Jeshi la Polisi limetajwa zaidi ya mara 10 kwenye mahojiano ya Ayo na Deo Bonge. Message gani ilikuwa inatumwa kwa Watanzania?

Cute Wife

JF-Expert Member
Nov 17, 2023
1,272
3,548
Wakuu,

1731656721166.png

Kama mnavyokumbuka wakuu tukio la Deo Bonge lilitrend mtandaoni majuzi, huku tukio hilo likiwa limetoka Novemba 11, kama ambavyo taarifa ya polisi ilieleza.

Ayo TV walikwenda chap kwa kuanza kumhoji mmiliki wa hoteli, ambaye alitujuza yeye ndio alimugiza mfanyakazi mwingine aende kurekodi tukio hilo baada ya kukosa ushirikiano kwa watu hao waliokuja kumkamata.

Ayo pia walimfuata Deo kumhoji kuhusu tukio hilo na kueleza kinagaubaga ya nini hasa kilitokea mpaka kufikia hapo.

Maneno haya ndio yaliyotalawala kwenye mahojiano hayo: NALIAMINI Jeshi la Polisi, Jeshi la Polisi LITAFANYA kazi yao, TULIACHIE Jeshi la Polisi, TULIAMINI Jeshi la Polisi….

Tukiangalia Bunge na Jina la Samia likitatwa mara 30+ na mbunge/waziri mmoja kwenye mchango wa dk 3 tunapigia mstari chawa yupo kazini. Kwenye mahojiano haya, message ilikuwa inatumwa kwa Watanzania?
 
Watu wasiojulikana.
Deo Bonge hataki kabisa,kabisaa kuzungumzia hilo swali. Waachie Polisi. Anaongea kama yule mtu wa Dar 24,ambaye,by the way,uchunguzi bado unaendelea.
Lakini Deo Bonge ni mtu matata sana.
Alitoa video moja ambayo anasema yupo Sheikh wa Kiislamu amemshutumu Father Kitima.
Father Kitima aliposema nchi hii chawa wa Samia wanavuruga amani,hili jambo halijampendeza yule Sheikh.
Sasa Deo Kibonge anasema ( kwa sauti ya kufika) kwamba huyu Sheikh anataka kugombanisha Wakristu na Waislamu,hiyo haikubaliki
Pia Deo Kibonge anasema yule Sheikh analalamika kuhusu watabiri wanaosema Mungu amewaambia kwamba Hamtaki Samia 2025.
In fact,yupo mtabiri mmoja kule Arusha,Mungu anamwambia kila siku kwamba Hamtaki Samia 2025.
Sasa Deo Kibonge anasema ( kwa kufoka) kwamba huyu Sheikh anataka kugombanisha watu.
Na haya mambo Deo Kibonge anaongea huku amekaa kwenye stool ndefu kwenye counter ya bar( bar ya kunywa pombe).
 
Hayo ndio masharti waliyompa maybe. Kumbuka AYO pia ni mtu wa kutumika, ukizangatia tukio lilivyotokea vyombo vingi viliripoti isipokuwa yeye.
Lakini vyombo hivyo vyote vilivyoripoti awali hawajapata nafasi ya kumhoji Tarimo.

Ndio kusema nani wa kwenda kuhoji anapangwa, na nini aseme ndio hicho anachosisitiza kwamba ANAIMANI NA POLISI.
suala lipo STAGED/SCRIPTED
Ndio maaana tamko la msemaji wa tanpol bado linapikwa.
 
Hii nchi ni ya kindezi sana. Muhanga anatumika kusafisha wahaini wake.

Ukute kakutanishwa kabisa na hao kina Michael waliotaka kumteka na kufundishwa cha kusema kwa usalama wake mwenyewe.

Mwisho wa Millard na media yake utakuja kuwa mbaya sana. Amekuwa kama Zitto Kabwe likija swala la upinzani, Millard ni Zitto wa media.
 
Back
Top Bottom