The Phylosopher
JF-Expert Member
- Mar 11, 2015
- 1,930
- 2,909
Mtangazaji wa kituo cha redio cha Wasafi FM amshambulia mtangazaji wa kituo cha redio DW ya Ujerumani, kwamba huyo mtangazaji alikosea sana namna alivyoripoti tamasha la kizimkazi.
Akizungumza katika kipindi cha asubuhi huku akikwepa kutaja jina la mtangazaji na kituo anachotangazia lakini akinukuu mambo aliyoyasema, Hando alisema tamasha la kizimkazi lina manufaa makubwa sana kwani limepelekea kupatikana Kwa huduma muhimu mjini humo na hivyo kukuza utalii.
Ingawa hakumtaja kwa jina mtangazaji huyo wala kituo cha redio alichotangazia, ila nilibahatika kumsikiliza Salma Said wa DW alipokuwa anazungumzia tamasha hilo, alisema limetumia mabilioni ya pesa mithili ya yale yaliyotumika kijijini chato wakati wa mtangulizi wa Samia.
Kwa mtazamo wa mtangazaji ni kama uharibifu wa fedha za umma.