Je, unajua kwanini hufanikiwi?

Mr-Njombe

Member
Aug 29, 2022
58
106
Mu hali gani!

Kunamitazamo mingi kuhusu suala la mafanikio ya mtu, lakini kwaujumla kufanikiwa nikufanikisha kutekeleza mipango na malengo tunayojiwekea katika maisha.

Lakini asilimiakubwa ya watu hushindwa kufanikiwa kwasababu zifuatazo;-

Kwanza
Kutojiwekea malengo au kupoteza focus ya kutekeleza mipango na malengo yake. kutokana na mambo mbali mbali yanayoibuka katika maisha. ("If you fail to plan you plan to fail")

Pili
Kukosa uthubutu (inferiority), Mtu kuhisi kwamba hawezi kufanya jambo,ama hastahili kua katika nafasi fulani.

Tatu
Kuogopa kufeli ama kupata hasara. Mafanikio hayaji kama mvua bali kwa kujituma na wakati mwingine kujitoa kwa hali na mali.

Nne
Kukatishwa tamaa, kwenye maisha na katika kila Jambo unalolifanya lazima kunawatakao kupa moyo na watakao kukatisha tamaa hivyo ni vema kuchukua mawazo chanya .

Japo zipo sababu nyingi lakini kwa leo wana JF napenda kuainisha hizi asanteni

Karibu Muungwana unaweza ongezea nyingine zitusaidie kifikra.

Naomba kuwasilisha.
 
Elimu za mafanikio mzitoe huko mtaani zaidi ndani ya jamii zenu Kwa vitendo zaidi ili ziweze fanikiwa Kwa kuwa ni asilimia kubwa mnoo kuliko wa humu mitandao ya kijamii
 
Back
Top Bottom