Jezi za Yanga leo zimevaliwa hatari

Nebuchadneza

JF-Expert Member
Oct 6, 2023
435
1,092
Salamu ya mjini sasa ni HAMSA

Aisee katika watanzania 10 ninaokutana nao 8 wamevaa jezi,za msimu uliopita au msimu huu,katika watu 100 ninaokutana nao mtu mmoja tu kavaa jezi ya simba,na akikutana na watu wa yanga kama anakimbia vile na kuhinamisha kichwa chini.

GSM wamepiga pesa sana kwenye huuzaji wa jenzi za yanga,yanga inaongoza AFRICA kwa huuzaji wa jenzi, zinavaliwa Africa nzima ukienda Uganda unazikuta, Kenya zimejaa Burundi na Congo zipo za kutosha aisee kwa hapo nawapa BIG UP hii ni record ya kibabe.

Mimi NEBUCHADNEZA, MASTER, GENIUS, MZEE WA KUWAINGIZA CHAKA.
NIliposema kuwa mechi ya simba itahairishwa makolo yalijaa yakajiamini kuwa yatashinda kwa kuwa mvua ilinyesha sana wakajua mvua niyao, kumbe kwa hali alisi ilivyo SISI CHURA(YANGA) huwa tunapenda mvua kubwa huwa ndo kipindi cha kupiga kelele za shangwe kwenye vidimbwi vyetu,ila kwa wenzentu MAKOLO (SIMBA) huwa wanaiogopa mvua kwa kuwa inahodhesha kucha zao na kupanda juu ya mtu ili kucha zisiho,rejea SIMBA WA MANYARA. Basi haya majina yanaendana kabisa na timu hizi zetu mbili pendwa hapa Bongo.

Kuna watu wanasema eti YANGA imewahonga baadhi ya wachezaji SIMBA ili waachi yale magoli ila kwa akili za kawaida ambazo hazihitaji hata kwenda shule. Ebu tuangalie usajili wa YANGA.

1. PACOME
2. MAX
3. YAO

Yani hao watu ni kisanga na nusu,usiombe kukutana nao kabisa. Haya anagalia sajili za SIMBA.

1. ONANA
2. CHEMALONE
3. MIQUISSON

HAHAHAHAHAHAHA vituko vya karne yani mpaka hapo umeona madhaifu ya watu wanaofanya sajili za SIMBA.
Wachezaji wa SIMBA wengi ni wazee,wapo slowly sana hawana mpira wa KASI rejea.

1. SAIDO
2. CHAMA
3. KAPOMBE

Ndani ya SIMBA kuna wachezaji 2 tu

1. KIBU DENIS
2. MZAMIRU

Lakini wote waliobaki hawafai kuchezea simba, waliletwa kwa mihemko ya viongozi wa SIMBA, hawana spirit ya kuchezea SIMBA, hizi timu mbili hapa bongo zinahitaji wachezaji wenye moyo wa kupanda kweli kweli, wanaojitoa kwa ajili ya timu.

YANGA WALICHOWA WIN SIMBA MBALI SANA NI KUSAJILI VYEMA WACHEZAJI WANZURI WENYE MOYO WA KUJITOA PIA KUTAFUTA KOCHA NWENYE FALSAFA NZURI NA UONGOZI MNZURI USIO NA MBAMBAMBA ZA BIL 20.

HAMSA HAMSA HAMSA HAMSA YOOO HAMSA HAMSA YOOOO.
 
Mimi leo ningetembea na mtoto wa mama mkwe angenuna tu! Jamani nimesifiwa leo, kila mtu na lake.
Kila ninayepishana nae lazima aongee neno, la kunisifu kupendeza au pongezi za ushindi mnono!

Hapo nilivaa jezi yangu kama walizovaa wazee wa kazi jana, na nakiri wengi sana tumeamka na jezi zetu.
Hii ni wiki ya jezi za Yanga, wengine tupisheni kwanza.
 
20231106_115947.jpg
 
Huwa yanga ikishinda tena haswa mechi kubwa kama ya jana jezi huuzika sanaaa.

Leo tumeringa sana na jezi zetu, full burudani yaani💚💚💛💛
 
Back
Top Bottom