopo wa Kikoba atalipa TZS 30,000 kwa mwezi badala ya 10,000. Na deni la Mangi atalipia TZS 180,000 kwa mwezi badala ya 100,000 alopanga.

Matokeo? Anaondoa madeni yake yote haraka.

Nafahamu kuwa mbinu hii inaweza kuonekana kuwa ngumu kwa watu wengi, na hasa kama unapitia maisha magumu kwa sasa. Ila, penye nia pana njia, na unaweza kujaribu, au kuboresha kulingana na mazingira yako.

Vitu vya Kuzingatia​

💡 Usikope ili kulipa deni lingine – Utajikuta kwenye mzunguko usioisha wa madeni.
💡 Uza vitu visivyotumika – Kama una simu ya zamani, kifaa usichotumia, au shamba lisilokuwa na tija tena, uza ili upate pesa za kulipia madeni.
💡 Ongeza kipato – Tafuta shughuli za ziada kama biashara ndogo, bodaboda, au kazi za mtandaoni ili kuongeza pesa za kulipa madeni.
💡 Epuka shinikizo kutoka kwa familia na marafiki – Usikubali kutumia pesa zako kusaidia wengine ilhali bado hujamaliza madeni yako.

Tuishie hapo kwa leo:​

Kama una deni lolote, usikate tamaa! Mbinu nlokupa leo ni namna moja rahisi, hata kama kipato chako ni kidogo. Anza na deni yenye kiasi kidogo, jitutumue kilimaliza, kisha piga hatua moja baada ya nyingine kuelekea uhuru wa kifedha.

Mchana mwema ndugu yangu. Pambana tu. Iko siku...
 
Noma sana!
 
Mie napataje hao wakopaji kwa kausha damu waje kwangu mie riba 10% tuu.
 
Back
Top Bottom