Je, unafahamu maana ya Hisa na Authorised Share Capital?

Masokotz

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
3,691
6,073
Kama umewahi au unamiliki kampuni basi maneno yafuatayo yatakuwepo katika msamiati wa maneno yako Share Capital, Authorized Share Capital, Paid up and issued shares. Maneno mengine ambayo utakuwa unayafahamu ni pamoja na maneno kama Limited Liability, n.k.

Kupata maana ya maneno haya ni rahisi sana ili kuelewa umuhimu na nguvu yake ni jambo lingine.

Unapoenda kusajili kampuni BRELA utakuta kila kiwango cha mtaji hisa (Share Capital) kina viwango/gharama tofauti za usajili.Moja kati ya maswali ambayo huwa nakutana nayo mara kwa mara ni pamoja na tofauti kati/na umuhimu wa share capital. Wengi huuliza iwapo kampuni yenye share capital ndogo/kubwa ina tofauti yoyote ile. Wengine pia huuliza kuhusu idadi ya hisa na gharama ya hisa moja. Wengine huuliza iwapo ni lazima hisa zote ziwe zimeshatolewa issued and paid up au sio lazima.

Kwa kawaida maswali kama haya yanahitaji elimu ya sheria na elimu ya Biashara kwani katika eneo hili utaalamu wa sheria za biashara na uendeshaji wa biashara huwa unahitajika. Eneo lingine ambalo huwa na utata huwa linahusu dhana ya limited liability na umuhimu wake kwa wamiliki. Maswali mengine ni pamoja na masuala ya kisheria na kibiashara na kikodi ynayohusu Limited Company kwa mfumo wa sheria za Makampuni na sheria za kodi za Tanzania.

Kwanza nikiri kwamba mimi ni mfanya biashara ila sio mwanasheria wala mtaaluma wa masuala ya kodi kwa hivyo basi yote ninayoandika hapa ni katika mtazamo wa kawaida na general knowledge na iwapo mtu anahitaji ushauri wa kitaalamu basi ni muhimu aonane na wanasheria, washauri wa kodi au wahasibu. Hata hivyo naweza pia kusaidia kupata wataalamu wanaoweza kukusaidia katika baadhi ya maeneo kwa kuzingatia mahitaji yako. Ujuzi na uelewa wangu utakusaidia kuweza kutumia huduma hizi za wataalamu kikamilifu na kwa mafanikio.

Turudi kwenye Mada.

Katika mada hii nitaanza kwa kuzungumzia dhana ya Limited Company,faida na umuhimu wake.Kwa kawaida Limited Company imezaliwa kutokana uhitaji wa kudhibiti kiwango cha Risk ambacho mtu anapata/kuchukua pale anapoamua kufungua biashara.Kwa mfano unataka kufungua duka ufanye biashara.Unapofanya biashara unaweza pata hasara au faida.Lakini pia unapofanya biashara kunaweza kutoka ukawa na madeni/mikopo na wakati mwingine unaweza pia ukaingia katika majanga au athari ambazo zitaweza kukuingiza katika hasara.Lengo la Limited Company ni kukulinda wewe binafsi dhidi ya athari hizo.

Unapokuwa na Limited Company huwezi poteza,nyumba au gari au mali yako nyingine kwa sababu tu ya matatizo ya kibiashara. Biashara yako inakuwa inajitegemea na inakuwa na uwezo wa kushtaki na kushatkiwa na inakuwa na independent legal existence yaani ni independent legal entity. Ikivunja sheria inashitakiwa kama ambavyo ungeshitakiwa wewe lakini wewe hautashitakiwa kwa sababu yake. Kuna mambo mengi sana yanayohusu Limited Company lakini kubwa kuliko LOTE ni kujilinda na kuwalinda uwapendao na mali zako. Unaposajili kampuni kama LIMITES maana yake unakuwa na haki ya kutumia neno LIMITED mbele ya Jina la Kampuni yako. BIASHARA yako inakuwa inajitegemea.

Mmiliki atawajikibika kwa kutegemea uhusika wako katika uendeshaji wa kampuni.Kwa mfano kama wewe ni mkurugenzi basi utawajibika kwa akdiri ya uwajibikaji wa wakurugenzi, kama ni muajiriwa utawajibika kwa kadiri ya muajiriwa.

