Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,340
- 120,880
Wanabodi,
CCM ni yule mwenye 10 aliyepoteza moja akabakiwa na 9,na upinzani ni yule aliyekuwa hana kitu akapata ile moja!。
CCM ni yule mwana mwema na upinzani ni mwana mpotevu aliyerejea nyumbani。
Watanzania wapenda haki wote,wana kila sababu ya kufurahia matokeo haya ya uchaguzi wa serikali za mitaa ambayo yanathibitisha lolote linawezekana 2025。
Uchaguzi wa serikali za mitaa umekwisha, hii ni makala ya pongezi kwa walioshinda na pole kwa walioshindwa.
Matokeo ya jumla ni kama ifuatavyo
i) Nafasi za Mwenyekiti wa Kijiji:
CCM imeshinda vijiji 12,150 sawa na asilimia 99.01, Wapinzani wameshinda vijiji 121 sawa na asilimia 0.09. Tukilinganisha na matokeo ya 2019, japo CCM ndie mshindi wa jumla, na wapinzani wameshindwa, lakini ukweli ni CCM imepoteza vijiji 121 ilivyokuwa inavishikilia, hivyo wapinzani wameshinda vijiji 121.
ii) Nafasi za Mwenyekiti wa Mtaa:
CCM imeshinda mitaa 4,213 sawa na asilimia 98.83, Wapinzani wameshinda mitaa 50 sawa na asilimia 1.17. Tukilinganisha na matokeo ya 2019, japo CCM ndie mshindi wa jumla, na wapinzani wameshindwa, lakini ukweli ni CCM imepoteza mitaa 50 ilivyokuwa inaishikilia, hivyo wapinzani wameshinda mitaa 50.
iii) Nafasi za Mwenyekiti wa Kitongoji:
CCM imeshinda vitongoji 62,728 sawa na asilimia 98.26, wapinzani wameshinda vitongoji 2,000 sawa na asilimia 1.74. Tukilinganisha na matokeo ya 2019, japo CCM ndie mshindi wa jumla, na wapinzani wameshindwa, lakini ukweli ni CCM imepoteza vitongoji 2,000 ilivyokuwa inaishikilia, hivyo wapinzani wameshinda vitongoji hivyo 2,000.
iv) Nafasi za Wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji:
CCM imeshinda nafasi 229,075 sawa na asilimia 99.31, wapinzani wameshinda nafasi 1,580 sawa na asilimia 0.69. Tukilinganisha na matokeo ya 2019, japo CCM ndie mshindi wa jumla, na wapinzani wameshindwa, lakini ukweli ni CCM imepoteza wajumbe 1,580 hivyo wapinzani wameshinda wajumbe 1,580.
v) Nafasi za Wajumbe wa Kamati ya Mtaa:
CCM imeshinda nafasi 21,148 sawa na asilimia 99.30, wapinzani wameshinda nafasi 150 sawa na asilimia 0.70. Tukilinganisha na matokeo ya 2019, japo CCM ndie mshindi wa jumla, na wapinzani wameshindwa, lakini ukweli ni CCM imepoteza wajumbe 150 hivyo wapinzani wamemeshinda wajumbe 150.
Ushindi wa jumla wa CCM ni nafasi 329,314 na kupoteza nafasi 3,901 ambazo zimenyakuliwa na upinzani, hivyo kwenye gainers na looses, CCM ndio wame loose na upinzani wame gain, ukilinganisha na uchaguzi wa 2019, kila aliyesimamishwa na CCM alishinda, hii inamaanisha, ikitolewa elimu ya kutosha ya uraia, ule mtindo wa Watanzania kuchagua kwa mazoea tuu utapungua, Watu watajengewa uwezo wa kuchagua kwa kufanya kitu kinachoitwa informed decisions, hivyo uchaguzi mkuu wa 2025, Wapinzani wakisimamisha wagombea wazuri kuliko wagombea wa CCM kwenye ubunge na udiwani, Watanzania, watawachagua, hivyo kupata tena Bunge lenye kambi ya upinzania, hivyo kuisimamia serikali kikamilifu.
