Je, tozo za simu zitakuwa chanzo cha uhakika cha ingizo la fedha?

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Feb 26, 2021
1,088
3,128
JE TOZO ZA SIMU ZITAKUWA CHANZO CHA UHAKIKA CHA INGIZO LA FEDHA.!?

Leo 10:15hrs 05/09/2021

Mwaka 2017,Rais wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli alikutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation ambayo ni mmiliki mkubwa wa kampuni ya Acacia Mining Limited Prof John L Thornton,taarifa kutoka ikulu zilisema katika mkutano huo walikubaliana kuwa kampuni hiyo ipo tayari kufanya mazungumzo na Serikali ya Tanzania ili kulipa fedha ambazo Tanzania imezipoteza kutokana na kampuni hiyo kuendesha shughuli nchini Tanzania,Je hii ilikuwa dhuluma!? Hapana,hiki kilikuwa chanzo cha kwanda cha kodi kuelekea kuset bar,kuweka standard na kukusanya kodi ya haki bila Mtanzania kudhulumiwa na mabepari kutoka kwenye rasilimali ambazo Mungu aliibariki Tanzania.

Baada ya Mazungumzo hayo Prof Thornton aidha alinukuliwa akisema kuwa kampuni yake ipo tayari kufanya mazungumzo na Tanzania yatakayozingatia maslahi ya pande zote mbili na pia ipo tayari kulipa fedha zote ambazo inapaswa kulipa kwa Tanzania,Kwa upande wake Rais Magufuli alisema Serikali inakaribisha mazungumzo hayo na itaunda jopo la wataalamu watakaofanya majadiliano na kampuni ya Barrick Jopo hilo litaundwa na wanasheria na maafisa wa serikali ili kufikia makubaliano ya kulipwa fedha zinazodaiwa na namna kampuni hiyo itakavyoendesha shughuli zake nchini maslahi ya pande zote mbili,hilo lilikuwa wazo la kwanza la kulipa kodi stahiki bila kudhulumu Rasilimali za Watanzania.

-Kodi kwa Wafanyabiashara wote Tanzania
Serikali ilipotambulisha EFD,walikupa mashine ya EFD baada ya mwaka walikuja kukokotoa jumla ya kodi kwa kutumia taarifa za EFD,it's obvious kodi ya EFD lazima iwe kubwa kuliko ile ya makadirio ya macho na kumsikiliza mteja ( Mfanyabiashara ) yaani " Self Tax assessment "Mathalani,kwa miaka kumi mfululizo kwakutumia Self Tax assessment ulikuwa unalipa kodi ya Tshs 1,400,000 kwa Mchanganuo wa 350,000|350,000|350,000||350,000 na kila mwaka ukapewa Tax clearance kwamba hudaiwi kodi yoyote,baada ya kutathimini kodi kutoka kwenye taarifa ya EFD tukakuta kodi yako stahiki ilipashwa kuwa Tshs 3,000,000 kwa mwaka,Sasa kwa kutumia Presumptive Tax Assessment tunasema hiyo tofauti yaani 3,000,000 - 1,400,000 =1,600,000,
Tunaangalia lesseni yako ni lini ulianza biashara,Mfano lesseni yako inasomeka 01|01|2011,Then, Tunachukua 2021-2011= 10Yrs,Hence,Tunachukua ile tofauti tunazidisha kwa muda uliofanya biashara,Yaani : 1,600,000 X 10 = 16,000,000"
Tunakupa Invoice ya Tshs 16M kama Tax arrears,Nimekupeni makadirio ya biashara ndogo tu,Nadhani mmeona kwanini watu walifunga account zao na kufungua kampuni mpya kikimbia kodi,kwa nini watu walifunga biashara na kukimbilia nchi jirani au walifungua biashara kwa majina mengine, Mfanyabiashara kamwe hapendi kulipa kodi ili apige Super normal profit,tuliona mapedeshee wakizunguka usiku mzima kugawa pesa kila Club ya usiku,Je pesa hizi za kuchezea walikuwa wanazitoa wapi!? Je kodi ilikuwa dhuluma au si dhuluma!?

-Rais Magufuli aliboresha sekta ya Utalii kama chanzo Cha kudumu cha kodi.

Mapato ya utalii nchini Tanzania yaliongezeka kwa asilimia 7.9 mwaka 2018 na 2019 kutoka Dola za Marekani milioni 2,412.3 mwaka 2018 hadi kufikia Dola za Marekani milioni 2,604.5 mwaka 2019,takwimu zilionyesha idadi ya watalii iliongezeka kutoka watalii 1,505,702 mwaka 2018 hadi 1,527,230 mwaka 2019.Jitihada za serikali ya awamu ya tano kwenye uwekezaji na utangazaji wa Tanzania kama eneo lenye vivutio vya kipekee vya utalii,wastani wa matumizi ya watalii kwa siku uliongezeka kutoka Dola za Marekani 193 mwaka 2018 hadi kufikia Dola za Marekani 266 mwaka 2019,watalii ambao hawakununua huduma kwa vifurushi, walitumia wastani wa Dola za Marekani 216 kwa mtalii kwa siku mwaka 2019 kulinganishwa na Dola za Marekani 135 mwaka 2018.Serikali ya CCM ya awamu ya tano ilinunua ndege za Tanzania na kulifufua shirika la ndege la Tanzania ili litumike kutangaza utalii na kwa hakika dhamira hiyo ilifanikiwa vyema kwani tuliona Watalii wakiongezeka,

