Je, unakumbuka nini kuhusu migomo shule za sekondari?

HansMaja

Senior Member
Nov 9, 2010
103
116
Hivi huduma shule za sekondari Tanzania zimeboreshwa? Nakumbuka miaka ya 90's tulikua tukisikia migomo ya wanafunzi kila kukicha.

Miaka ile ndio palitokea mgomo Sekondari ya Tambaza na wanafunzi wote tulisambaratishwa kwa kuhamishwa na shule kubadilishwa kua High School. Je, unakumbuka nini kuhusu Migomo shule za Sekondari?
 
Waliokuwa wanagoma 90s ndiyo wazazi wa leo, hao hao ndo walimu wa leo. Wanajua mbinu zote na wanadhibiti. Pia wanaosoma siku hizi ni wadogo kwa umri, wanashindwa kuwazidi uwezo hawa wagomi wa 90s.
 
Hivi huduma shule za sekondari Tanzania zimeboreshwa? Nakumbuka miaka ya 90's tulikua tukisikia migomo ya wanafunzi kila kukicha. Miaka ile ndio palitokea mgomo Sekondari ya Tambaza na wanafunzi wote tulisambaratishwa kwa kuhamishwa na shule kubadilishwa kua High School. Je, unakumbuka nini kuhusu Migomo shule za Sekondari?
Kipindi hicho nchi ilikuwa inapitia kwenye kipindi cha mabadiliko ya kiuchumi kwa Serikali kujiondoa kwenye kuendesha baadhi ya huduma za jamii ikiwemo elimu.(Masharti ya wafadhili)
Hivyo kuathiri huduma nyingi zilizokuwa zinatolewa shuleni kama chakula kizuri, kuondolewa kwa usafiri wa kwenda na kurudi shuleni kwa wanafunzi kwa gharama za serikali.nk
Hivyo,mabadiliko haya yaliambatana na migomo ya wanafunzi kwa shule zile kubwa kama Tambaza, Tosamaganga,Songea Boys na nyinginezo.
 
Nami nilisoma Tambaza,kwenye kuhamishwa nikapelekwa Songea Boys,siku nimeripoti Songea Boys nilishangaa maisha ya kula mihogo,viazi na Ugali maharage😭,lakini baada ya muda nilizoea na kumaliza salama Kidato cha Nne 1997
Nimesikitika mmoja ya washkaji zangu wa karibu tangu Tambaza mpaka Songea Boys amehukumiwa kifungo cha maisha jela wiki mbili zilizopita kwa kosa la Madawa ya Kulevya akiwa na Boss wake Chonji
 
Nami nilisoma Tambaza,kwenye kuhamishwa nikapelekwa Songea Boys,siku nimeripoti Songea Boys nilishangaa maisha ya kula mihogo,viazi na Ugali maharage,lakini baada ya muda nilizoea na kumaliza salama Kidato cha Nne 1997
Nimesikitika mmoja ya washkaji zangu wa karibu tangu Tambaza mpaka Songea Boys amehukumiwa kifungo cha maisha jela wiki mbili zilizopita kwa kosa la Madawa ya Kulevya akiwa na Boss wake Chonji
Mwana kumbe wwe ni Sambukile! ?
 
Hivi huduma shule za sekondari Tanzania zimeboreshwa? Nakumbuka miaka ya 90's tulikua tukisikia migomo ya wanafunzi kila kukicha.

Miaka ile ndio palitokea mgomo Sekondari ya Tambaza na wanafunzi wote tulisambaratishwa kwa kuhamishwa na shule kubadilishwa kua High School. Je, unakumbuka nini kuhusu Migomo shule za Sekondari?
Ninakumbuka tuligoma kula wali na viazi mviringo eti tuwe tunakula ugali, tulipikiwa siku moja tu na hatukupikiwa tena. Mgomo ulianzishwa na mwanafunzi wa kisukuma.
 
Hakuna kilichoboreshwa bali wanafunzi ndio wamebaki wadogo mashuleni kiasi cha kukosa uwezo wa kufanya resistance, Mashuleni huko maozo yapo kibao tatzo wanaosoma kwa sasa ni watoto wadogo ambao hawana uwezo wa Ku organise migomo
 
Hivi huduma shule za sekondari Tanzania zimeboreshwa? Nakumbuka miaka ya 90's tulikua tukisikia migomo ya wanafunzi kila kukicha.

Miaka ile ndio palitokea mgomo Sekondari ya Tambaza na wanafunzi wote tulisambaratishwa kwa kuhamishwa na shule kubadilishwa kua High School. Je, unakumbuka nini kuhusu Migomo shule za Sekondari?
Hivi tulikua watu wazima sana kipindi hiko mpaka kujielewa au ndio bas ilikua inatokea tu
 
Ni takriban miaka 30 imepita siwezi kuusahau yale matukio ya kutisha.
Baada ya majadiliano ya kutaka wanafunzi wasitishe mgomo kushindikana usiku saa mbili kengele ikapigwa, maelekezo yalikuwa mafupi tu form 1 na 2 kaleteni mawe tunaanzia nyumban kwa headmaster. Uharibifu mkubwa ulifanyika na watu waliumia wakiwemo wanakijiji, askari na wanafunzi
 
Sasahivi wanasoma vitoto nakumbuka sisi tulikinukisha police walikuja kutuliza mmoja wapo tulimkung'uta Hadi walipokuja wazee wenyewe sasa ffu ndo tukatulizwa.

Matukio tuliyofanya

Kuchinja kuku na mbuzi za headmaster wetu

Kujihudumia duka la shule Hadi tukamalizia Kila kitu na kuvunja vunja Kila kitu.

Mlinzi alipigwa kama Ngoma ama dufu.

Mpishi alipigwa vilevile alikuwa anaweka mafuta ya taa tukimwambia anasema kesho anaongeza zaidi nk
 
Ni takriban miaka 30 imepita siwezi kuusahau yale matukio ya kutisha.
Baada ya majadiliano ya kutaka wanafunzi wasitishe mgomo kushindikana usiku saa mbili kengele ikapigwa, maelekezo yalikuwa mafupi tu form 1 na 2 kaleteni mawe tunaanzia nyumban kwa headmaster. Uharibifu mkubwa ulifanyika na watu waliumia wakiwemo wanakijiji, askari na wanafunzi
Ilikuwa kawaida sana kukinukisha saivi Nina miaka hata 13 sijawahi sikia hata mgomo kidogo tu. Daaah😂😂😂
 
Back
Top Bottom