Katika Kusajili kampuni pembeni ya kuwa na jina ni lazima uwe na katika ya kampuni/Company By Laws/Memorandum and Articles of Association. Hizi ni nyaraka mbili.Moja inaelezea malengo ya kuundwa kwa kampuni na ya pili inaendelea kueleza uendeshaji na usimamizi wa kampuni husika. Nyaraka hizi mbili ni makubaliano ya wale wamiliki (Shareholders) ambao wameamua kuunganika kuunda kampuni.

Kumekuwa na katabia ka watu kuwaingiza watu kwenye hizi nyaraka kisela bila kufikiri umuhimu na nafasi yao katika biashara husika. Hii ni hatari kwani itakapotokea kampuni imeingia katika mgogoro na kama watu uliowaweka sio wema wanaweza kukutoa kwenye kampuni yako na kujikuta huna haki. Ndio maana huwa nawashauri watu waingie makubaliano yanayohusu uanzishaji wa kampuni(Pre incorporation agreement) ili kila mmoja ajue haki na wajibu wake katika uundaji wa kampuni.

Hizi nyaraka(Memorandum and Articles of Association ni standard na unaweza kuandaa mwenyewe au kuandaliwa na mwanasheria ila ni lazima zizingatie mfumo uliopendekezwa na Serikali katika sheria ya makampuni na kanuni zake. Katika nyaraka hii pia honesha kiwango cha mtaji na idadi ya hisa na bei ya kila hisa na idadi ya hisa ambazo kila mtu amechukua(Subscribe).

Hisa ni nini? Hisa ni kipande cha umiliki ni uthibitisho wa kiwango cha umiliki wa hisa katika kampuni husika. Kwa mfano kama kampuni imeundwa kwa mtaji HISA wa kiasi cha shilingi Milioni moja basi unaweza kuamua kuzigawa hisa zako katika vipande hisa 100 vyenye thamni ya shilingi 10,000 kila moja. Kwa lugha nyingine kila mwanahisa atapaswa kulipia shilingi 10,000 kuchangia katika mtaji hisa. Kama mtua akilipa shilingi 50,000 basi atakuwa na HISA 5 ambazo unaweza kusema ni 5% ya kampuni. Sasa kulingana na utendaji wa kampuni kibishara bei ya hisa inaweza kupanda au kushuka kwa kutegemea na ukwasi wa kampuni. Kwa mfano kama mmeanzisha kampuni kwa gharama ya milioni 1 (share capital) na kisha baada ya mwaka mkafanya biashara na kuingiza faida ya milioni 100 basi thamani ya hisa yako 1 itakuwa imekuwa 1,000,000. Ukiwa na hisa tano milioni 5. Kama mtagawiwa faida basi utapewa milioni tano ambayo itakatwa vikodi fulani na maisha yataendelea. Iwapo mtaamua kununua shamba kwa milioni 100 zenu basi umiliki wenu katika hili shamba utakuwa na uwiano sawa na hizo hisa zenu.Kama mkiamua kuchukua mkopo basi uwiano wa deni lenu kwa kila hisa utakuwa ni sawa na uwiano wenu katika hisa.

Hata hivyo kwenye upande wa deni wewe hutakamatwa kama kampuni itshindwa kulipa deni bali utapaswa kuiweka kampuni yako chini ya muflisi (Mfilisi-Hapa unahitaji kuelewa sheria ya ufilisi/bankruptcy na maamuzi ya mahakama) Rejea kufilisika kwa benki.Katika hali kama hii kuna mengi ambayo wewe kama mmiliki huwa umelindwa. Ndio maana watu wengine kwa kutambua hilo huwa wanawake mali zao katika TRUST na biashara zao katika limited Company na kisha wao wenyewe wanajikatia bima za maisha. Hili huhakikisha kwamba wakiyumba huku wanashika huku na wasipokuwepo familia zao zinaendelea kuwepo na hata kampuni ikifilisika wanakuwa salama ingawa kama ulikuwa mkurugenzi wa kampuni iliyofilisika na ikaonekana kulikuwa na ukiukwaji wa sheria unaweza kuwajibishwa na hata kupigwa marufukuwa kuwa mkurugenzi katika kampuni.

