Je, takwimu za ufaulu wa mitihani ya kidato cha nne zinaelezea kuhusu uwezo wa wanafunzi kwenye masomo yao?

DaudiAiko

JF-Expert Member
Dec 2, 2012
365
303
Wanabodi,

Tupo katika kile kipindi cha mwaka ambacho kama kawaida, tuna rubuniwa kwa maneno matamu. Maneno matamu yanayoweza kutoa nyoka zaidi ya kumi pangoni. Ni kweli, hakuna marefu yasiyo na ncha na ukiona vya elea basi ujue vimeundwa.

Fahamu kwamba takwimu zozote zile zinaweza kutafsiriwa kwa njia nyingi na wachambuzi tofauti na tafsiri hizi tofauti huweza kuleta conclusions ambazo zinaweza kuonyesha kitu fulani kuwa kizuri au kibaya.

Ila takwimu ambazo nitajadili wala sio ngumu bali ni takwimu zinazo onyesha idadi ya wanafunzi walio faulu katika daraja la kwanza mpaka la nne kwenye mitihani ya kidato cha nne wa mwaka 2024. Kwa mujibu wa taarifa za NECTA, asilimia 92.37 ya wanafunzi waliofanya mitihani walifaulu. Takwimu hii haitupi taarifa za kutosha kuhusu ufaulu wa wanafunzi.

Kwa mfano, asilimia ngapi ya wanafunzi waliofanya mtihani walipata F zaidi ya tano kwenye masomo yao na bado wakakidhi kigezo cha ufaulu wa daraja la kwanza mpaka la nne?. Ufaulu wa somo la hisabati na kiswahili ulikuwaje kwa wanafunzi wenye ufaulu wa daraja la kwanza ikilinganishwa na daraja la nne?. Je matokeo mazuri kwenye masomo ya sayansi yalichochewa na wanafunzi kusoma kwenye shule binafsi?. Kati ya asilimia 92.37 walio faulu mtihani, ni wangapi wanakidhi vigezo vya kuchaguliwa kuendelea na kidato cha tano kwenye shule za serikali?.

Tofauti na kuendelea na kidato cha tano, Je mwanafunzi aliyefaulu kwa daraja la nne anafuzu kujiunga na chuo chochote na katika wadhifa upi?. kama wanafunzi wenye ufaulu wa daraja la kwanza na daraja la nne wote wamefaulu, kuna tofauti yoyote ya ubora wa wanafunzi wanapopata changamoto kwenye masomo mbalimbali?.

Soma Pia: NECTA yatangaza matokeo ya kidato cha nne 2024. Yatazame hapa!

Kama zoezi la kukusanya takwimu lingekuwa endelevu, tungeweza kufahamu maendeleo ya mwanafunzi mwenye ufaulu wa daraja la nne kwenye mitihani ya kidato cha sita na hata chuoni. Mpaka hapo, nafikiri umepata picha halisi. Utakuwa umeelewa kwamba sio nyeupe au nyeusi, kutoa takwimu ya idadi ya wanafunzi waliofaulu na waliofeli tu haitendei haki wanaotaka kufahamu undani wa matokeo ya mitihani ya kidato cha nne.

Kuwa na uhalisia kwenye takwimu kutaiwezesha serikali kuwa na mipango dhabiti inayolenga kuendeleza wanafunzi wenye uwezo mkubwa darasani na ambao watahitaji kupitia njia ndefu zaidi ili kutimiza malengo yao kielimu. Sambamba na hayo, ni vyema kuwa na mfumo wa elimu unaolenga kudemonstrate ufaulu kwenye mitihani na uwezo wa wanafunzi kwenye uhalisia wa fani zao
 
Back
Top Bottom