Je, ni kweli Adhabu ya Viboko inasaidia kuongeza Nidhamu na Uelewa kwa Mtoto?

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
668
1,076
1714407695519.png

Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye Sheria inayoruhusu Adhabu ya Viboko kwa Wanafunzi Shuleni licha ya adhabu hiyo kutajwa na kupigwa marufuku kwenye takriban Mataifa 51 ikielezwa kuwa ni ya Kikatili na inayoumiza badala ya kufundisha

Ili kufahamu zaidi, Shirika la Save the Children na WILDAF kwa watafanya Mjadala kuhusu Adhabu ya Viboko na Athari zake kwa Watoto kupitia XSpaces ya JamiiForums, Jumanne Aprili 30, 2024 Saa 12 Jioni hadi saa 2:00 Usiku

Shiriki Mjadala https://jamii.app/SaveTheChildren

Pia unaweza kuweka maoni yako kwenye uzi hii na yatasomwa siku ya mjadala

Karibu
---
MJADALA UMEANZA
Siku ya Kimataifa ya Kukomesha Adhabu ya Viboko' huadhimishwa Aprili 30 kila Mwaka. Je, kwa mtazamo wako kulinganisha na hali halisi iliyopo Shuleni na Nyumbani, unadhani Viboko vinasaidia malezi ya Mtoto na Adhabu gani inaweza kuwa mbadala wa Viboko?

UPDATES
WAKILI BARNABAS KANIKI, Save the Children

Mpaka leo (Aprili 30, 2024) ni Nchi 67 zimeweza kukomesha adhabu ya vibokoLeo pia Nchi ya Sri Lanka imepitisha Sheria ambayo inakataza Adhabu hiyo

Mjadala kama huu unaweza kurahisisha jinsi ambavyo Wadau tunaweza kufanya kazi na Serikali ili kumwezesha Mtoto kusoma katika Mazingira mazuri na kujua ni njia zipi zinaweza kutumika kumuadhibu

ANATOLI RUGAIMUKAMU, Mkurugenzi wa Uendeshaji Programu - Save The Children
Madhara ya Adhabu ya Viboko yanaweza kusababisha changamoto ya Afya ya Akili, Kimwili na KihisiaTumeshuhudia mara kadhaa na hata ikiripotiwa katika Vyombo vya Habari, Watoto wakipoteza Maisha kutokana na kuadhibiwa kupitiliza

Watoto wanaopata adhabu ya viboko mara nyingi wanapata madhara ya kushindwa kujiamini, hali hiyo imeenda pia hadi hatua ya ukubwani na inawaathiri hata katika Maisha yao ya kila siku

Adhabu ya viboko pia inaweza kusababisha matatizo ya Akili kwa Mtoto kuwa na changamoto ya kusahau

Mtoto ambaye anaathiriwa na Adhabu ya Viboko hawezi kuwa na ufanisi mzuri darasani, mara nyingi wamekuwa wakifeli katika mitihani yao au masomo kwa jumla

Nimesoma Ripoti ya WHO (Shirika la Afya Duniani), Watu wanaopata ukatili wa viboko wanaweza kuwa na matatizo ya Presha, Magonjwa ya Akili na wasiwasi wanapokuwa Watu wazima

Ninasema kuwa matumizi ya viboko sio njia sahihi kwa kuwa inasababisha maumivu ya kisaikolojia na Akili, madhara yake Mtu anaishi na hali hiyo Maisha yake yote na kupunguza utendaji wake katika masuala mbalimbaliKama Nchi na Wadau kwa ujumla tunahitaji kuwa na sauti moja ili kuhakikisha adhabu ya viboko inakoma

ANNA KULAYA, Mratibu Kitaifa - WiLDAF
Wakati tunajadili suala hili, tunatakiwa kujiuliza kutoka ndani ya mioyo yetu kama tunaamini Adhabu ya viboko ni sahihi, jiulize ulivyomchapa mtoto kuna faida gani imepatikanaPia, kwa kizazi cha sasa unatakiwa kujiuliza ukiwa mzazi je, ni sahihi kuendelea na Adhabu ya Viboko?