Serikali ya CCM ya awamu ya tano,chini ya Rais John Magufuli iliboresha gharama za utalii na kuwavutia Watalii wengi hazipishani sana na za nchi jirani, na idadi kubwa ya watalii walitoka nchi za Marekani, Uingereza na Ujerumani katika kipindi cha mwaka 2019.Kwa takwimu za mwaka 2019 kwa nchi zilizopo kusini mwa Jangwa la Sahara,Tanzania ilishika nafasi ya pili kwa kuingiza fedha za kigeni kupitia sekta ya Utalii iliyoboreshwa vyema kwa dhamira na maono ya Rais Magufuli kama sehemu ama chanzo muhimu cha kukusanya kodi na sio tozo kwa Wananchi, kinara ilikuwa nchi ya Afrika ya Kusini.Rais Magufuli alidhamiria kuboresha miundombinu iliyokuwa hafifu katika mbuga za Taifa pamoja na kuyapandisha hadhi mapori ya akiba kuwa Mbuga za Taifa na pia kuongeza matumizi yaliyokuwa ya kiwango cha chini sana ya Credit card.Je kuboresha sekta ya Utalii ilikuwa dhuluma au si dhuluma!?

-Rais John Magufuli alilinda Rasilimali za Watanzania ili zilete kodi ya kuijenga Tanzania ya Viwanda.

Mwaka 2017,Rais wa Tanzania John Magufuli aliliagiza Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kujenga ukuta wa kuzunguka vitalu vya kuanzia A hadi D vyenye madini ya Tanzanite katika eneo la Mererani, Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara ili kudhibiti uchimbaji na biashara ya madini hayo,Rais Magufuli alitoa agizo hilo kwenye sherehe ya ufunguzi wa barabara ya Kia - Mererani iliyofanyika katika eneo la Mererani,Rais Magufuli amesema pamoja na kujenga ukuta huo haraka iwezekanavyo, soko la Tanzanite litapaswa kuwa katika eneo hilo, Tanzanite yote itapita kupitia lango moja na aliitaka Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kushiriki katika ununuzi wa Tanzanite.Rais John Magufuli alisikika akisema"Lile eneo la kitalu kuanzia A hadi D ambalo ndio lina mali nyingi ya Tanzanite, naagiza Jeshi la Wananchi kupitia Suma-JKT na wengine, najua wameshamaliza utafiti, waanze kujenga ukuta eneo hilo lote na kazi hii ifanyike haraka, watakapojenga ukuta wataweka kamera na patakuwa na mlango mmoja ambapo patajengwa vifaa maalum, nataka niwaeleze ukweli ndugu zangu wa Simanjiro hata kama utameza Tanzanite itaonekana"

-Serikali ya CCM,chini ya Rais Magufuli iliongeza Mapato ya madini baada ya kuimarisha udhibiti wa soko la madini nchini Tanzania.

Kuimarika kwa udhibiti wa shughuli za madini na kuongezeka kwa uzalishaji miongoni mwa wazalishaji katika migodi mikuu, hususan ile ya Geita na North Mara, kumeinua mapato yatokanayo na uuzaji wa nje wa madini ya dhahabu kwa Tanzania,Kwa mujibu wa tathmini ya uchumi ya mwezi April 2019 Benki kuu ya Tanzania (BoT) ya mwezi April, mapato yatokanayo ya uuzaji wa dhahabu yameongezeka kwa $100 milioni (takribani Sh223 bilioni) mwishoni mwa mwaka uliomalizika Machi, mwaka huu,ikilinganishwa na mwaka uliomalizika Machi, 2018.Tathmini hiyo ilionyesha kuwa mapato yanayotokana na mauzo ya nje ya dhahabu yaliongezeka kwa kiwango cha dola bilioni 1.68 katika mwaka uliomalizika mwezi Machi 2019 kutoka dola bilioni $1.53 kiwango kilichorekodiwa wakati wa mwaka uliomalizika Machi 2018.

Mafanikio haya katika sekta ya madini nchini Tanzania yanakuja baada ya Dkt John Pombe Magufuli kudhibiti Rasilimali ya madini kwa manufaa ya Watanzania,akamteua Profesa Shukurani Elisha Manya kuwa Kamishna wa Madini ambaye alikuwa ndiye Mtendaji Mkuu wa Tume ya Madini nchini baada ya kumfuta kazi Kamishna aliyekuwepo,Mnamo mwaka 2017, Serikali ya Rais John Pombe Magufuli iliazimia kupitia upya sheria katika Rasilimali za Watanzania, bunge la Tanzania likapitisha mabadiliko ya sheria tatu zilizoleta mabadiliko makubwa ya kisheria na mfumo wa taasisi zinazoongoza sekta ya mafuta, gesi na uzalishaji wa madini, Shukrani za dhati kwa Utumishi uliotukuka wa Rais John Pombe Magufuli,naamini uko ulipo una maisha mazuri baada ya kuisahau dunia na shida zake.

