Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,392
- 121,023
Wanabodi
Japo Sikukuu ya Christmas inasherekewa kwa shamra shamra sana, wengi wakidhani ndio sikukuu kubwa ya Wakristo, ukweli ni kuwa Pasaka ndio sikukuu kubwa ya Wakristo kutokana na fumbo la Paska, hakuna mtu yoyote aliyemshuhudia Yesu Kristo akifufuka, na baada ya kufufuka alikaa duniani kwa siku 40, kabla ya kupaa mbinguni, hakuna anayejua alikuwa anakaa wapi!. Fumbo hili la Paska ndio msingi mkuu Imani ya Ukristo.
Jumapili ya leo ni sikuu ya Pasaka, hivyo naomba nianze Makala yangu, kwa kuwatakia Wakristo na Watanzania wote, heri ya Pasaka.
Dini kuu mbili za Tanzania, Wakristo na Waislamu, zote zina sikukuu mbili mbili kubwa, kwa Waislamu ni sikukuu ya Iddi El Fitri na Sikukuu ya Iddi El Haj, shamrashamra za kusherehea Idi el Fitri na kubwa na inashereherekewa na watu wa dini zote mbili kwa shamrashamra na kuvaa nguo mpya kwa watoto.
Kwa Wakristo, sikukuu mbili ni Krisimasi na Pasaka, Krismasi ni kusherehekea kuzaliwa kwa Masiha, Yesu Kristo na Pasaka ni kusheherekea kufufufuka kwake. Krisimasi ndio yenye maandalizi ya muda mrefu na heshehekewa kwa shamra shamra sana, kuliko Pasaka, lakini ukweli Pasaka ndio sikukuu yenye maana kubwa kwa Wakristo kuliko Krismasi, kutokana na kitu kinachoitwa Fumbo la Paska ambalo ndio kiini cha Imani ya Ukristo
Fumbo la Imani ya Ukristo ni kuamini Kristo Alikufa, Kristo Alifufuka, Kristo Atakuja tena. Kristo kabla ya kufa, alisulubiwa kwa ajili ya Wakristo, akateswa kwa mamlaka ya Ponsyo Pilato, akafa, akazikwa. Akafufuka siku ya tatu ilivyoandikwa.
Fumbo la Pasaka ni kiini cha imani ya Kanisa inayopaswa kutangazwa na kushuhudiwa kwa watu wa Mataifa. Kwa njia ya mateso, kifo, ufufuko kutoka kwa wafu na kupaa mbinguni, mwanadamu amekombolewa kutoka katika dhambi na mauti!
Leo Jumapili ya Pasaka. Hii ndiyo siku aliyoifanya Bwana tuishangilie na tuifurahie. Ni siku ya ufufuko wa Bwana wetu Yesu Kristo. Ni siku ya tatu baada ya kifo chake. Kwa Wayahudi ni siku ya kwanza ya juma. Hii ni kwasababu siku za Kiyahudi zilianza jioni na kuisha jioni. Wayahudi hawakuhesabu siku kwa kuanzia saa sita ya usiku hadi saa sita ya usiku kama nyakati zetu. Ilipofika saa ya machweo yaani jua lilipoanza kuzama siku iliisha na mara siku mpya ilianza. Yesu alizikwa siku ya Ijumaa, akashinda siku nzima, siku ya Jumamosi hadi mapambazuko ya siku ya Jumapili. Hizo ni siku tatu. Tunazihesabu tatu, siyo kadiri ya masaa 24, bali kadiri ya majina ya siku jinsi walivyohesabu Wayahudi.
Kwanini tarehe ya kuadhimisha sherehe ya Pasaka hubadilika kila mwaka. Sikuu ya Pasaka ya Wayahudi iliitwa ‘Passover’, ili kuepuka Pasaka kuangukia siku za katikati ya Juma, ni lazima iadhimishwe siku ya Jumapili ambayo ni siku ya kwanza ya juma yaani jumapili
Hivyo Jumapili ni siku ya kwanza ya juma, siku ya ufufuko, ni siku ya uumbaji mpya tunaporudishiwa sura na mfano wa Mungu tulioupoteza kwa dhambi ya asili. Pasaka ni sikukuu Kuu. Pasaka ya sasa sio tena ile Pasaka, ya Wayahudi, waliyokumbuka kutolewa kwao utumwani Misri bali ni siku ya kukombolewa kutoka utumwa wa dhambi na nguvu za shetani.
