Pyaar
JF-Expert Member
- Feb 11, 2018
- 15,567
- 75,998
Ukuaji wa uchumi wa nchi ni pamoja na matumizi ya teknolojia mbalimbali ili kuongeza uzalishaji na kuinua uchumi wa nchi na maendeleo kwa ujumla.
Katika Sekta ya uvuvi, kilimo cha samaki kimekuwa kikihimizwa kila leo kwa lengo la kuongeza uzalishaji ili kuendana na mahitaji ya soko.
Kwa Tanzania nimekuwa nikiona mabwawa yakichimbwa kwa ajili ya ufugaji samaki.
Lakini kumbe si mabwawa tu, pia fish cages zinaweza kutandikwa ziwani na uzalishaji wa samaki ukaendelea.
Kilichonifanya niandike hapa:-
i) Mbegu ngeni inayoletwa (Spp. ngeni)
Ufugaji huu unahusisha mbegu ngeni kutoka nchi za wenzetu (Tilapia spp) na inasemekana mbegu ngeni ni tamu ukilinganisha na hii ya kwetu ya asili.
Je, uwepo wa mbegu hii ngeni haiwezi kuitawala Spp. tuliyonayo, na mwisho wa siku tukapoteza kabisa ile ya kwetu?
ii) Aina ya chakula
Chakula kinachotumika kuwalisha hawa samaki inasemekana kina kemikali ambazo baadaye huwaathiri samaki majike na kugeuka kuwa madume.
Je, endapo hiyo kemikali itaathiri samaki wa asili na kukumbwa na mabadiliko hayo,kuzaliana kwa samaki wa asili kutaendelea kuwa sawa?
iii) Uvuvi haramu
Serikali yetu imekuwa ikipiga vita juu ya uvuvi haramu, je, huu uwekezaji hatuwezi kuuterm katika uvuvi haramu?
Wataalamu wa masuala ya uvuvi na kilimo cha samaki, naombeni elimu kuhusu hili.