Je, ni wakati sasa wa kuwa na Wizara ya Malalamiko (Ombudsman)?

Masokotz

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
3,677
6,049
Habari za Wakati huu,

Kwanza niseme tu kwamba andiko hili limekuwa inspired na Mgomo wa Wafanyabiashara wa Kariako pamoja masuala mengine ambayo yamejitokeza hapa nchini katika kipindi cha nyuma.Kimsingi kama nchi tunao mfumo wa kiserikali ambao unahusisha Bunge,Serikali na Mahakama.Hata hivyo katika kutazama mambo kwa kina nimegundua kwamba bado huu mfumo ambao tumecopy and paste sio effective katika kuongeza tija na uwajibikaji wa wananchi.

Hoja yangu leo ni je, sasa ni wakati wa kuwa na ofisi ya malalamiko?Ofisi hii kazi yake ni kupokea malalamiko ya wananchi na kuyafikisha kwenye mamlaka za juu za kimaamuzi ilikuweza kutafuta muafaka wenye kuzingatia maridhiano na uelewano.

Hizi ofisi za Ombudsman ndio zitapokea maandamano yote,malalamiko yote,kero zote na migogoro yote ambayo haina msingi wa kuamuliwa na Mahakama. Na iwapo baada ya kuyatazama yanaonekana ni ya kwenda Mahakamani basi wahusika wataelekezwa kwenda Mahakamani.

Kwa Mfano. Mtu akienda Mahakamani na ikaonekana kwamba kuna mambo ambayo hajapendezwa nayo kwa ujumla wake basi anaenda Ofisi ya Malalamiko ambapo ni lazima asikilizwe,aeleweke, aeleweshwe na kuridhishwa.

Kwa Mfano Ofisi hii itamuuliza Mtu Maswali Matano:
  1. Je, Malalamiko yako Yanahusu nini?
  2. Je, ni Maamuzi/hatua/huduma gani ambayo hukubaliani au hukuridhishwa nayo?
  3. Je, ulitaka/Ulitarajia Maamuzi/huduma/hatua gani zichukuliwe katika kushughulikia suala lako
  4. Je, unafikiri kilichosababisha maamuzi/huduma/hatua ulizotaka zifanyike zisifanyike ni nini?
  5. Je, unataka tukusaidieje?au nini kifanyike(Mfano)
    1. Watumishi/Wahusika Wawajibishwe
    2. Sheria/kanuni/taratibu zirekebishwe
    3. Nipewe Taarifa zaidi/Elimu
    4. Suala langu lishughulikiwe kama ambavyo nilitarajia/nilitaka
Wakishapokea hayo malalamiko wao Jukumu lao ni Kutuma Taarifa kwa kitengo Husika ambacho kilitoa huduma na kuwaelekeza juu ya namna na malalamiko ambayo yamepokelewa, Mtoa malalamiko anaweza kuwa na uhuru wa kutoa malalamiko anonymously au kwa kujitambulisha, Malalamiko yanaweza kutolewa kwa njia ya simu, Email, Barua ya Posta na hata pia yanaweza kukusanywa kwa njia ya kuzungumza na Vikundi.

Katika malalamiko yote ni lazima mlalamikaji ataji kwa uwazi ofisi ambayo alihudumiwa. Wakuu wa Vitengo wapewe Time limit ya muda wa kushugulikia malalamiko hayo na kuyatolea ufafanuzi.

Ninaamini hili litaongeza uwazi na Uwajibikaji wa Watumishi na Pia kuongeza uwajibikaji na uelewa wa wananchi wa masuala mbalimbali.

Mwisho wa kuwasilisha.

PS. Nafikiri Pia itapendeza kama Ikitungiwa sheria na kanuni zake ili kuongeza uwajibikaji wa kisheria.Ikiwamo wa kuwajibika kutoa taarifa kuhusu malalamiko waliyopokea na hatua zilizochukuliwa na/dhidi ya wahusika.
 
Naona CCM mnataka kujiundia taasisi nyingine kupiga hela. Hakika adui mkubwa wa taifa hili ni CCM!

Bila katiba mpya, TUNAJIDANGANYA!
 
Naona CCM mnataka kujiundia taasisi nyingine kupiga hela. Hakika adui mkubwa wa taifa hili ni CCM!

Bila katiba mpya, TUNAJIDANGANYA!
Mkuu,Umetazama Taasisi au Umetazama CCM au Umetazama Hoja?Hebu jaribu kutazama hoja tuijadili then CCM na Ulaji Tutajadili wakati mwingine.
 
Gharama ya kuendesha hiyo wizara ni kubwa kuliko kumwondoa madarakani anayelalamikiwa kwakuwa hajui wajibu wake
 
Back
Top Bottom