Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,106
- 10,173
Novemba 5, 2016, Suleiman Hiyari Mtarisi akiwa mteja wa Airtel(T) Limited alikosea kutuma fedha na aliwaomba mtandao wake warudishe fedha aliyotuma kimakosa ambayo ilikuwa ni Tsh 18,000. Mtu wa huduma kwa wateja alimuhakikishia kurejesha muamala ndani ya saa 24. Fedha hizo zilishindwa kurejeshwa ambapo alipiga simu mara kadhaa hadi Novemba 8 ambapo muamala wake ulirejeshwa.
Novemba 9, Suleimani aliokea simu kutoka kwa mtu aliyejitambulisha kuwa mfanyakazi wa Airtel na alikuwa na maelekezo ya kuingua akaunti yake. Kwa kuwa alikuwa amewasiliana na Airtel siku moja nyuma hakumtilia shaka hivyo. Baadae alibaini ameibiwa Tsh 1,200,000 kutoka kwenye akaunti yake kutoka kwenye akaunti ya Airtel.
Suleimani aliripoti polisi na Airtel kuhusu wizi huo lakini kutokana na sintofahamu akaenda Kamati ya Malalamiko ya TCRA ambapo wote walisikiliza malalamiko yake na kuiamuru Airtel irejeshe fedha hizo kwa mteja wao kwa kuwa ilionekana kama ni mtu wa ndani aliyekuwa anafahamu kuhusu Suleiman hadi kufanikisha wizi huo.
Uamuzi wa kamati umerekodiwa katika malalamiko Namba TCRA/02/11/Oktoba/2018.