SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 6,991
- 11,497
Katika pitapita zangu huku mitandaoni, nimekutana na comment zaidi ya moja ya watu wanaosifia kit ya jezi za Tanzania zilizotumika huko AFCON na nilipofuatilia inaonyesha watu hao siyo Watanzania. Hili ni jambo jema sana.
Mfano, kuna mmoja alisema "So this Tanzanian fine jersey just wasted, the most beautiful jersey this Afcon, a pity I won't see this kit again in Afcon", kwa tafsiri ya haraka haraka akimaanisha "Kwa hiyo hii jezi kali ya Tanzania imetumika bure, jezi kali kuliko zote katika hii AFCON, ni bahati mbaya hatutaiona tena katika mashindano haya"
Niliwahi kuwasifia Sandaland walipotoa jezi ya kwanza kabisa ya Simba ya msimu huu.
Nimekutana na comment nyingine ya mtu mmoja baada ya mechi na DRC amehoji inakuwaje Tanzania inatumia kit nyingi, akisema hii ni kit ya tatu kuiona inatumika. Pamoja na kwanza inaonyesha haelewi sheria za mashindano huwa zinataka timu ziwe na jersey zaidi ya moja ila kuna jambo la msingi katika comment yake.
Tujaribu kubuni na kutumia jezi kuu ambayo itakuwa ni unique ambayo tutakuwa tunaitumia mara kwa mara ili iwe utambulisho wa timu ya Taifa, na tubadili pale tu inapohitajika kufanya hivyo au hadi mashindano mengine makubwa tutakayoshiriki. Jersey ni kama logo hautaki kila siku uwe unaibadilisha badilisha bila sababu maalumu. Ukiangalia mechi tatu tulizocheza huko AFCON, tungeweza kutumia jezi moja yoyote katika zile tatu katika mechi zote maana hazikuwa zinaingiliana na jezi ya timu nyingine.
Mtandao maarufu wa habari za michezo wa ESPN umeipa nafasi ya 15 kati ya 24 kit jersey ya Tanzania.
Mtandao wa Urban Pitch umeiorodhesha home jersey ya Tanzania ya blue yenye kola ya njano shingoni kama moja ya jezi 5 bora katika mashindano.
Mtandao wa Balls.ie wa huko Ireland umeipa jersey ya Tanzania nafasi ya 4.
Kwa kumalizia, nadhani katika maboresho ya jezi kuu inahitaji pia kuwa na alama ya nyota kuleta maana nzima ya "Taifa Stars". Nyota inaweza kukaa moja kifuani kama ya Ghana au tukazipanga kama 3 hivi mabegani kumaanisha mastar wetu ni wapiganaji wetu.
Nje ya Mada: Aishi Manula ameorodheshwa katika moja ya top 5 saves za hatua ya makundi. Tujivunie kidogo na hili!

Mpaka sasa nimependa tone ya wekundu anaotumia Sandaland kwenye jezi ya Simba. Vunjabei alikuwa anachanganya shade za wekundu zaidi ya moja kwenye jezi moja, sina uhakika ni ubunifu wa wapi wa nguo unaoweza fanya kitu kama hicho. Zile nguo walizovaa wakati wanakwenda Uturuki ni kali sana ingawa najua ni za mpito. Ile combination ya blue na red inanikumbusha Tommy Hilfiger.