Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,170
- 5,525
Salaam ndugu zangu,
Aisee kumekuwa na tabia ya viongozi wa Mitaa mbalimbali kugeuza shida za Wananchi kama miradi yao ya kujipatia pesa.
Mpaka sasa kwa hapa Dar es Salaam nimeishi mitaa mitatu na nimefanikiwa kufika Ofisi za Serikali za Mitaa kwa ajili ya kupata barua ya Utambulisho.
Cha ajabu viongozi hawa wamekuwa wakiandika barua hizo na kupiga mihuri kwa pesa. Kitu kinachotia shaka ni kwamba kila mtaa huduma ni hiyo hiyo lakini bei ni tofauti. Kuna mtaa nilitozwa 3000, mwingine 2000, na mwingine 5000.
Sasa hapa najiuliza je ni sahihi kulipia kuhudumiwa na Viongozi wa serikali za mitaa? Je, suala hili lipoje Kikanuni?
Vipi wewe mtaani kwako unapohitaji huduma kwa viongozi wa mtaa unalipia?