Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 1,124
- 2,194
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam kwa kushirikiana na wananchi linaendelea kusimamia mifumo ya kiusalama ya kuzuia matukio ya kihalifu katika maeneo mbalimbali ya Jiji. Kwa ujumla hali ya Jiji ni salama.
Hata hivyo tarehe 24/04/2025 majira ya saa 5 asubuhi huko maeneo ya Cocobeach Oysterbay Kinondoni mtu mmoja mwanaume, ambaye hajafahamika jina wala makazi yake, anaye kadiriwa kuwa na umri wa miaka 30 hadi 35 alikutwa akiwa kwenye mchanga wa ufukwe wa bahari, hajitambui huku akiwa amefungwa bandeji nugu ya muda mrefu (PoP) kwenye mkono wake wa kulia.
Taarifa hiyo ilifikishwa Polisi na watu wanne wafanyabiashara ndogondogo wa eneo hilo ambao pia hawamtambui mtu huyo ambaye alipelekwa Hospitali ya Mwananyamala ambapo ilibainika kuwa alikuwa amekwisha fariki dunia na maiti hiyo imehifadhiwa Hospitali ya barabara ya Kilwa kutokana na matatizo ya nafasi ya kuhifadhi hospitali ya awali. Uchunguzi juu ya chanzo cha kifo hicho unaendelea.