Jifunze aina 3 za watu kwenye maisha yako

Pasta Joshua

Member
Aug 2, 2020
14
110
Katika maisha kuna aina nyingi za watu , leo nitakupa aina tatu za watu ambazo zinaweza kuwa msaada kwenye maisha yako kwa namna moja au nyingine.

1.Leaf People (Watu Majani).
Hii ni aina ya watu ambao wanakuja kwenye maisha yako kwa kipindi fulani tuu. Hawa ni watu ambao hautakiwi kuwategemea, Ni watu dhaifu sana. Maranyingi wanakuja kuchukua wanachokitaka na kukitamani kutoka kwako na wanaondoka.

2.Branch People (Watu matawi)
Hawa ni aina ya watu ambao ni imara sana, lakini huwa wanaondoka maisha yakiwa magumu. Nao watakaa na wewe kwa kipindi fulani na kuondoka maisha yakiwa magumu.

3.Root People(Watu Mizizi).
Hawa ni watu wa muhimu sana, huwa hawafanyi vitu vikaonekana kwa watu.

Wapo na wewe vipindi vyote vigumu na vyepesi, watakusaidia kusimama nyakati ngumu ambazo hata maji amna na unakiu kali sana.

Pia cha ajabu hawa watu huwa hawasemi kuwa wapo nawe na huwa hawagunduliki kirahisi.

Wanakuwa wanakupenda sana ila hawasemi.Ebu jitahidi uwagundue. Wakati mwingine ni watu wa kujitokeza sana kwenye majanga yako

Hawaishi na wewe kutokana na cheo, au nafasi fulani uliyo nayo katika maisha bali huwa na wewe kutokana na jinsi ulivyo.

Jiulize je!! Ni aina gani ya watu walio kuzunguka kati ya hawa. Watu majani, Watu Matawi na Watu Mizizi.????

FF7F7A1E-6072-46E1-8485-E74C45D04217.jpeg
 
Sina hata rafiki wa karibu sinaga ukaribu na watu kabisa na sipend hekaheka na watu napenda kukaa pekee angu nakufanya mambo yangu bila kelele na mtu mtu akipiga kelele za redio tu nakereka
 
Watu ndiyo wametupa darasa la kujua uhalisia wa wema, ubaya, unafiki, na umuhimu wa watu!

Watu ndiyo changamoto

Watu ndiyo fursa,

watu ndiyo daraja,

Muhimu kujua, na kuwaelewa watu!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom