MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,991
Soma vizuri bandiko langu!Unasema werema kapewa ulaji mbona hutwambii ni nafasi gani kapewa? Hii hekaya ya kusadikika kwa kuunganisha dot ukimpelekea Kubenea atakulipa vizuri maana mkiiuza front page mtayakamata manyumbu ya kutosha.
What is research?No research no right to speak keep quiet and shuuuutt upppp
Inawezekana hali hii haiwezi kubadilika!Bora hii 2015 iende zake sasa maana imetuvurugia sana afya ya mijadala hapa JF
Soma vizuri Ujaji Ulaji??Unasema werema kapewa ulaji mbona hutwambii ni nafasi gani kapewa? Hii hekaya ya kusadikika kwa kuunganisha dot ukimpelekea Kubenea atakulipa vizuri maana mkiiuza front page mtayakamata manyumbu ya kutosha.
Mkuu kama kiongozi umepata nafasi kwa waliokuwa nawe kutumia ushirikina basi hata wewe uwe mlokole kwenye hilo nawe ni mshirikina tuu. Hivyo hivyo Pesa za wizi au Rushwa na hadaa.Tulisema tatizo ni mfumo,mnajionea wenyewe
Ni kweli mkuu watu kwa uzembe wa kushirikisha akili katika maswala walikuwa na matumaini makubwa sana kiasi cha kuwa tayari kugombana na mtu yeyote anayemkosoa Dr.Magufuli lakin kwasasa taratibu wameanza kuelewa,hizo ndio hela za press conference pale SERENA HOTEL..Mkuu kama kiongozi umepata nafasi kwa waliokuwa nawe kutumia ushirikina basi hata wewe uwe mlokole kwenye hilo nawe ni mshirikina tuu. Hivyo hivyo Pesa za wizi au Rushwa na hadaa.
Matokeo ya fedha za ESCROW na kauli zile za Muhongo za kutishia kumwaga Michele na hatimae yeye na Katibu wake kutulizwa no wazi Pesa zile zilipigwa ili zitumike kwenye kampeni.
Hili linaondoa utakatifu anaotaka JPM kujinadi nao eti sijapokea hela ya mfanyabiashara yeyote kwenye kampeni.
Sawa lakini zile Rumbesa za Stanbic ndizo zilikuwa zinamlipia chakula, petrol, posho za watukanaji kina Bulembo, posho za wakata viuno na burudani kina Wema na mengine mengi tuu.
Usafi anaojinadi nao uko wapi?
Kurudishwa kwa Prof. Muhongo na pia aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliachim Maswi kumezua maswali ambayo yanahitaji majibu mbadala!
Nisingepata maswali kama wangerudishwa na Serikali ya Rais Kikwete kutokana na historia yake kiutendaji lakini ninapatwa na maswali baada ya kurudishwa kwenye nafasi za juu za kisiasa katika serikali ya Rais Magufuli ambayo inajipambanua na nimeiona ni no-nonsense, results-driven government.
Kwa alichokifanya Rais Magufuli na historia aliyonayo ndani ya serikali, uteuzi wa Prof. Muhongo na Maswi unatoa picha nyingine kwenye kadhia ya Tegeta Escrow Account.
Wakati wa sakata la Tegeta Escrow account, Kumbukumbu zinaonyesha Prof. Muhongo aliwahi kusema hawezi kujiudhuru na kama ikitokea hivyo basi nchi itatikisika.Kwa maana nyingine, alikuwa amebeba bomu kubwa la kisiasa ambalo alikuwa tayari kuripua iwapo atashinikizwa kujiudhuru hata hivyo inaonekana alishauriwa na watu wa ‘’kitengo’’, akajiudhuru ili kulinda heshima ya serikali kwa matarajio ya baadaye.
Hata aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliachim Maswi aliwahi kusema hahusiki na sakata hili bali alifanya kazi kama alivyoshauriwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Fredrick Werema.
Maswi baada ya kusafishwa na tume ya maadili, aliteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara huku Prof. Muhongo akijikita kutafuta nafasi ya kuteuliwa kuwa mgombea Urais na ubunge kwa tiketi ya CCM.
Aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Fredrick Werema alikiri hata ndani ya Bunge, kuwa ni kweli kuwa alitoa ushauri kwa mamlaka ya juu ili kuidhinisha fedha kutolewa na kwa maana hiyo yuko tayari kubeba msalaba wa Prof Muhongo na Maswi. Kwa sasa amerudi kwenye kazi yake ya Ujaji.
Mpaka sasa tunachofahamu ni kuwa, pesa zilichukuliwa lakini hatufahamu nani aliyechukua na kuweka kwenye ‘’mifuko ya lambo’’ na lumbesa katika Benki ya Stanbic, lakini kikubwa zaidi, hizo pesa zilienda wapi?
Uchunguzi wa sakata hili mpaka sasa ‘’haujamalizika’’ lakini waliowajibika kisiasa wamerudishwa katika nafasi za juu nchini.
Kwa yanayofanyika kwa sasa, kuna hatari na uwezekano tulikuwa tunacheza ngoma ya kisiasa ambayo hatufahamu mapigo yake achilia mbali wapigaji wake.
Hizi teuzi zinaacha maswali mengi bila majibu!
Ama kweli usilolijua...

Ama kweli usilolijua]
Kuna maswali mengi yanahitaji majibu kwenye suala la Tegeta Escrow Account!labda. ngoja tusubili tuone kuna nini tena. Make kwa style hii unaweza kusikia wa chenji za rada na wa pesa ya mboga nao wanaula.
SFO walisham clear huyo mnayetuhumu rada. Tafuta gia nyingine mkuu. Cheap politics ndio zinazoiua nchi hii.labda. ngoja tusubili tuone kuna nini tena. Make kwa style hii unaweza kusikia wa chenji za rada na wa pesa ya mboga nao wanaula.
Inawezekana unayoyasema ni kweli!Msiyoyajua ni mengi kuliko muyajuayo,HAPPY NEW YEAR.