Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,965
- 13,739
Akitoa taarifa hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Kamishna Msaidizi wa Polisi, ACP Justine Masejo amesema Katika kuhakikisha sikukuu hizo zinasherekewa kwa amani na utulivu Jeshi hilo litahakikisha linatoa ulinzi kwenye nyumba za ibada, kumbi za starehe pamoja na maeneo mengine yote Katika Mkoa huo ambapo askari watapangwa katika doria za miguu, pikipiki, magari na doria za mbwa katika Jiji la Arusha lakini pia Mkoa kwa jumla.
ACP Masejo ametumia fursa hiyo kuwatakia Wananchi wote wa Mkoa wa Arusha na wageni walifika katika Mkoa huo Kheri ya Krismas na Mwaka Mpya 2024 huku akiwakumbusha kauli mbiu isemayo ulinzi unaanza na mimi.
Sambamba na hilo amewapa angalizo kufanya vitu kwa kiasi, bila kuvuka viwango wala mipaka ambayo inaweza kusababisha wakaingia mwaka mpya wakiwa na changamoto zilizosababishwa na furaha iliyopitiliza.