the guardian 17
JF-Expert Member
- Aug 15, 2024
- 334
- 489
Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro limewakamata watu saba wanaodaiwa kuendesha biashara haramu ya fedha mtandaoni bila kibali cha Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Soma pia: Jeshi la polisi Mbeya limewakamata watu watano kwa kuhusika na mchezo wa upatu wa LBL
Watuhumiwa hao ni wawakilishi wa kampuni ya Leo Beneth London (LBL), wakifanya shughuli zao katika Manispaa ya Morogoro na Turiani, Mvomero.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, SACP Alex Mkama akizungumza leo Alhamisi, Februari 20, 2025 amesema waliwakamata watuhumiwa hao Februari 18, 2025, Kilakala, Manispaa ya Morogoro wakiwa na vifaa vinavyohusiana na biashara hiyo.
Watuhumiwa ni David Francis (35), Boazi Amboniye (42), Kundi Msalaba (31), Moses Dugomela (22), Isaya Paulo (25) na Baraka Sanga (32).
Msako huo umefanyika kwa kushirikiana na BoT, ikiwa ni sehemu ya kudhibiti utapeli wa fedha kupitia mitandao ya simu na teknolojia nyingine za kifedha.
Source: MwananchiDigital