Ninachotaka ufahamu ni kwamba Mkurugenzi wa kampuni anawajibika kuhakikisha kwamba kampuni inawajibika kwa wateja, wamiliki na kwa serikali na kukiwa na ukiukwaji basi atawajibika kwa kadiri ya nafasi yake. Mmiliki yeye wajibu wake ni kuchangia mtaji na kusbiri faida. Kuna watu ambao huamua kuwa wakurugenzi na wamiliki kwa 100% hawa huwajibika katika maswala ya uendeshaji kama wakurugenzi na sio kama wamiliki.

Hili ni somo refu na ninaamini kuna maeneo ambayo sijayaweka sawa kwani maelezo yangu ni kwa kadiri ya uzoefu wangu katika uendeshaji na usimamizi wa kampuni.Hata hivyo ni muhimu ukatafuta maarifa zaidi iwapo unataka kuanzisha kampuni binafsi ili ufahamu kwa kina kile ambacho unaweza kufaidika kwa kuwa na LIMITED COMPANY.

Iwapo unahitaji kupata maelezo zaidi au kusajili kampuni yako wasiliana nasi ili tuangalie namna ambavyo tunaweza kukusaidia kufikia lengo.

Kuhusu SISI

Masoko Consulting ni Strategic Consulting Firm (Washauri waelekezi wa Kimkakati) ambao tunatumia mbinu za kisasa na utaalam wa kisasa katika kuwasaidia wateja wetu kutambua fursa na kuzitumia kwa ajili ya kukuza biashara zao na kukuza faida.Lengo letu ni kuwasaidi wafanyabiasha wadogo na wakati kubadilisha na kuboresha mfumo wa uendeshaji na usimamizi wa biashara zao ili ziendane na dunia ya kisasa kwa kuwawezesha kufikia zana za kisasa,utaalamu wa kisasa na teknolojia katika kuendesha biashara zao.

Sisi tunatoa huduma ya usajili wa Majina ya biashara,kampuni,leseni,TIN number NGOs,Taasisi za Kijamii,SACCOS,Taasisi za KIDINI,Taasisi za ELIMU,Viwanda,UWEKEZAJI na pia tunatoa ushauri juu ya namna bora ya kuendesha biashara yako.Unaweza kupata huduma hizo kwa gharama nafuu.Baadhi ya huduma hizo ni pamoja na:
  1. Kwanza tutakushauri kuhusu muundo wa biashara yako faida na hasara pamoja fursa mbalimbali
  2. Pili tutakufanyia utafiti na ushauri wa Jina la Biashara yako kwa kuzingatia vigezo vya SOKO
  3. Tutakufanyia Taratibu zote za usajili kuanzia Uandaaji wa Nyaraka Mpaka Kukamilika kwa Usajili Kampuni,TRA,Mashine za EFD na VFD,Vibali vya TBS pamoja na leseni
  4. Tutakuandikia Company Profile ya Kisasa kwa Lugha ya Kiingereza na Kiswahili
  5. Kama unahitaji mkopo kutoka katika taasisi za fedha tutakusaidia kufanya mchakato kwa kuzingatia mahitaji yako na vigezo vya taasisi husika.
  6. Tutakutengenezea Website ya kisasa kwa ajili ya Biashara na huduma zako.
  7. Tutakutengenezea, Logo, Business Card,Letter Head pamoja na Nyaraka nyingine za Kibiashara
  8. Tutakupatia Mfumo wa Kutunza kumbukumbu kwa njia ya Mtandao au kwenye Computer yako kwa ajili ya kusimamia Biashara yako
  9. Tutakufanyia Initial Marketing kwa Wateja wako (Inategemea aina ya biashara )wa Mwanzo ili kuwa na customer base ya kuanzia
  10. Pia tutakusaidia Mchakato wa Kufungua Bank Account kwa kutumia jina la Biashara yako (Deposit Ya Kwako)
  11. Tutakuwa nawe katika mchakato mzima wa kuendesha biashara yako mpaka itakapokuwa stable na wewe kupata uzoefu wa kutosha katika biashara yako.

Huduma hizi zinapatikana kwa pamoja au kwa moja moja na mfumo wetu wa malipo ni nafuu na unazingatia matokea katika kila hatua.Kama unahitaji huduma zetu wasiliana nasi kwa email:masokotz@yahoo.com au kwa simu +255710323060.

