Etugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 5,631
- 12,875
Kwa mtazamo wangu Tanzania hatuhitaji hicho kizazi hata kidogo,,kwa wengine wanaona hiyo generation ni babu kubwa na kutamani nasi tungekuwa nayo
Jirani zetu wakenya huenda wanastahili kuwa nayo kutokana na back ground yao,,kwa sababu ukabila ni sehemu ya maisha yao ya kila siku,hata siasa zao kwa mlengo mkubwa zina chagizwa sana na ukabila
Si ajabu hata hali hiyo kufikia sasa imehamasishwa sana na ukabila,,,tukio la hivi karibuni pamoja na raisi wao kutoamua kusaini huo mswada na kutaka urejeshwe bungeni lakini bado hiyo gen z inakuja na matakwa mengine ya kutaka kumtoa raisi wao madarakani
Hapa ndipo unapojiuliza je,kuna nini nyuma ya pazia? Unapata picha kwamba kuna ajenda kubwa ambayo imejificha nyuma yake,,,je vijana wataendelea kutumika kama daraja ili wenye ajenda zao wafanikishe mpango wao?
Hapa ndipo ambapo kijana unatakiwa utumie ule msemo wa Jk "akili za kuambiwa changanya na zako" mwisho wa kunukuu.
Mpaka sasa tumeona maafa makubwa yametokea,,kuna ambao wamepoteza uhai wao na kuacha majonzi katika familia,ndugu jamaa na marafiki.
Natambua kwamba ili mabadiliko yapatikane wakati mwengine baadhi yetu inatakiwa tujitoe mhanga ili kizazi kijacho kifurahie matunda yetu kama ambavyo wafanyakazi wa viwandani zamani walivyojitoa mhanga mpaka leo haki za wafanyakazi zinatambulika na kuheshimika kimataifa.
Kwanini nasema Tanzania hatuhitaji gen z? Kwasababu ukitaka kujifunza mambo kutoka kwa watu basi jifunze kupitia makosa yao,,kwani utapata kujifunza kuyaepuka makosa yao na kufuata yale ambayo yataleta tija zaidi .
Yaliyotokea kwa wenzetu tumeyaona tena sio mara ya kwanza,tuliwahi kuona vurugu kama hizi miaka ya nyuma na maafa mengi yalitokea, je nasi tunataka maafa kama hayo kwa kivuli cha gen z?
Hapana Tanzani tuna namna yetu ya kudili na mambo yetu,,kikubwa tutumie nguvu ya ballot box kuonyesha malengo yetu ni nini? Na pili ni kupaza sauti na kukosoa serikali kwa ustaarabu pale inapo bidi,,huu ndio ustaarabu wa taifa letu pendwa
Tusidhani kuingia barabarani na kuvunja amani ya nchi njia pekee ya kutatua kero zetu,,na siku zote njia ya mazumgumzo ndio njia muafaka katika kufikia maelewano,,wewe angalia hata katika historia,watu watanyanyua mitutu lakini mwisho wa siku watakaa mezani na kuyazungumza. Je kuna haja gani ya kuanzisha vurugu na kupata athari kubwa kisha baadae ndio tuje kuzungumza?
Mwisho Viongozi wa nchi hii,yanayo tokea kwa majirani nadhani mnayaona,,msingoje ikatokea gen z kama ya wenzetu ndio mje kusema lau tungejua,,nikiwa kama mtu aliye somea Sayansi ya Siasa nafahamu kwamba Kiongozi anatakiwa kunusa viashiria vya migogoro vikiwa katika hatua ya mwanzo kabisa kabla havijawa vikubwa na kuwa bomu ambalo kulishughulikia itachukua nguvu kubwa sana.
Viashiria tayar vipo hapa nchini kwetu tena vingi tu,basi tusiwe vyura kwani itafika kipindi watu watachoka na watasema kama mbwai mbwai,,sipendi tufikie huko,,hii nchi ni kisiwa cha amani na utulivu basi na iwe hivyo siku zote.
Gracias
Ni hayo tu!