Jeshi la Polisi lapekua nyumba ya Boniface Jacob, laenda na GJ Malisa Moshi kupekua nyumba yake

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,591
8,818
Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es Salaam bado linaendelea kuwashikilia Boniface Jacob na Godlisten Malisa. Wanatuhumiwa kwa makosa ya uchochezi na kuzua taharuki katika jamii.

Polisi wameondoka na Godlisten Malisa kwenda naye Moshi, Kilimanjaro usiku huu ili kufanya upekuzi nyumbani kwao wakitafuta simu ambayo polisi wamesema wanaitaka kwa ajili ya uchunguzi.

Polisi wamekwenda nyumbani kwa Boniface Jacob, Mbezi-Msakuzi, Dar es Salaam pia kufanya upekuzi ikiwa ni pamoja na kutafuta simu ambayo polisi wamesema wanahitaji ili kufanya uchunguzi.

Jeshi la polisi limesema kwamba wao ndiyo walalamikaji katika jambo hili, na kwamba Boniface Jacob na Godlisten Malisa wamefanya uchochezi na kuzua taharuki katika jamii dhidi ya Jeshi la Polisi.

Pia, jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es Saalam limesema kwamba, kuna makachero wa jeshi la Polisi kutoka mkoa wa Arusha ambao wanatoka Arusha kuja Dar es Saalam ili kumuhoji Boniface Jacob.

Tuteendelea kuwajulisha kwa ambayo yanaendelea. MSIOGOPE. MSIOGOPE. MSIOGOPE. MSIOGOPE.

MMM, Mtikila.

PIA SOMA
- Kamanda Muliro: Malisa GJ, Boniface Jacob wakamatwe kwa tuhuma za kupotosha taarifa za kifo cha Robart Mushi

- Boniface Jackob afika kituo cha Polisi cha Oysterbay ili akamatwe kama alivyoagiza RPC

- Hatimaye Malissa na Boniface Jackob waachiwa kwa dhamana
 
Wako watu walipendekeza Jeshi la Polisi Livunjwe na Kuundwa upya , lengo likiwa ni kuliboresha kwa kutimua hawa waliopo wenye akili za kizamani wakiwemo akina Muliro na wenzake na kuleta Askari wapya wenye akili ya kisasa .

Mwanzo nilipinga wazo hili lakini sasa naamini waliowaza vile waliona Mbali sana .

Anayetuhumiwa kupotosha mitandaoni amekuja ili mumuonyeshe upotoshaji wake halafu mnaenda kupekuwa nyumbani kwake ili mupate upotoshaji kwenye makabati au mnataka kukagua thamani ya nyumba yake ? Hivi ndivyo Police wa Nchi zote wanavyofanya au ni hawa wa CCP MOSHI pekee ?

Screenshot_2024-04-25-19-13-27-1.png
 
Back
Top Bottom