SI KWELI Prof. Mkenda asema ‘Mwanafunzi asiyefikisha GPA ya 3.8 ataondolewa sifa za kupata ajira’

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Salaam ndugu zangu,

Nimekutana na picha ya JamiiForums ikienea ikionesha ujumbe wa Prof. Mkenda unaodai kuwa kwa sasa vigezo vya kupata kazi kwa Wanafuzni ni kuwa na GPA 3.8. Jambo hili limenistua.

Je kuna ukweli hapa? Picha yenyewe hii hapa chini:

1692345772593.png
 
Tunachokijua
Kumekuwapo habari inayodaiwa kuwa ni ya JamiiForums ikimuhusisha Waziri wa Elimu Prof. Mkenda kusema kuwa kwa sasa vigezo vya kuajiri wanafunzi wa chuo ni kuwa na ufaulu usioupungua GPA 3.8. Ujumbe huu umekuwa ukisambaa kwenye makundi sogozi ya mitandao mbalimbali ikiwamo WhatsApp na Telegram. Habari hiyo imesambaa kutokana na kuenea kwa picha iliyoletwa na mleta mada hapo Juu.

Je kuna ukweli wa taarifa hii?
JamiiForums imefuatilia taarifa na picha hiyo inayosambaa na kubaini kuwa picha hiyo ilitumika katika mitandao ya Kijamii ya JamiiForums siku ya Julai 28, 2023 lakini sehemu ya maandishi ya picha hiyo ilihaririwa kwa lengo la kupotosha.

Picha hiyo ilitumika katika mitandao ya kijamii ya JamiiForums kutoa taarifa ya vigezo vya wanafunzi watakaopata Ufadhili wa masomo wa Rais Samia. Soma: Hapa Sehemu ya taarifa hiyo Prof Mkenda anasema:

“Ufadhili wa Samia ni kwa Wanafunzi wa Shahada ya Kwanza waliopata ufaulu wa juu kwenye Masomo ya Sayansi, wakianza kusoma hawatakiwi kushuka ufaulu, Mwanafunzi ambaye hatafikisha ufaulu wa gpa 3.8 ataondolewa ufadhili wa Rais Samia na kuingizwa kwenye mikopo ya kawaida ili waendelee kusoma.”

1692346698778-png.2720604

Picha halisi iliyotumiwa na JamiiForums kutoa taarifa Julai 28, 2023

1692345772593-png.2720588

Picha yenye maandishi yaliyohaririwa na kusambaa kwenye mitandao ya Kijamii
Aidha, JamiiForums imebaini kuwa Wakati mwingine ambapo Waziri Mkenda alizungumzia masuala ya GPA ilikuwa ni Desemba 12, 2022 ambapo alipoeleza kuwa Serikali itaanza kutozingatia kigezo cha GPA pekee katika ajira za Vyuo Vikuu, na badala yake kuzingatia uwezo kwa kupitia mchakato wa usaili. Soma: Hapa

Hivyo, JamiiForums inasisitiza kuwa ujumbe ulioambatana na picha hiyo hauna ukweli.
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom