Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 45,326
- 63,858
Laana ya rasilimali "resource curse" ni ile hali ya nchi zenye kuwa na rasilimali nyingi kuwa na maendeleo duni, ufisadi mkubwa, migogoro na demokrasia hafifu kutokana na wingi wa rasilimali ilizo nazo.Yani rasilimali walizo nazo inakuwa ndio kikwazo cha maendeleo yao kiuchumi na kisiasa.
Inasemekana katika baadhi ya maeneo ya dunia nchi ikishakuwa na rasilimali nyingi, raia wanakuwa wavivu kufanya maendeleo ya teknolojia yenye kutumia nguvu kubwa za akili, wanapenda kuagiza zaidi bidhaa za uchuuzi kuliko kutengeneza nchini mwao, wanaopenda kuishi kwa rushwa na urasimu wanakuwa wengi na pia migogoro ya aina mbalimbali inaongezeka sana hali inayodidimiza maendeleo.
Chukulia mfano wa nchi yetu
Ardhi, Tanzania ni nchi yenye ardhi kubwa sana lakini kila kona ya nchi kuna migogoro watu wanagombania ardhi.
Uchumi wa bidhaa, fremu na uchuuzi, Sehemu kubwa ya uchumi wetu ni biashara za kuchuuza bidhaa malighafi za kilimo, madini na za kutoka nje huko China. Sekta za teknolojia na viwanda ni duni sana.
Rushwa na ufisadi hilo wala halina ubishi, ni wimbo wa kila siku. Urasimu uliopitiliza nao ni tatizo kubwa kila mahali.