Je, ni kweli Waalimu wa madrasa walitumiwa na Wajerumani kufundisha watoto wa Kiafrika elimu ya kizungu?

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
3,212
7,260
Wadau Uzi hii naomba usiunganishwe kwingineko na ujadiliwe kwa kushahidi au takwimu za historia

Je, ni kweli walimu wa madrasa walitumiwa na Wakoloni Wajerumani kufundisha watoto wa Kitanzania?

Kwamba walimu wa madrasa walijua kusoma na kuandika kiarabu hivyo ikawa rahisi kwao kujifunza na kuelewa lugha ya kijerumani na kiingereza kwa urahisi kuliko wale wasiojua kusoma kabisa.

Kwamba shule iliyotumika ilikuwa ni pale ilipo sasa Hospital ya Ocean road?

Kwamba Walimu halo walikuwa mahiri na weledi mkubwa kwenye eneo la kufundisha na walipendwa na kukubalika na Wajerumani.

Kwamba waalimu hao waliendelea na imani yao ya Uislamu pamoja na kufanya Nazi za Wajerumani

Naomba Mchango wenu kwenye hilo.

Mzee wetu Mohammed na Paschal Mayala tunaomba Mchango wenu
 
Back
Top Bottom