Jeshi la Polisi laahidi kutoa ushirikiano Maandamano ya CHADEMA (MWANZA)

Mjanja M1

JF-Expert Member
Oct 7, 2018
4,023
14,190
Wakati Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kikitarajia kufanya maandanamano ya amani jijini Mwanza Februari 15 mwaka huu, Jeshi la Polisi limetoa rai kwa viongozi na wafuasi wa chama hicho kuwa wanalo jukumu mahsusi la kuhakikisha wanazuia lugha za uchochezi, kejeli na matusi kwa viongozi wa serikali, sambamba na kujizuia kutoa lugha zinazoweza kusababisha uvunjifu wa amani kwa jamii

Barua ya Jeshi hilo yenye Kumb. Namb. EA.740/794/01/5 iliyotumwa CHADEMA leo, Jumanne Februari 13.2024 imeeleza kuwa maandanamano hayo yasisababishe uvunjifu wa amani, watu kuibiwa, kuporwa au kuharibiwa mali zao hivyo wahusika wameelekezwa kupita kwenye Barabara walizoomba ambazo ni Barabara ya Kenyatta kuanzia eneo la Buhongwa senta, Mkolani, Nyegezi, Butimba, Mkuyuni, Igogo, Nyamagana na Isamilo, sambamba na Barabara ya Nyerere ambayo wanatakiwa kuanzia Igoma senta, Mhandu, Mabatini, Nata, Nyerere Plaza, Mataa na Nyamagana

Barua hiyo ambayo imesainiwa na Kaimu Mkuu wa Polisi (W) Nyamagana Apolinary A. Ndibaika -SP imeendelea kufafanua kuwa katika makutano ya Barabara za Kenyatta na Nyerere viongozi na waandamanaji hawataruhusiwa kufanya mkutano wa hadhara mahali hapo hadi watakapofika uwanja wa Furahisha

Aidha, Barua hiyo ambayo nakala zake zimepelekwa kwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza na Mkuu wa wilaya ya Nyamagana imewataka CHADEMA kutumia upande mmoja wa Barabara ili kuruhusu watumiaji wengine wa Barabara kuendelea na shughuli zao

Pia, CHADEMA wamekumbushwa kuzingatia muda wa kuanza na kumalizika kama ilivyoainishwa kwenye Barua ya CHADEMA iliyotumwa awali wa Jeshi la Polisi, hiyo ikienda sambamba na kutoanzisha mambo mengine ambayo hayamo kwenye taarifa iliyotolewa Polisi

20240213_162849.jpg


20240213_162854.jpg
 
Ni jambo jema , ingekuwa kipindi kile cha shetwani na wafuasi wake bc tungesikia kuwa interejensia inaonyesha chadema mnataka kuyatumia maandamano kuipindua serikali ya chatto..... kila la heri ndg zetu wa mwanza mi nayasubiria ya hapa mbeya mjini tarehe 20/2/2024 ..... kutoka niliko huku makongorosi hadi mby ni masaa tu.....people'sssssssssss
 
Dsm mlienda umoja wa mataifa hizo sheria mbona zilipitishwa
Mnahangaika bure
 
Tunataka mabilion ya Millenium toka Nchini Marekani

kuna Wahuni wamehongwa waandamane ili tupate picha za kuonesha Wazungu

wakati wa JK iliruhusiwa mivurugu vurugu ya Katiba mpya tukapigwa billion 700
 
Back
Top Bottom