Jifunze kupitia wanandoa hawa

Mtuache

JF-Expert Member
Mar 12, 2021
256
656
"Wanandoa walihamia kwenye nyumba mpya.

Asubuhi iliyofuata wakiwa wanapata kifungua kinywa, yule mwanamke akamuona jirani yake akianika nguo nje alizofua.

Akasema, "naona kama zile nguo hazijatakata vizuri; huyu jirani hajui kufua vizuri. Inawezekana anahitaji sabuni ya unga yenye nguvu zaidi."

Mumewe akatazama, kisha akakaa kimya.

Kila mara jirani yake alipoanika nguo zake nje ili zikauke, yule mwanamke akawa anatoa maneno yale yale.

Mwezi mmoja baadae, yule mwanamke akashangaa kuona nguo zilizofuliwa vizuri kabisa zikiwa zimetundikwa kwenye kamba, akasema, "tazama, hatimae sasa amejifunza kufua sawa sawa. Najiuliza ni nani atakuwa amemfunza kufua vizuri hivi?"

Mumewe akamjibu, "niliamka mapema sana leo asubuhi na nikasafisha madirisha yetu yote."

Na hivyo ndivyo maisha yalivyo...

Tunayoyaona tunapowatazama wengine hutegemea zaidi usafi na uwezo wa dirisha tunalotazamia.

Hivyo, usiwe mwepesi sana kuwahukumu wengine, kipekee pale ambapo mtizamo wako wa maisha umezongwa na hasira, wivu, huzuni, hali hasi au matamanio ambayo hayajatimia.

Kumhukumu mtu hakumpambanui yeye alivyo bali hupambanua wewe ulivyo."

Asante kwa kusoma
 
FB_IMG_17311300387023753.jpg
 
nikajua mumewe ndio kaenda kumsanua jirani, sasa hapo niige nini mimi wakat kila mmoja anaishi na kichaa chake kinavyompelekesha? umbea tu
 
sisi siyo wakamilifu sana kiasi cha kuhukumu wengine
Asante kwa ujumbe mzuri
 
Watu tunajipea sana uperfect....
Kuna muda unamwacha mtu ajiinue ili mwisho wake ajionee mwenyewe
 
Back
Top Bottom