Jeshi la Polisi lakamata Wafanyabiashara watatu wakituhumiwa kuuzaji pombe bandia Ruvuma

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,594
13,274
ru2.jpg

Hali ya ulinzi na usalama Mkoa wa Ruvuma ni shwari, na ushwari huu umetokana na ushirikiano mzuri uliopo baina ya Jeshi la Polisi na wananchi kuhakikisha jamii na Mkoa kwa ujumla unaendelea kuwa salama.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma linapenda kutoa taarifa ya mafanikio ya doria, misako, operesheni kwa kipindi cha mwezi Machi hadi Aprili 2024 kama ifuatavyo;

Kupitia misako, doria na Opereshi mbalimbali zinazoendelea kufanyika kwa kipindi tajwa hapo juu katika wilaya ya Mbinga, Jeshi la Polisi Mkoa wa kwa kushirikiana na Maafisa wa TRA tulifanikiwa kukamata jumla ya wafanyabiashara 03 ambao majina yao yamehifadhiwa kwa sababu za kiupelelezi waliokuwa wakijihusisha na biashara haramu ya uuzaji wa pombe bandia wakiwa na jumla ya Maboksi 131 ya bidhaa bandia za vinywaji vikali aina ya Smart gin ambayo walikuwa wamehifadhi katika stoo za maduka yao pamoja na chupa za pombe aina tofautitofauti 36 ikiwa, Master 12 , Elephant Gin 16, Café Kahawa 08 na Double Vibe 03 ambazo zilikuwa zikiuzwa kwa wananchi kitendo ambacho ni kinyume cha sheria.
ru3.jpg

Ru1.jpg
Pia kupitia Operesheni zinazoendelea kufanyika Mkoani Ruvuma huko katiki vijiji vya Nambecha – Mkuyuni, Kata ya Mgombasi na kijiji cha Njalamatata kata ya Mkongo Wilaya ya Namtumbo na Kijiji cha Ndongosi – Muhukuru Halmashauri ya Songea Vijijini tuliwakamata jumla ya watuhumiwa watatu (05) ambao majina yao yamehifadhiwa na kuteketeza mashamba ya bhangi jumla ya hekari tano (05) ambazo walikuwa wamelima kwa kuchanganya na mazao mengine ya Soya, Tumbaku, Mpunga, Mahindi na maharage.

Aidha katika misako tuliyoifanya katika maeneo yote ya Mkoa wa Ruvuma tulifanikiwa kukamata watuhumiwa 23 wakiwa na dawa za kulevya aina ya Bangi wakiwa na jumla ya Kete 472, Bhangi kavu yenye uzito wa 107Kg, Mbegu za bhangi 6 Kg na Mtuhumiwa Moja akiwa na madawa ya kulevya yadhaniwayo kuwa Heroine jumla ya kete 03.

Vilevile Kupitia Operesheni zinazoendelea kufanyika Mkoa wa Ruvuma, tarehe 13.04.2024 katika Mtaa wa Hoa Hoa Wilaya ya Mbinga Jeshi la Polisi tulifanikiwa kumkamata mwanaume mmoja aliyetambulika kwa majina Edmund Kelvin Komba, (34), Mkazi wa Mtaa wa Hoahoa Mbinga akiwa na Dazani mbili za milipko (baruti) aina ya Super Powder 90 zenye 12PC kila Dazani kinyume cha sheria. Mtuhumiwa amefikishwa Mahakamani kwa hataua za kisheria.

Sambamba na hilo Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma Kwa upande wa mafanikio ya kesi za Mahakamani tumefanikiwa kuwafikisha mahakamani jumla ya watuhumiwa 12 wa Makosa Makubwa wakihusishwa na tuhuma mbalimbali ambapo Mtuhumiwa 01 wa kosa ya mauaji alikuhukimwa kunyongwa hadi kufa, watuhumiwa 02 wa kosa la kubaka walikuhukumiwa miaka 30 jela kila mmoja, Mtuhumiwa 01 wa kosa la kubaka alihukumiwa kifungo cha maisha jela, Watuhumiwa 02 wa kosa la kupatikana na nyara za serikali walihukumiwa kifungo cha Miaka 20 jela kila mmoja, Mtuhumiwa 01 wa kosa la wizi alihukumiwa miaka 30 jela,

Sanjari na hilo Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma kupitia Operesheni na Misako tulifanikiwa kumkamata Alpha Christopher Minja, (32), Mchaga, Mkazi wa Sanawari Arusha ambaye alikuwa akijihusisha na makosa ya unyang’anyi na wizi ndani ya magari akiwa na jumla ya Raptop 10 ambazo aliziiba maeneo mbalimbali Mkoani Ruvuma.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma linatoa wito kwa raia wema kuendelee kushirirkiana na Jeshi la Polisi katika kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ili waweze kushughulikiwa kwa mujibu wa sheria na Mkoa wetu uendelee kuwa salama wakati wote.

Aidha, niwatake Wananchi kuhakikisha wanaepuka kujihusisha na biashara haramu ambazo ni kinyume cha sheria za Nchi, badala yake niwaombe kujikita katika kufanya biashara halali za zitakazowasaidia kuwa vipato ambavyo vitaleta tija kwao na Jamii kwa ujumla.

Imetolewa na,
Marco G. Chilya – SACP
Kamanda wa Polisi (M) Ruvuma.
 
Pombe bandia au zimeingizwa kinyume na utaratibu?

Kama wanywaji wakinywa wanalewa, how come zinakuwa bandia?
 
Back
Top Bottom