Strong ladg
Senior Member
- Jul 15, 2021
- 155
- 435
Niende kwenye mada . Swali ambalo nimeanza kujiuliza hivi karibuni, ni nini faida ya kuwa na AU kwa sasa hapa Afrika. Kwanza fedha tu za kujiendesha AU zinatolewa kwa asilimia kubwa na Umoja wa Ulaya. Hizo fedha haziji bure zinakuja na masharti kibao, maana yake ni kwamba Umoja wa Afrika unaendeshwa na Umoja wa Ulaya,nini maana ya kuwa na AU kama bajeti yake tu inatushinda?
Pili AU imeshindwa kuleta suluhisho la kudumu kuhusu vita na ukosefu wa usalama kwenye nchi za Afrika. Mfano sasahivi Sudan kuna vita ambayo hatuoni ikiisha karibuni lakini AU wako kimya kama hakuna kinachoendelea hapo Sudan.
AU imeshindwa kuweka utaratibu wa kurahisisha usafirishaji rahisi wa bidhaa na usafiri rahisi wa watu kati ya nchi za Afrika.
Kama hiyo haitoshi viongozi wa Afrika ambao ndio wanakutana Addis Ababa Ethiopia asilimia kubwa ni wala Rushwa, vibaraka, n.k n.k . Yaani umoja unaundwa na Ruto, Tinubu, Ouattara aisée what do you expect.
Hitimisho langu ni kwamba Umoja wa Afrika umeshindwa kufikia ndoto za waanzilishi wake kina Kwame Nkrumah na badala yake umekuwa ukitumiwa na maadui wa Afrika kutekeleza ajenda zao.
Naomba kuwasilisha na nakubali kukosolewa.