Kufuaatia sintofaham inayoendelea nchini juu ya polisi kuuawa kizembe na majambazi huku wenyewe wakijiandaa kuua raia wanaodhamiria kutimiza takwa la kikatiba kuhusu maandamano na mikutano sept 1 kwa jina la ukuta; Haya ndio maoni yangu binafsi juu ya swala hili..
Na kwa kuanzia; nimejielekeza kumweleza kiongozi wa mapolisi kwa kuwa; kiongozi ndie dira ya chombo hiki..
Hii wizara inaongozwa na mmoja Wa mawaziri Vijana kabisa na anatajwa kuwa genius..
First class economist toka UDSM..
Anatajwa kuwa mmoja Wa warithi Wa JPM ndani ya CCM mwaka 2025..
Bila shaka; nilitegemea weledi Mkubwa sana Wa kuliendesha jeshi letu la polisi kwa usasa Zaidi; kisomi Zaidi; kiteknolojia Zaidi..
Sikutegemea angetumia njia zile zile za kugeuza polisi kuwa Adui Wa watu..
Polisi kutumia nguvu na silaha dhidi ya raia wema wasio na silaha na wasioasi..
Sikutegemea polisi wetu chini yake watumie intimidation techniques..
Nilitegemea kuona polisi huru wasiofungamanishwa na siasa uchwara zinazogawa watu (wao wapinxani na ss watawala)..
Kwa kinachoendelea juu ya UKUTA na matukio ya kihalifu Kila uchao (with reference ya Moshi juzi na jana dsm) ni dhahiri uendeshwaji wa jeshi letu ni business as usual..
Inaweza pia kuwa kielelezo cha kushindwa kwa waziri tunayeamini ni mahiri; msomi na kijana..
Inasikitisha sana Mtu Mwenye maono ya kuwa Amiri jeshi mkuu wetu anaendesha jeshi letu kisiasa na kuacha wakifa kizembe huku nguvu ikielekezwa UKUTA..
Inaonekana UKUTA wasio na silaha ni tishio kubwa kuliko MAJAMBAZI; wauza unga na wakwepa kodi..
Lazima Mwigulu kakaangu ajitafakari..
Akipitia mitandao ya kijamii; ataona jinsi RAIA waalivyokosa Upendo kwa polisi wao..
Vijana wanashabikia polisi kuuawa kinyama na maajambazi..
Ni ukatili kwa kiwango cha unyama..
Ila hii haijaja makisudi..
Ni zao la uendeshwaji mbovu Wa jeshi letu la polisi kwa mbinu za kikoloni..
Tuna polisi ambayo ipo integrated na watawala (CCM)..
Wamebebeshwa agenda ya kisiasa na wanatumikishwa kisiasa..
Adui Wa ccm ni adui Wa polisi..
Hii si Sawa..
Tusibadilika; si ajabu ya Tandahimba 2012 yatajitokeza tena mwaka huu..
Tandahimba polisi waliwindwa km kuku na RAIA..
Wakalazimika wahamishwe wote na kuletwa wapya 200 kufuatia mgogoro Wa polisi na RAIA..
Ni disaster..
We must change before the change finish us..
Na Ally Rama..