Je, ulishawahi kushuka na begi/mzigo wa abiria mwenzio kwa bahati mbaya? Mtu aliyeshuka na box langu la samaki mwaka 2012 sasa ni family friend

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,892
16,406
Habari za wakati huu kaka na dada zangu wote wa hapa JamiiForums.

Ndugu zangu watanzania;

Je, ulishawahi kushuka na begi/mzigo wa abiria mwenzio kwa bahati mbaya? Mtu aliyeshuka na box langu la samaki mwaka 2012 sasa ni family friend.

Kuna kamsemo kamoja huwa kanatamba sana huku mitaani uswahilini kwetu kwamba kuibiwa mume inauma sana kuzidi maumivu ya jino.

Kwa mfano labda ningekuwa nimemuoa Bushmamy alafu aje kugundua mimi mumewe Soldier ninaibwa na jimama kama witnessj vile eti maumivu yatakuwa makali kuzidi jino linavyouma nyakati za usiku.

Wooote wanaosema na kuushadadia msemo huu mimi ninawaona kama hawajui nini maana ya maumivu. Hivi unayajua maumivu ya mtu kushuka na mzigo wako wa thamani katika safari?

Yaaani umechaguliwa kujiunga na chuo cha SAUT huko Mwanza alafu unapokuwa safarini kwenda ku-report abiria mwenzio anashuka na begi lako uliloweka vyeti vyako vya form four na form six.

Hivi unayajua maumivu ya mtu kushuka na mtoto wako wa miaka 2 njiani baada ya kumuomba akubebee ndani ya daladala ya Mbagala - Kariakoo?

Mimi yalinikuta mwaka 2012. Baada ya kupata taarifa za kifo cha baba yangu mdogo nikiwa Dodoma ikanibidi kufunga safari mpaka Wilaya ya Rorya mkoa wa Mara.

Shughuli za mazishi zilienda kama zilivyopangwa hakika Mungu alikuwa ni mwema katika hilo lakini kwa bahati mbaya mama yangu hakuweza kufika kwa sababu kadhaa za kiafya kama ujuavyo watu wazima.

Kabla sijaanza safari ya kurudi Dodoma nimalizie michoro yangu alafu niende Dar kupumzika mama akanipigia simu akinisisitiza kwamba nipitie Bunda kwa shangazi mdogo wake na baba nimbebee samaki wake satto waliokaangwa vizuuuuri kabisa.

Sawa, nikasema isiwe kesi mimi huuyooo kutoka Tarime mpaka Bunda nikabeba samaki kisha nikasepa mpaka Mwanza nikalala siku moja pale guest moja ya Buzuruga kisha asubuhi huyo na bus la kuja Dodoma.

Bus ilikuwa inakuja mpaka Dar sasa mimi nilikata tiketi ya Dodoma kwa maana nina issues zangu huku. Nimeshuka ninapewa kondakta anatoa mizigo ya abiria kuangalia box langu halipo.

Daaaaah aiseee moto ulitaka kuwaka. Samaki hawapo? Nitamwambia nini bi mkubwa nikirudi Dar? Kumbe baada ya ukaguzi mzuri ikaja kugundulika kuna abiria mmoja alishukia huko Singida alikuwa na box kama langu ndio akaondoka nalo lakini yeye box lake likawa limebaki pale kwenye bus.

Alichokifanya kondakta akachukua lile box la abiria mwingine kisha akalipeleka ofisi zao kuu pale Dodoma akaniambia wewe nenda home ukalale kisha njoo baada ya siku mbili tutakupigia simu na utalikuta box lako la samaki hapa.

Sawa kwa kuwa ilikuwa ijumaa nikaenda jumapili asubuhi mida kama ya saa tano kasoro hivi nikakutana na yule yule jamaa aliyechukua box langu akiwa pale pale ofisini.

Baada ya kupiga story kadhaa nikaja kugundua kumbe anafundisha shule moja na mtoto wa mama yangu mkubwa pale pale Singida. Nilikereka lakini nikapata funzo moja.

Nikiwa ninasafiri begi/mzigo wangu unakaa katika boti ya pembeni inayotazamana na dirisha nililopo kiasi kwamba hata watu wakiwa wanashuka njiani ninakuwa ninaona ni nani anateremka na mzigo upi.

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Mwaka 2004 ruti ya Kimara - Kariakoo kabla ya kuja mwendokasi kuna baba mmoja aliwahi kuombwa na abiria mwenzie amsaidie kubeba begi kwa maana daladala ilikuwa imejaa sana.

Wakati wa kushuka yule jamaa mwenye begi akashuka kimya kimya akaondoka. Kumbe begi lilikuwa na bangi kilo kadhaa ndani.

Sitaki niendelee kusimulia kwa maana yule baba alitia sana huruma na ilibidi abiria ndio wamtetee kwa Polisi kuwa begi sio lake aliombwa tu na abiria mwingine amsaidie kubeba.

Hii dunia wee acha tu.
 
Kuna siku nilishuka Bus stand ya Shinyanga mjini mara nikashangaa kuna mtu ananipigia kelele ndani ya bus niliyokuwa nimepanda,
bus ikasimama na akashuka mdada fulani anadai Bag langu ni lake nikamuonesha alama ya Bag ila akawa ameshaachwa na Bus
 
Ukisoma comment yangu #2 kuna bibi mmoja jirani yangu ananiambia akina mama wengi waliokuwa wanashindwa malezi ya watoto walikuwa wanatumia njia hii katika kuwatelekeza watoto wao miaka hiyo ya 2003.
 
Mwaka 2015 natoka Arusha kwenda Dar, nafika Ubungo begi langu halipo ila kuna linalofanania, kufungua ndani limejaa nguo za watoto tu. Begi langu lilikuwa na vyeti vya kidato cha 4 na 6.

Mida ya saa 5 usiku napigiwa simu na mhudumu wa ofisi ya bus kwamba limepatikana nikachukue asubuhi yake. Baada ya mapumziko ya siku mbili nkaendelea na safari, awamu hii natoka Dar kwenda Tukuyu Mbeya, nashuka Tukuyu mjini naenda zangu guest kupumzika, natoka kuoga sasa nipake mafuta kufungua begi nakutana na nguo za watoto, kumbe nlishuka na begi la mtu na langu likapitiliza kwenda Kyela.

Kufupisha stori tu tangu siku ile nikisafiri na begi la kuweka kwenye buti huwa nalifunga kibendera cha kitambaa asee maana zile safari zilinipa tabu kweli afu msimu ule ndio Majinja ilikuwa imeua watu wengi sana Iringa, sisahau kabisa yale matukio maana matokeo yake yalinifanya nichelewe kuripoti kituo cha ajira hadi ikanibidi nirudi wizarani kuomba kupangwa upya.
 
Back
Top Bottom