Je unaenda kuwa mzigo au?

Joseverest

JF-Expert Member
Sep 25, 2013
52,598
70,876
Wakati mwingine mzazi anapokuambia uvumilie ndoa ndiyo ilivyo anamaanisha kua hembu kaa huko kwa mume wako unataka uondoke ili uraudi kwangu unitie matatizo, nimeshamaliza kulea halafu unataka uje na watoto wako unitupie hapa hapana!

Ndiyo najua hawezi kukuambia hivyo kwakua ni mzazi wako, ila wakati mwingi wazazi wanachoka, wakiona huwezi kujitegemea ni ngumu sana kukuambia kua rudi mwanangu, watatafuta namna ya wewe kubaki kwa mumeo ili uendeleee kuwa mzigo kwake.

Lakini hata wale marafiki zako wanaokuambia kua vumilia ndoa ndiyo zilivyo, mara nyingi nao wanajua ukiondoka huna kazi basi watasumbuka kukukopesha na kukusaidia saidia, hivyo wanaona bora ubaki tu huko uvumilie mateso kama wanawake wengine.

Lakini mumeo anapokuambia ondoka kama untaka wakati mwingine si kama hakupendi au anataka uondoke hapana, anajua unamtegemea kwa kila kitu kuanzia Pedi mpaka chakula hivyo anajua kua huwezi kuondoka, huendi popote na atakunyanyasa na kukupiga atakavyo.

Kwa maana hiyo basi dada yangu, hembu jaribu kujitegemea kikipato. Acha kulialia kuwa mume hakupi mtaji, kwani huyo mumeo yeye alipewa mtaji na nani, nani alimtafutia kazi, kwanini wewe usijilegeze ukakusnaya kamtaji kako ukaanza biashara hata kama ni ya maandazi.

Kwamba ajue tu kuwa na wewe unaweza kuishi mwenyewe na si kumtegemea yeye tu. Lakini wakati mwingine hata wewe unatishia tu kuondoka lakini unajua huondoki kwani huwezi kujitegemea na nyumbani washakuambia hapa hurudi wakaijifanya wanapenda ndoa yako kumbe washakuchoka.

Sasa naomba ujiangalie, wewe binti ambaye hujaolewa je ukiolewa sasa unaweza kutoka kwenye ndoa na kujitegemea, vipi wewe ambaye uko kwenye ndoa, akisema ondoka leo, je unaweza kujitegemea au unaenda kuwa mzigo kwa Baba yako na ndugu zako wengine?

Najua unajibu, ushajijua kama wewe ni mzigo au la? Badilika, maisha yamebadilika, acha kuwa mzigo acha kulialia.
 
On point Jose..
Lakini mbona umesema sisi tu, kwani nyie hamuwezi kuja kuwa mizigo?
Tena nyie ndo mbaya zaidi cos mwanaume akiishiwa, halafu na hizo ego zenu si rahisi kurudi kwa wazazi ni heri afe kisabuni kwa mwanamke wake.
 
On point Jose..
Lakini mbona umesema sisi tu, kwani nyie hamuwezi kuja kuwa mizigo?
Tena nyie ndo mbaya zaidi cos mwanaume akiishiwa, halafu na hizo ego zenu si rahisi kurudi kwa wazazi ni heri afe kisabuni kwa mwanamke wake.
Mara chache sana huwa inatokea
 
1. Andrew Chenge
2. Daniel Yona
3. Nazir Karamagi
4. Lazaro Nyalandu
5. Basil Mramba

Ebu ngoja leo nilale mapema aiseeeeee....... Maana hizi
zimetosha
 
Mh!, labda kama nyie wa sayari nyingine.
Ndoa zinapo vunjika au wanandoa kutengana, mara nyingi wanawake ndio wanaorudi makwao na kua tegemezi. Hii ni kutokana na wengi wao kuwa wamama wa nyumbani bila kujishughulisha.

Wengi huwategemea waume zao kuwahudumia kila kitu, sasa wanapotengana ndo inabidi warudishe mpira kwa kipa!

I think joseverest has a point!
 


He has a point yes but, hizi zama wanawake wanajitahidi pia kujikwamua kimaisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…