Karibu sana
 
Kwanini threads nzuri za kujenga kama hizi hazisomwi sana, na reply zake huwa chache sana, shukrani sana kwa elimu hii kuna kitu nimepata
 
Na haya masoko ya hisa ni nini na yana maana gani au kazi gani e.g(Dar es salaam stock exchange, New York stock exchange, London stock exchange, Tokyo stock exchange)
 
Lakini nilikuwa napenda kujua nini maana ya hati fungani?
Na haya masoko ya hisa ni nini na yana maana gani au kazi gani e.g(Dar es salaam stock exchange, New York stock exchange, London stock exchange, Tokyo stock exchange)
Umeuliza Maswali matano katika swali moja.

Hati Fungani nini?

Hati fungani ni aina ya hati anayopatiwa mtu kama uthibitisho wa mkopo.Hati hizo mara nyingi zinaandamana na dhamana fulani ambayo inamuhakikishia mnunuaji wa hati hizo kwamba atalipwa kiasi fulani cha pesa katika kila kipindi fulani na baada ya muda wa mkataba atarudishiwa Pesa yake aliyowekeze.So hati fungani Mkopo kutoka kwa muwekezaji kwenda kwa kampuni.Kwako wewe huo ni uwekezaji na kwa yule unayempatia ni mkopo.Tofauti na mikopo ya kawaida ambayo inakuwa na masharti hati fungani huwa hazina masharti sawa na mikopo na riba yake mara nyingi huwa ni kubwa zaidi kuliko ya akaunti za akiba.hati fungani maarufi ni zile zinazotolewa na serikali(Treasury Bonds) ingawa pia kuna makampuni makubwa nayo hutoa hizo Bonds.

SOKO la hisa ni kama masoko mengine(Sehemu ya kuadlishana bidhaa/huduma) ila soko jhili bidha inayouzwa na kunuliwa ni PESA kwa kutumia PESA.Yaani unatoa PESA kununua PESA.Katika eneo hili wahusika wakubwa ni wanahisa ingawa pia wakati mwingine makampuni na serikali huenda kule kwa ajili ya kununua na kuuza hisa mpya zikiwemo hati fungani.

Hati fungani pamoja na hisa zinauzwa na kununuliwa katika Masoko ya HISA kwa kusingatia vigezo na masharti ya Soko husika la hisa.

Kwa kawaida mwanahisa wa kampuni fulani anapotaka kuuza HISA zake anazipeleka katika soko la hisa kupitia kwa BROKER ambaye ataziweka sokoni kwa niaba yake na kumuuzi mtu mwingine ambaye anatka kununua hisa katika soko hilo.

Ili hisa za kampuni ziweze kuuzwa katika soko la hisa ni lazima kampuni iwe LISTED(Kuorodheshwa katika soko) mchakato wa kuorodhesha huanza kwa kitu kinaitwa IPO ambapo kampuni ya UMMA hupeleka Hisa zake kuuzwa kwa mara ya kwanza.Baada ya hapo hisa zinakuwa FREELY floated kwenye soko la hisa na BEI yake hupanda na kushuka kwa kutegemea mahitaji ya soko na utendaji wa kampuni.

Ni somo refu lakini kwa ufupi SOKO la HISA ni SOKO ma MITAJI ambapo wenye mitaji na wanaohitaji mitaja wanakutana ili wajenge uchumi
 
Kwanini threads nzuri za kujenga kama hizi hazisomwi sana, na reply zake huwa chache sana, shukrani sana kwa elimu hii kuna kitu nimepata
Ni kwa sababu haziandikwi kwa ajili ya watu wote.Zinaandikwa kwa ajili ya wachache ambao zinawafaa ila kwa sababu ni ngumu kuwapata wachache hawa ambao ni wateule basi huwa tunaziweka kwenye majukwaa ya wazi huku tukijua kwamba wanaohusika watapa kitu.
 
Kwenye Uzi kama huuu, wachangiaji wapo wachache sana, nchi inahitaji watu wasome kweli maesabu na uwekezaji ndio tuweze kutoka sehemu Moja kwenda nyingine

Sent from my Nokia 1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Umeuliza Maswali matano katika swali moja.