Nitoe pongezi kwa CCM, chama kubwa, chama bingwa kwa ushindi mkubwa wa kushinda nafasi 329,314 kilioupata katika uchaguzi huu, lakini pia nitoe pole kwa CCM kupoteza nafasi 3,901 ambazo ilikuwa nazo,sasa omezipoteza。na。 zimeshikwa na upinzani, na kutoa pole kwa upinzani kushindwa na CCM, lakini pia pongezi upinzani kuwapokonya CCM nafasi 3,901 ambazo CCM ilikuwa inazishikilia sasa zimeshikwa na upinzani. Kushinda ni kushinda tuu, kuna raha yake, na kushindwa pia ni kushindwa, kuna maumivivu yake, hongereni CCM na Wapinzani kwa kushinda, wote mmeshinda, na poleni CCM na Wapinzani kwa mlicho poteza, wote mmeshinda na mmeshindwa.
Nitoe pongezi kwa vyama vyote vilivyoshiriki uchaguzi huu vizuri kwa kunadi sera zao na kufanya kampeni za kiungwana na kistaarabu, na pia nitoe pole kwa rabsha rabsha na maafa yaliyotokea, ukiwemo uvujaji wa machozi, jasho na damu.
Nisiwe mtovu wa shukrani kwa kidogo ili tupatiwe kikubwa, japo mpaka sasa bado sijajua kilitokea nini kwenye sheria mpya ya uchaguzi, iliifuta sheria ya uchaguzi wa serikali za mitaa, na kuunda sheria moja ya uchaguzi chini ya tume huru ya uchaguzi. Kwanza nitoe pongezi za dhati kwa kiongozi wetu Mkuu Rais Samia, kutupatia sheria mpya ya uchaguzi, kwa vile Rais Samia sio mwanasheria, naomba niendelee kumsisitizia, hii sheria yetu mpya ya uchaguzi ni sheria batili, inakwenda kinyume na katiba ya JMT. Naomba tuirekebishe kabla ya uchaguzi mkuu wa 2025.
Pia tushukuru kwa Tume huru ya Uchaguzi, Watanzania walitaka Tume Huru na shirikishi ya uchaguzi, hii tume ya uchaguzi, badi ni tume ile ile, ila jina ndio limebadilishwa kuitwa Tume Huru, Watanzania hatukutaka mabadiliko ya jina la Tume ya Uchaguzi, kutoka, Tume ya Uchaguzi kuwa Tume Huru ya Uchaguzi, tunaomba mabadiliko ya Tume ya Uchaguzi kuwa ni tume huru na shirikishi ya uchaguzi.
Nashauri tuyatumie mapungufu tulioyaona kwenye uchaguzi huu kama shamba darasa la chaguzi zijazo, mimi nikisisitiza elimu ya uraia kutolewa kikamilifu. Mimi nikiwa ni mmiliki wa kampuni ya uaandaaji wa maudhui, kufuati nguvu ya mitandao ya kijamii, hakuna sababu ya kusubiri vipindi virushwe kwenye TV au redio, kila mwenye kuweza kutoa elimu ya uraia, atoe na kuisambaza kupitia mitandao ya kijamii, kufika 2025, elimu ya uraia iwe imeenea.
Japo ukuaji wa demokrasia ni mchakato hivyo, naendelea kusisitiza, CCM na serikali ya CCM, ina wajibu wa kulea vyama vya upinzani ili vikue na kujenga demokrasia ya kweli, Watanzania ni wamoja, na tunajenga nyumba moja, hakuna sababu ya kugombea fito, uchaguzi umekwisha, sasa kazi ni moja, kujenga nchi.
Mungu Ibariki Tanzania.
Paskali
- Mchungaji mwema huwaacha kondoo wake 99 na kwenda kumtafuta kondoo mmoja aliyepotea,akimpata ni furaha,akimkosa ni huzuni!
- Mtu mwenye viti 10, akiingia kushindana,akapoteza kiti kimoja,japo ameshinda vile 9 na kupoteza kimoja tuu,mshindi ni yule aliyekuwa hana,na sasa amempora huyo mwenye kumi na kubakiwa na 9。Aliyeshindwa ni aliyepoteza!na aliyeshinda ni aliyepata!。
- Yule mwana mpotevu aliporejea nyumbani alifanyiwa sherehe kubwa huku yule mwana mwema hakufanyiwa kitu。