Je, Primier Bet ni matapeli?

Aputwike

Senior Member
Aug 9, 2016
172
189
Wasalaam wanajukwaa.

Kwa uchache tu, naomba kuleta malalamiko yangu hapa, hususani kwa wale kamati ya kubashiri.

Huwa napenda sana kutumia kampuni ya bahati nasibu ya Primier Bet, lakini wanamatatizo mawili makubwa.

Tatizo la kwanza, ambalo naliona limekaa kitapeli, ni pale unapo toa pesa kwenye account yako ya M-Pesa, tigopesa, au Airtel Money nk, na kuingiza kwenye account yako ya Primier Bet(app), mara nyingine huwa haifiki(inakuwa pending). Na hii unaweza usiipate daima. Kwa upande wangu, hili tatizo limenitokea karibia mara mbili. Na mara zote nimewapigia sikuwahi kufanikiwa kuipata hiyo pesa kuingia kwenye account yangu ya P. Bet. Nikiwapigia, wakipokea wanasema niwatumie muamala, lakini mwisho wa siku hawaingizi wala kurudisha hiyo pesa. Nimetuma sana miamala lakini hola. Kila atakayepoke, habari ni "nitumie muamala" na hakuna wanachofanya. Sasa hii ni wiki ya pili. Kama nilivyokata tamaa kwa pesa ya kwanza ikapotelea kwao, na hii sasa nakwenda kukata tamaa ili waendelee na utapeli.

Jambo la pili, ni hii namba yao ya 0621444666 ya huduma kwa wateja. Ni namba ambayo mara nyingi haipatikani, na ikipatikana ni marachache, yaani wanapatikana wanapojisikia utafikiri ni mtu binafsi na si kampuni.

Nimeandika haya, huenda kuna mtu(wale wanao bashiri) aliwahi kukumbwa na kadhia kama hizi. Na zaidi, naomba hawa Primier Bet, kama wanavyo wahi kuchukua pesa zetu, basi wawe na uharaka wakutatua kero hizi. 'Win win situation' ndiyo inayotakiwa, na si utapeli wanaoufanya.

Asanteni, na naamini manung'uniko haya yatawafikia.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kama ulisha ona tatizo tena zaidi ya mara mbili si bora ukahama kampuni. Ya nini ung'ang'anie wakati unapata hasara kila siku, kuna kampuni nyingi tu tena nzuri. Hamia betpawa hawana ata makato

MGC
 
Back
Top Bottom