Jerry Muro analiaribu soka la Tanzania, wahusika mtazameni kwa umakini.

TAWA

JF-Expert Member
Jun 23, 2013
3,673
1,571
Huyu jamaa amekuwa anaongea saña wakati mwingine anaongea maneno ambayo si ya kiuana michezo.
Hivi karibuni ametokea kuiropokea TFF kuwa waliwafanyia makusudi katika maandalizi ya mechi yao dhidi ya Mo Bejaia iliyofanyika Algeria eti kwamba TFF ilificha vifaa ambavyo CAF walitoa kwa ajili ya mechi hiyo.
Leo ameibuka na kuilaumu tena TFF na Azam media kuwa wanawahujumu katika kuelekea mechi yao dhidi ya mazembe.
Kuna kipindi alionesha hadharani mbele ya vyombo vya habari kumnyanyapaa msemaji wa simba kutokana na hali yake (Albinism).
My take:
Huyu si mwanamichezo, wanaohusika naye hebu wamtazame kwa jicho lingine. Ipo siku atasababisha mgogoro ambao utalighalimu soka la Tanzania.
Ninaomba moderators uzi wangu huu uwekwe katika kumbukumbu,
 
TFF ndio wanaoharibu mpira wa Tanzania. Muro anaongea hivyo kwavile anaipenda Yanga lkn hao TFF hawana upendo na Yanga wala timu ya taifa. Yanga walipambana kufika hapo walipofika pamoja na figisu figisu kutoka TFF za kuilazimisha Yanga kucheza mechi nyingi za viporo kwa karibu karibu huku wakikabiliwa na mechi za kimataifa. Figisu la mwisho TFF kutaka kuifanyia Yanga ili kuwavuruga wasifanye vizuri ktk mechi za kimataifa ilikuwa kulazimisha uchaguzi usimamiwe na wao TFF halafu waje kumkata Manji wakati wa kurudisha fomu na kumpitisha mtu wao wakijua kabisa huyo mtu wao asingekubalika na Wana Yanga na mgogoro ndio ungeibukia hapo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…