-Baada ya Kupumzika kwa Rais Magufuli,tuliobaki tukarudisha mpira kwa kipa.

Baada ya kupumzika kwa Rais John Magufuli,tukaanza kuona umuhimu wake ulikuwa wapi,wanyonge wakafahamu walichopoteza,Rais Magufuli katika uongozi wake aliamua kumpunguzia mzigo mwananchi wa kawaida haswa katika masuala ya kodi. Aliwakamua waekezaji wakubwa ambao walikuwa wakikwepa kodi kwa kudhibiti mianya yote ufisadi,rushwa na uvujaji wa Mapato,na kuhakikisha rasilimali za Tanzania zinajenga Tanzania mpya,Rais Magufuli aliwekeza akili kubwa kwenye miundo mbinu ya barabara sababu ndio kitu pekee ambacho kinaweza kukuza uchumi na kumgusa mtanzania wa kawaida,

Rais John Magufuli aliwaamsha Watanzania kwa kuwafumbua macho kwamba Tanzania ni tajiri na tukisimamia vizuri Rasilimali zetu,basi tuna uwezo wa kuijenga Tanzania na kuwa kama Ulaya,namkumbuka sana Rais wa Libya, Muammar Gaddafi aliyeijenga Libya kwa Rasilimali za Libya na kufikia kuwapa maisha mazuri Wananchi wake na kuanza kuwalipa Wananchi wake kila anayeoa na kumpa nyumba kila anayekwenda kuanzisha Familia mpya,Rais Ghadaf ndiye aliyepigania kuanzishwa kwa benki ya Afrika na yeye alijitolea kuingiza mtaji katika benki hiyo,yote hayo ni kutoka kwenye Rasilimali za Libya,Mambo yote mazuri yalitendeka baada ya kupigania Rasilimali ya Libya iwanufaishe Wananchi wa Libya na Jambo hilo,Rais Muammar Gaddafi alilifanikisha,kwa Tanzania,Rais John Magufuli aliwaambia Watanzania wao ni matajiri na ndio mabosi wa Rasilimali zao, Rasilimali nyingi Mungu ametujalia ili zitunufaishe Watanzania na sio wezi,mafisadi au mabepari,Hiyo peke yake ilitosha kufufua uzalendo wa Watanzania na kupenda nchi yao,itoshe to kusema kwamba,

Sasa tupo kwenye mlengo tofauti na maono ya Rais John Magufuli,tozo kwa kila Mtanzania ni kuhamisha kodi toka kwa wawekezaji na wafanya biashara wanaoshusha mizigo Zanzibar na kuiingiza Tanzania bara kwenye vijahazi kurudi kwa Watanzania ambao tayari maisha yamewapiga na hawana kitu. Hamasa ya kuwaleta Watanzania pamoja imepotea na kila Mwananchi anahofu kesha itakuja kodi gani ya kuzidi kumkamua,Shule za Msingi na Sekondari sasa hivi zimerudisha tozo kwa wanafunzi kama ilivyo kuwa Kabla ya JPM. Sasa hivi Wazazi masikini wana haha watapata wapi Shilingi 500 - 1,000 kila siku ili mtoto aweze sahishiwa mtihani na kukaa shule baada ya muda wa kawaida wa masomo.Ni dhahiri kwamba mabadiliko haya ya muda mfupi hayaja wakaa vizuri Watanzania. Pia italeta wakati mgumu sana kwa Chama Cha Mapinduzi katika kinyang'anyiro cha 2025.

Niseme kwa uchungu, Tanzania imepata hasara kubwa kwa kifo cha Rais Magufuli,Mungu angemwacha hadi maono take yatimie,Mapenzi ya Mungu yatimizwe hapa duniani Kama ilivyo mbinguni,Yupo mtabiri mmoja ametabiri "kipo Chama kipya kinakuja chenye sura na utambulisho wa chapa ya Nyati,ambacho kitakuwa mwiba mchungu katika Uchaguzi ujao,Hapa Kazi Tu","Shujaa amejikwaa juu ya Shujaa,wameanguka wote wawili"(Yeremia 46:12)

Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business.

-Master of Leadership and Management.

Recent Publication;-
-Assessment on the Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.
 
Ndiyo maana tunalia na katiba mpya itakayotengeneza mfumo imara na sio kutegemea mtu imara.

Siku MaCCM yatakua na akili timamu na kuelewa umuhimu wa katiba mpya ni zaidi ya huo uchu wao wa madaraka labda ni karne ye 30 huko.
Kumbaf.
 
Tunataka mifumo imara hata tukipata rais bogus mifumo inafanya kazi kamakawa....siomtu awe kama Mwalim mkuu utaweza wapi
 
Back
Top Bottom