Je, ni umri upi sahihi wa kijana kuoa?

Nov 11, 2019
58
70
Ndugu zangu, napata shida sana kuelewa mawazo tofauti tofauti ya wazazi na walezi wetu.

Mara zote wazazi wangu na walezi pamoja na ndugu na jamaa wanao wanaonizunguka wamekuwa wakisisitiza nioe mara baada ya kuona nimepiga hatua flan kielimu na kiuchumi..

Na mara zote wamekuwa wakisisitiza nioe kwani kuoa ni ufunguo wa riziki, ufunguo wa uchamungu na usafi wa roho na zaidi ni ulinzi wa machafu yote yasiyo mpendeza Mungu.......

Nikiwa na umri wa miaka 24 naona bado nahitaji kuendelea kutafuta ili kujijenga kiuchumi,

Bahati mbaya wengi wamekuwa wakisisitizwa kujiandaa kabla ya kuoa, naomba kujua ni vipi vya kujiandaa kabla ya kuoa?

Regard
Songorokajr
 
Mkuu swala umri sahihi kuoa, inategema maswala makuu mawili, moja ni kupevuka kiakili na kupevuka kimwili. Hivyo unaweza ukawa umepevuka mwili (miaka imekuwa mingi) na ukawa huajapevuka kiakili (uwezo wa kuhudumia familia, uchumi n.k). Basi hakuna umri specific wa kuoa ingawa kuanzia miaka 23-27 ni umri unaongaziwa na jamii ili kutoleta sifa mbaya ya kuchelewa kuoa.

Ni maoni tuu
 
Ndugu zangu, napata shida sana kuelewa mawazo tofauti tofauti ya wazazi na walezi wetu.

Mara zote wazazi wangu na walezi pamoja na ndugu na jamaa wanao wanaonizunguka wamekuwa wakisisitiza nioe mara baada ya kuona nimepiga hatua flan kielimu na kiuchumi..

Na mara zote wamekuwa wakisisitiza nioe kwani kuoa ni ufunguo wa riziki, ufunguo wa uchamungu na usafi wa roho na zaidi ni ulinzi wa machafu yote yasiyo mpendeza Mungu.......

Nikiwa na umri wa miaka 24 naona bado nahitaji kuendelea kutafuta ili kujijenga kiuchumi,

Bahati mbaya wengi wamekuwa wakisisitizwa kujiandaa kabla ya kuoa, naomba kujua ni vipi vya kujiandaa kabla ya kuoa??

Regard
Songorokajr
Miaka 30 basi
 
Aloooooooo.
we oa unapojiona akili yako imekomaa na imepembuka katika kukabili majukumu ya familia.
 
Mkuu hakuna umri maalum ila unashahuriwa tu usipite miaka 32 ukichelewa sanaa uoe ukiwa na 34 ila pia mwanzo uwe na 27 na kuendelea

Cha umuhimu kikubwa uwe na uchumi wa kueleweka kidogo usioe alafu haujui mtakula nn! Wewe na mwenzako kingine umpate partner wako anayekupenda kweli na kukuheshimu Kama unavyotakiwa wewe kumuheshimu nakumpenda pia

Kingine usiwe na udhuru uwe mwanaume sawa sawa usije ukaoa alafu mambo yako hayapo Sawa huko chini wazi tu hautakuwa unamridhisha mtoto wa watu itakuwa Sawa na bure tu

All in all kupata mwenza wa maisha siku hizi ni shughuli pevu
 
Hakuna umri sahihi wa kuoa! We ukijiona unajiweza kiuchumi we oa tu hakuna tatizo, but usioe kama bado hujajiweza kiuchumi utaisumbua familia yako na utawapa shida watoto wako
 
Back
Top Bottom