Je, wajua ulimwengu ukupao kila kitu utakacho katika kanuni asili ya maumbile? Sehemu ya pili

Apiov

Platinum Member
Nov 13, 2023
8
37
JE WAJUA ULIMWENGU UKUPAO KILA KITU UTAKACHO KATIKA KANUNI ASILI YA MAUMBILE? - SEHEMU YA PILI

Leo katika mwendelezo wa mada hii, tutaangazia Kanuni nyingine ya Hermes. Katika sehemu ya kwanza tuliona Kanuni za Chini Juu, Juu Chini na Kanuni ya Mtetemo. Ahsanteni kwa nyote mliovutiwa na Mada hii hata mkanifikia na kuomba mwendelezo. Kwa kuwa maarifa si mali yetu binafsi, basi nami sina budi kuyatoa kwenu kama nilivyopewa na watu wengine kwa njia mbalimbali za kujifunza na Tahajudi.

Kanuni yetu ya leo ni Kanuni ya ‘Uwili’ au kwa kimombo ni (Principle of Polarity)

Kanuni hii inasema kuwa: “ uwepo wa Kila kitu katika Ulimwengu ni katika Uwili. Kila kitu kinarindima ndani na nje, kila kitu kinakuwepo na kutokuwepo. Kila kitu kina mfanano wa tofauti yake yaani (Everything has its pair of opposite). Yaani vitu visivyofanana maana yake vinafanana! Naam kadili unavyovipa utofauti, ndivyo unavyovifananisha. Ndio maana tunafananisha ni gari gani linakimbia kuliko lingine; na sio gari gani linakimbia kuliko pilau.! Utofauti ni Ufanano katika asili, isipokuwa ni tofauti katika nyuzi tu.

Kwa jinsi hii ni sawa na kusema kuwa Kweli zote ni Nusu kweli tu… kwa maana ili kitu kiwe kweli ni lazima uvuke nusu ya Uongo, kwa hiyo nusu ya pili baada ya nusu ya Uongo ndio tunaita Ukweli. Na hivyo hivyo Uongo ni nusu Ukweli... kumbe hata barafu ni nusu ya joto na ndio maana barafu ikizidi sana inaweza kukuletea madhara kama ambavyo ungeshika kitu chenye joto kali. Naam hivyo basi, hata mikanganyiko yote huweza kusuluhishwa.

Kanuni nyingine ni ile maarufu ya Sababu na Matokeo (Principle of Cause and Effect) Mwanafalsafa wa Kigiriki Aristole, aliita Kanununi hii Causality Principle. Yaani kanunu ya Usababishi. Ambapo yeye alieleza jinsi Mwanadamu anavyoweza kuelewa sababu Kanuni ya sababu ya uwepo wa maumbile maada ya asili. Katika aina zake 4 za Sababu, anataja sababu moja kubwa yaani (Final Cause) kama sababu ya kila kitu kuwepo.

Turudi kwa Hermes sasa;
Kanuni hii inasema kwamba—kila kitu kina sababu na kila sababu ina matokeo yake, kila kinachotokea hutokea kutokana na kanuni. Hata pale tunaposema kitu fulani kimetokea kwa nasibu tu, ni kwasababu tumekua hatuijui Kanuni husika. Huenda Nasibu ndio ikawa jina la Sheria hii. Kusema hivyo, ni sawa na kusema kwamba, hakuna kinachotokea nje ya Kanuni.

Katika Sayansi ya kisasa hasa inayotumia methodolojia ya kuthibitisha mienendo ya maumbo asili, hutumia sana kanuni hii ya Usababishi. Kwamba hupima ni jinsi gani kitu fulani kimetokea? Wanaanza kufatilia kisababishi. Lakini mara nyingi ni mpaka waone matokeo. Ndio maana baadhi yao hukataa dhana mbalimbali ambazo haziwezi kupimwa na kufatiliwa chanzo chake. Wanakubali kile tu ambacho kita survive lab test! Ukienda mbali zaidi, huu pia ndio msingi wa Logic. Kwamba vitu vitokee kwa mfuatano unaoeleweka. Kwamba A izalishe B na B izalishe C na C izalishe D nk.

Je, umewahi kusikia maneno kama malipo ni hapa hapa Duniani? Kwamba Duniani wawili wawili? Kwamba hakuna kinachotokea hivi hivi? Kule China, katika utamaduni wao wana msemo unaosema kwamba “Good fortune comes in pair”, haya yote huonesha nguvu ya Kanuni hii ya pair au mfanano lakini pia kanununi ya Cause and Effect kwamba kila kitu kimesababishwa, na Matokeo ni kile Kilichosababishwa.

Katika Ulimwengu wa Kisomi katika mijadala ya Kifalsafa na Kisayansi, Kanuni hizi zinapata misuko suko ya kupingwa. Ni kawaida hili. Mfano hiyo Kanuni ya (Cause and Effect) ilipingwa sana na Magwiji wa Falsafa kama David Hume, Immanuel Kant nk.

Mfano, David Hume alisema kwamba Kanuni ya uwepo haiwezi kuthibitika kwa macho ya nyama kwa kuwa hatuoni ni wakati gani A anasababisha kutokea kwa B. Ila tunachoona ni A anakuwepo na B anakuwepo. Lakini Kant yeye alisema Kanuni hii inawezekana kwa Vitu onekana pekee lakini si kwa vitu visivyoonekana. (Yaani vitu vilivyo katika vyenyewe).

Mpenzi Msomaji, Kanuni hizi zinatufunza nini katika maisha yetu ya kila siku? Huenda kanuni ya mfanano ikatupa ujasiri juu ya kutokujiona tupe peke yetu katika challenges mbalimbali tunazopitia, au mafaniko fulani tuliyonayo. Kwamba hakuna kitu cha pekee, angalau kila kitu kina mwenzake mahali fulani. Lakini pia huenda ikatufunza kuwa hakuna tatizo lolote lisilotatulika na kuletwa katika uwiano sawa na kinyume chake. Maana tumeona kuwa tofauti si tofauti bali ni mfanano, barafu si barafu bali ni joto/moto na kinyume chake ni sahihi.

Katika kanuni ya Usababishi, huenda inatufunza kuwa tunaweza kutatua changamoto za ulimwengu huu na zile za binafsi kwa kufatilia chanzo halisi cha matatizo hayo. Kwani matatizo kama tulivyoona ni matokeo tu.

Shukrani kwa kujipa muda na kumakinika na mada hii. Natumai tutaonana tena katika Makala ijayo ya mwendelezo wa Mada yetu, panapo Majaaliwa.

Apiov Lwiwa, PhD
Doctor of Philosophy in Philosophy
 
Ahsante sana mkuu.
 
Back
Top Bottom