Hati Fungani nini?

Hati fungani ni aina ya hati anayopatiwa mtu kama uthibitisho wa mkopo.Hati hizo mara nyingi zinaandamana na dhamana fulani ambayo inamuhakikishia mnunuaji wa hati hizo kwamba atalipwa kiasi fulani cha pesa katika kila kipindi fulani na baada ya muda wa mkataba atarudishiwa Pesa yake aliyowekeze.So hati fungani Mkopo kutoka kwa muwekezaji kwenda kwa kampuni.Kwako wewe huo ni uwekezaji na kwa yule unayempatia ni mkopo.Tofauti na mikopo ya kawaida ambayo inakuwa na masharti hati fungani huwa hazina masharti sawa na mikopo na riba yake mara nyingi huwa ni kubwa zaidi kuliko ya akaunti za akiba.hati fungani maarufi ni zile zinazotolewa na serikali(Treasury Bonds) ingawa pia kuna makampuni makubwa nayo hutoa hizo Bonds.

SOKO la hisa ni kama masoko mengine(Sehemu ya kuadlishana bidhaa/huduma) ila soko jhili bidha inayouzwa na kunuliwa ni PESA kwa kutumia PESA.Yaani unatoa PESA kununua PESA.Katika eneo hili wahusika wakubwa ni wanahisa ingawa pia wakati mwingine makampuni na serikali huenda kule kwa ajili ya kununua na kuuza hisa mpya zikiwemo hati fungani.

Hati fungani pamoja na hisa zinauzwa na kununuliwa katika Masoko ya HISA kwa kusingatia vigezo na masharti ya Soko husika la hisa.

Kwa kawaida mwanahisa wa kampuni fulani anapotaka kuuza HISA zake anazipeleka katika soko la hisa kupitia kwa BROKER ambaye ataziweka sokoni kwa niaba yake na kumuuzi mtu mwingine ambaye anatka kununua hisa katika soko hilo.

Ili hisa za kampuni ziweze kuuzwa katika soko la hisa ni lazima kampuni iwe LISTED(Kuorodheshwa katika soko) mchakato wa kuorodhesha huanza kwa kitu kinaitwa IPO ambapo kampuni ya UMMA hupeleka Hisa zake kuuzwa kwa mara ya kwanza.Baada ya hapo hisa zinakuwa FREELY floated kwenye soko la hisa na BEI yake hupanda na kushuka kwa kutegemea mahitaji ya soko na utendaji wa kampuni.

Ni somo refu lakini kwa ufupi SOKO la HISA ni SOKO ma MITAJI ambapo wenye mitaji na wanaohitaji mitaja wanakutana ili wajenge uchumi
Vipi treasury bond na treasury bills zote zinaitwa hati fungani kwa Kiswahili?
 
Nauliza kwa Kiswahili mkuu. Hati fungani ni zote t-bills na t-bonds au linatumika kwa moja tu
Well kwa kiswahili zinamaana moja,Dhamana za serikali au hati fungani na zipo katika makundi mawili yaani muda mrefu au muda mfupi
 
Nimependa, kwanza umeonesha competence kubwa alafu ukatukaribisha hii ni nzuri sana. Maswala ya kampuni yana mambo mengi sana ila na leo nimeongeza kitu kidogo.
 
Nakutafuta soon boss hongera sana upo vizuri na umegusa sehemu zangu husika
 
Habari, Nauliza kuhusu hisa na Faida zake unazoweza kupata nahitaji ufafanuzi. Na yapi masoko mazuri ya Kununua Hisa na ni muda Gani unafanya uwekezaji na Faida zake.
 
Habari, Nauliza kuhusu hisa na Faida zake unazoweza kupata nahitaji ufafanuzi. Na yapi masoko mazuri ya Kununua Hisa na ni muda Gani unafanya uwekezaji na Faida zake.
Mkuu,hisa ni kipande cha umiliki.Kampuni zinazouza hisa zake kwa umma zinaitwa Public Company.Private Company haziuzi hisa kwa umma.Kwa Tanzania kuna soko la hisa la DSE ambamo ndio watu wanapofanya mauzo na manunuzi ya Hisa.
 
Back
Top Bottom