LGE2024 Je, ni sawa kwa Viongozi wetu wa Mtaa kututoza pesa ili watupigie mihuri kwenye shida zetu?

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
2,170
5,525
Salaam ndugu zangu,

Aisee kumekuwa na tabia ya viongozi wa Mitaa mbalimbali kugeuza shida za Wananchi kama miradi yao ya kujipatia pesa.

Mpaka sasa kwa hapa Dar es Salaam nimeishi mitaa mitatu na nimefanikiwa kufika Ofisi za Serikali za Mitaa kwa ajili ya kupata barua ya Utambulisho.

Cha ajabu viongozi hawa wamekuwa wakiandika barua hizo na kupiga mihuri kwa pesa. Kitu kinachotia shaka ni kwamba kila mtaa huduma ni hiyo hiyo lakini bei ni tofauti. Kuna mtaa nilitozwa 3000, mwingine 2000, na mwingine 5000.

Sasa hapa najiuliza je ni sahihi kulipia kuhudumiwa na Viongozi wa serikali za mitaa? Je, suala hili lipoje Kikanuni?

Vipi wewe mtaani kwako unapohitaji huduma kwa viongozi wa mtaa unalipia?
 
Mkuu viongozi wa serikali za mitaa, vitongoji, na vijiji ambao huchaguliwa na wananchi huwa hawalipwi mshahara wowote ule. Hizo ni kazi za kujitolea tu.

Kwa hiyo wana utaratibu wao wenyewe wa kujiwekea vyanzo vyao vya mapato yao. Na kimojawapo ni kupitia huduma hizo wanazozitoa kwa wananchi wao.

Kwa hiyo basi ni kama vile umechangia kidogo kwa viongozi wako. Ijapokuwa ni vigumu sana kupata risiti.
 
Sasa hapa najiuliza je ni sahihi kulipia kuhudumiwa na Viongozi wa serikali za mitaa? Je, suala hili lipoje Kikanuni?

Vipi wewe mtaani kwako unapohitaji huduma kwa viongozi wa mtaa unalipia?
Swali moja hua unaulizwa umeishia hapa kwa muda gani? Km ni chini sana ya umri wako lazima wakuchaji kimfano una miaka 30 unaulizwa umeishia hapa kwa mda gani ukisema miaka yote 30 hawana tatizo na wewe unapigiwa bure ukisema miaka 2 au 3 wewe unaonekana wa kuja lazima uchajiwe tu na kweli lazima ikutoke maana huna namna
 
Hii ndio CCM na bado mbali na hilo atataka umpe ya Chai au Lunch.
Utadhani umemuajiri wewe na halipwi mshahara!!

Tufike mahali iwe BASI!
Sio Serekali ya Mtaa tu mapaka mjumbe wa nyumba 10 anataka umpatie chochote wanaita hela ya kombe yaan zile copy za karatasi inabidi uchangie maana zile sio bure pamoja na wino wa muhuri Ila km ukiwa born hiahia hawakusumbui
 
Hawajitolei na hakuna aliyewalazimisha kuwa viongozi, kodi au toro za serikali lazima zipitishwe kisheria, wanachofanya ni illegal
 
Huelewei maana ya kujitolea, ukijitolea haupangi utalipwa nini au kiasi gani, unayemhudumia ndio anaamua.
 
Hawajitolei na hakuna aliyewalazimisha kuwa viongozi, kodi au toro za serikali lazima zipitishwe kisheria, wanachofanya ni illegal
Wakuja wakikujua lazima ulipie chochote maana wewe unapita TU sasa ulisikia wapi mtu kaenda dukani kapewa bidhaa alafu asilipie? Ndio maana wanakuuliza umeishia hapa mda gani? Wakiona wewe ni mkulungwa miaka yote umeishia hapo hawakuombi hata 100 yako unapewa huduma bure
 
Watu wanauza mifugo na mazao ili kuhongo wapate uenyekiti wa Kijiji / vitongoji huku wakijua hivyo vyeo havina mshahara hivyo mishahara yao ni huko kushikilia mihuri tu maana hakuna fungu linalotoka Serikalini.
 
Hebu fanya utafiti ujue bajeti/fedha ya ofisi ya serikali ya mtaa wanapewa bei gani kwa mwezi,ukijuwa tu
Hapo utajuwa kwanini wana wa charge gharama ya mihuri nk

Ova
Ni heri mtaa upitishe tozo tasmi za kuhudumia ofisi ya mtaa kila mwezi kuliko kufanya mambo kienyeji.
 
Na hili agizo la Jerry Slaa kutaka hao viongozi wa mitaa wasitumike kwenye mchakato wa mauziano ya ardhi itasababisha hiyo mihuri wagonge hata kwa 50K.

Maana mrija nuo umekatwa!
 
Rubbish
 
Sio Serekali ya Mtaa tu mapaka mjumbe wa nyumba 10 anataka umpatie chochote wanaita hela ya kombe yaan zile copy za karatasi inabidi uchangie maana zile sio bure pamoja na wino wa muhuri Ila km ukiwa born hiahia hawakusumbui
Na mjumbe wa nyumbe kumi hata sio rasmi katika mfumo wa sasa wa vyama vingi.
 
Rabbit au Rubbish utajua utakapochajiwa 2000/3000/5000 na lazima utoe bila hivyo karatasi yenyewe yenye muhuri haupewi sio hapo TU hata ukienda mahakamani shughuli ni hio hio lazima ulipie muhuri na Saini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…