GadoTz
JF-Expert Member
- Nov 20, 2014
- 370
- 636
WCB moja ya lebo zilizofanya vizuri na wanaendelea kufanya vizuri kwenye kiwanda cha muziki Tanzania na hata nje ya mipaka.
Ila hapa kati ni kama lebo ilianza kudorola haswa baada ya kuondoka wasanii wao powerful, Harmonize na Rayvanny.
Ile nguvu ya WCB kuisikia kila kona ya nchi imepungua sana.
Walau Zuchu na Mbosso ndio walibaki kama mihimili ya lebo.
Sasa nimesikia Mbosso tayari kaondoka Wasafi na washamalizana na Diamond yupo huru.
Pia Lavalava mkataba wake umefika mwisho muda wowote wanamalizana na WCB.
Kwa mantiki hiyo Wasafi itabaki na wasanii wawili, Zuchu na D Voice ambae hafanyi vizuri bado. Kwa kifupi WCB ipo kwenye kilele kinachofata ni kudondoka.
Sasa ili isidondoke inatakiwa kufanya nini? Wanatakiwa kubadilisha ladha na kuendana na zama mpya za muziki (new generation).
WCB inatakiwa kubadilisha kuanzia management mpaka wasanii, yani inatakiwa kuzaliwa upya, ionekane mpya machoni na masikioni kwa watu.
Refreshment hii sio kuondoa wasanii waliobaki bali kuongeza wengine wenye ladha tofauti.
Nimeona Laizer ameweka tangazo wanatafuta wasanii wapya na ametoa details za wasanii kutuma profile na kazi zao. Well and good, lakini kwa sasa wanahitaji zaidi ya wasanii wapya wanahitaji pia ladha mpya.
Baibuda ndio imekuwa kama identity ya WCB lakini kwa sasa nafikiri wangejaribu kuleta pia aina nyingine ya muziki kama fusion ya choir na afro pop kwa mtazamo wangu wasanii wanaoimba huu muziki ni dili kwenye soko la Africa. Lakini pia wangejaribu kuleta msanii wa kumuuza kwenye international market ambae anaweza akapanda majukwaa makubwa Africa na akasound kama wenzie kwenye majukwaa asiwe msanii wa playback.
Kibishara sidhani kama ni sahihi kumchukua msanii kama Aslay kama tetesi zinavyosema nafikiri waingize damu changa tupu, though itachukua muda kupromoti wasanii wapya ila ina uhai kwenye biashara.
Don Jazzy alishawai kutumia hii formula akaja na kina Rema, Ladpoe na Ayrastarr baada ya kina Tiwa savage kusepa, Rema na Ayrastarr wamemlipa sana Don Jazzy.
Kwa hiyo Diamond kwenye hii refresh anayotaka kufanya aangalie sura mpya na radha mpya, kuna wasanii kama Ivra na Treysa (sina hakika na spelling), wanajua na wanaweza kufanya vizuri wakipata usimamizi wa lebo kubwa kama Wasafi.
Lakini pia atafute ghost writers kama Don Jazzy pale Marvin ana waandishi kama kumi kazi yao ni kuandika tu, japo falsafa ya WCB inataka msanii anaeweza kuandika mwenyewe lakini waandishi wanasaidia kubadilisha fleva za msanii anakuwa achoshi kumskiliza hata akikaa kwenye muziki muda mrefu.
Kwa sasa WCB naweza kusema ipo kwenye nafasi mbili kuimalika na kuzidi kuwa powerful au kudondoka kabisa na kupotea.
Inategemea na maamuzi atayofanya Diamond.