Ufufuko wa Yesu
Kadiri ya desturi ya Wayahudi, mwili wa mtu aliyekufa akazikwa alipaswa kupakwa mafuta kwa siku tatu, baada ya kuzikwa, kwa sababu, waliamini kwamba roho ya mtu aliyekufa hubaki karibu na mwili kwa siku tatu na siku ya nne huenda kwa Mungu. Kwa sababu hiyo, walipaswa kuupaka mafuta mwili wa Yesu kwa siku tatu. Yesu alikufa siku ya Ijumaa na hivyo alipakwa mafuta mara ya kwanza kabla ya kuzikwa. Siku iliyofuata ilikuwa ni sabato, pia ilikuwa ni sikukuu kubwa ya Pasaka ya Wayahudi, hivyo hawakumpaka Yesu mafuta, kwa sababu, siku hiyo ya Sabato, hawakuruhusiwa kufanya kazi yeyote.
Baada ya kuzika, kwa vile tayari kulikuwa na fununu mitaani, za wafuasi wake kuuiba mwili wake kutoka kaburini, halafu wakauzike mahali pengine pa siri, na kujidai amefufuka na kupaa mbinguni, Pilato akaamuru kaburi lake lizibwe kwa jabali kubwa linalohitaji watu 12, kuliviringisha, kisha wakawekwa walinzi wanne kulinda 24/7 kwa kupokezana.
Kilichotokea hakuna ajuaye, hilo jabali lilibiringokaje, walinzi kushtuka, wanakutana na sanda tuu iliyofinywangwa finywangwa, mwili haupo!. Wakiripoti watauwawa, hivyo wakala kona kwa kutokomea kusikujulikana, hivyo ufufuko ni fumbo ambalo hakuna aliyeshuhudia!.
Baada ya sabato ilifuata Jumapili, siku ya kwanza ya juma ambayo ndiyo siku ya tatu baada ya Yesu kufa. Wanawake walienda kuupaka mwili wa Yesu mafuta mapema asubuhi. Walikuta kaburi liko wazi, na Yesu amekwishafufuka, sasa ni mzima. Hili ndio fumbo la Paska.
Ufufuko wa Yesu Kristo ndio msingi wa imani Ukristo. Kuteswa kwake kwa kupigwa mijeledi, kuvikwa taji la miiba, kutemewa mate, kutundikwa juu ya msalaba, kufa na kuzikwa kisha kufufuka ndio hasa kilele cha fumbo la ukombozi wa Ukristo, na ni kwa kupigwa kwake, sisi tumeponywa!
Wanawake Wake ni Watu Muhimu kwa Mungu
Kuna kasumba ya kuwadharau wanawake katika dini kuu zote mbili za kwa wanawake kuturuhusiwa kuwa Ma Imamu na Makasisi wa Katoliki, lakini kwa Mungu Wanawake ni watu muhimu, ni Wanawake ndio waliokwenda alfajiri kaburini kuupaka mwili wake mafuta nao wanashuhudia kuwa amefufuka na Yesu baada ya kukufuka aliwatokea kwanza wanawake, kuonyeshea umuhimu wa wanawake.
Ufufuko ni mabadiliko kutoka utu wa kale, kwenda utu upya, kutoka maisha ya dhambi kwenda maisha ya utakatifu.
Ufufuko wa Kristo ni wokovu wa Ukristo kwa kukombolewa kutoka mautini na kuwekwa huru kutoka utumwa wa shetani na upotevu wa milele. Mlango wa paradisi uliofungwa kutokana na dhambi ya asili ya Adamu na Eva, au Adamu na Hawa, umefunguliwa kwa kifo na ufufuko wa mwana wa Adamu, yaani Yesu Kristu.
Pasaka ni Habari Njema kwa Wakristo kwamba Kristo Mfufuka yuko kati yao, yupo pamoja nao na ndani ya kila mmoja wao. Kristo ameshinda dhambi na kifo,
Nawatakieni Heri ya Pasaka
Pasakali