Yehoyada Yedidia
Member
- Jan 20, 2015
- 16
- 33
Kwanza kabisa ni vyema unaposoma huu uzi upanue uelewe wako na kiwango chako cha kuyaangalia mambo kwa mapana na marefu.
Kwa miaka miwili mpaka mitatu sasa kumeibuka wimbi kubwa la vijana wachekeshaji (comedian) kila kona ya Tanzania. Ukiwakuta vijana wana camera mtaani lazima tu watakuwa wanarekodi kichekesho kwa ajili ya kusambaza mitandaoni.
Nawaza; je, watanzania wamepatwa nini mpaka soko la kutaka kuchekeshwa limeongezeka. Je, stress zimeongezeka? Watu hawataki tena mambo serious? Tunatoana kwenye mambo ya maana? Mpaka mtu mmoja anauliza kwani Tanzania ni channel ya vichekesho kwenye king'amuzi cha dunia?
Hii ikanifanya nianze kuangalia pia kwenye mitandao ya kijamii vitu vyenye ushabiki mkubwa ni vile visivyo na maana sana. Mambo mengi ya msingi hayatiliwi maanani tena. Ukiweza kuchekesha au ukavujisha video wewe unakuwa ni "mtu wa maana sana" kwa msemo wa sasa mjini.
Juzi siku ya Eid nilipata nafasi ya kumsikia Gwajima mbunge wa Kawe akitoa somo kwa wananchi kuhusu sekta tano ambazo zinaweza kutuinua kama taifa.
Gwajima anasema kilimo, uvuvi na ufugaji zikiwa ni sekta tatu kubwa zinaweza kuajiri mtu wa aina yeyote, kiwango chochote cha elimu na akafanikiwa. Gwajima anasema ni rahisi kwa nchi yetu kuwa "bakuli la chakula" kwa nchi za Afrika na ulimwenguni kote. Kwa aina ya nchi yetu ambayo ina mito na maziwa na bahari, nchi ikilimwa ya kutosha basi chakula hakitakuwa shida tena kwa watanzania.
Gwajima akaongeza kuwa mtu akishiba hata kuwaza kwake kunaweza kubadilika. Gwajima anasema kuna mashamba mengi yako pembezoni mwa maziwa na mito ambayo hayahitaji kabisa bajeti kubwa kuyalima. Kwenye hotuba yake Gwajima ameshusha takwimu za nchi kuvuna "maokoto" ya kutosha kutoka kwenye sekta ya kilimo huku akisisitiza mpango uwe wa MUDA MREFU.
Gwajima anasema mito na maziwa na bahari yetu pendwa sio sehemu tu kucheza wakati wa sikukuu ufukweni. Kuna samaki ambao uvunwaji wao ungelisogeza sana taifa. Gwajima aliwashauri wananchi kuchangamkia vizimba vya ufugaji katika maeneo yaliyoainishwa na serikali.
Akishusha desa kuhusu ufugaji Gwajima anasema wafugaji bado hawajatosha kwenye nchi hii iliyojaa nyika na mapori.
Kama mifugo ingekuwa inatosha basi viwanda vya kusindika nyama na maziwa na ngozi vingekuwa vingi sana. Gwajima anasema hapo ni vyema sana uwezeshaji uwe mkubwa sana kuhakikisha sekta hii inatema mpunga wa kutosha kwenye mapato ya nchi kuliko ilivyo sasa.
Nikawaza haya madini sasa mbona ni ya muhimu kuliko goal la Yanga ambalo linaangaliwa kila saa kama mtu kabandika maharage. Gwajima aombwe ashushe haya madini hata kwenye interview na media inayojielewa ambayo sio mali ya ukoo kusudi wengi hasa vijana wapate.
Tucheke lakini ukishavunjika mbavu kwa vichekesho akili yako iwaze Tanzania inaendaje na wewe Mtanzania unaendaje.
Nitarudi baadaye nimalizie yale niliyoyasikia yanayohusu mlima wa chuma na makaa ya mawe, mambo ya utalii na madini ya kutosha. Nikawaza wazalendo bado wapo na wenye kuipenda nchi bado wapo. #ChekaUkiwazaMaendeleo
Mkufya Majiponda