Kama Nchi tumesaini mikataba mingi ya Haki za Binadamu na kulinda Watoto, hivyo tunatakiwa kuzingatia mikataba tuliyosaini na uwepo wa Adhabu za VibokoPia, tujue tunapozungumzia Adhabu hiyo maana yake ni nini? Tafsiri zipo nyingi lakini lengo ni kutumia nguvu ili kumfanya Mtu aumie na imekuwa ikitolewa sehemu nyingi kuanzia ngazi ya familia

Tafsiri ya Kamati ya Haki za Kiraia ya Umoja wa Mataifa imekuwa ikieleza kuwa Adhabu ya Viboko ni sehemu ya ukatiliKwa Tanzania tuna Sheria ambayo ilifanyiwa maboresho Mwaka 2017, ukisoma inaelezea kuhusu Adhabu ya viboko, imetafsiriwa kuwa kuanzia Umri wa Miaka 16 ni Mtu mzima

Sheria inaeleza kuwa baadhi ya mambo ambayo ni halali kwa adhabu ya viboko mfano Ujambazi, Wizi wa Ng’ombe, Ubakaji na mengine kadhaaUkiangalia Sheria imeeleza makosa ambayo unayaona ni makubwa, sasa inakuwaje kwa Adhabu kubwa kama hizo kwenda kutekelezwa kwa Watoto

Pamoja na yote hayo Sheria zetu za Nchi ikiwemo ya Corporal Punishment Act zinaruhusu Adhabu ya viboko

Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Watoto umetaja Nchi Wanachama kulinda Watoto, Mkataba wa Afrika wa Watoto nao unaeleza kuwa Watoto wanatakiwa kulindwa

Kama Nchi pia tumekuwa tukiripoti Kamati mbalimbali za Kimataifa, zipo kama Kamati 6 zinazohusika na Mikataba mbalimbali na zimekuwa zikielekeza moja ya sehemu ya kuangaliwa ni kufanya uwezekano wa kufuta Adhabu ya Viboko

Ukiangalia Sheria ya Corporal Punishment Act Pamoja na Sheria nyingine za Nchi zinakinzana juu ya uwepo wa Adhabu hiyo

Mfano kwa Shuleni, Adhabu ya Viboko inatakiwa kutolewa kwa ruhusa ya Mwalimu Mkuu na kama hayupo anatakiwa kukaimisha maelekezo kwa maandishi juu ya Adhabu hiyo, tujiulize je kwa uhalisia hilo linafanyika?

Tafiti nyingine zinaonesha kuwa baadhi ya Walimu wamekuwa wakitumia Adhabu ya Viboko kama sehemu ya kuondoa hasira au Msongo wao wa Mawazo jambo ambalo si sawa kwa kuwa kila Binadamu ana haki ya kuheshimiwa Utu na Heshima yake

MICHAEL KITAMBI, Mwalimu
Viboko vimekuwa vikitumika tangu enzi za mababu zetu lakini binafsi naona Viboko sio njia sahihi ya kumuelimisha au kumfundisha Mtoto, njia hiyo imekuwa ikichangia kuwapa Watoto hofu, tunaona kupitia maeneo yetu ya kaziMtoto anaweza kuogopa kwenda shule kwa kuwa tu kaona kuna Mwalimu fulani anatoa adhabu ya viboko

Miaka ya hivi karibuni kumekuwa na matukio mbalimbali ya kusababisha vifo kutokana na Adhabu ya Viboko

Pia, wapo ambao wamepata madhara ya Kimwili kwa kuchapwa sehemu ambazo sio sahihi na hazitakiwi kusumbuliwa, tunayaona hayo yanatokea kwenye maisha yetu ya kazi za Ualimu

Nikiwa nasoma Darasa la Tano kuna Mwalimu wa Hesabu alikuwa anatoa Adhabu kali ya Viboko, hiyo ikasababisha niwe nakimbia somo lake, sijamsahau huyo Mwalimu kwa kuwa alichangia msingi wangu mzuri wa Hesabu uharibike.

Nilipokuwa 'level' ya juu ilitokea hivyo pia kwa Mwalimu wa Somo la Bookeeping, naye akasababisha nikakimbia somo hiloLeo hii nimekuwa Mwalimu, kilichonitokea nakiona kinatokea kwa baadhi ya Wanafunzi dhidi ya Walimu wanaotumia staili ya viboko

Nilipokuwa nasoma nilikuwa namuelewa vizuri Mwalimu ambaye alikuwa akiniita na kuniambia nimekosea hapa na hapa

Tujiulize Adhabu ya Viboko imesaidia nini au nani amekaa kwenye mstari kwa kuwa tu kuna Adhabu ya Viboko?

Wengi wao wanaochapwa wanatengenezewa usugu na uadui na pengine kutokea kama kilichonitokea mimi kwa kukimbia Somo la Mwalimu anayetumia Adhabu ya Viboko kwa wingi

SONIA VOHITO, Mtaalamu Mkuu wa Sheria wa WHO-New York
Nchi ambazo zimezuia Adhabu ya Viboko Duniani mpaka sasa zinawakilisha 14% ya Watoto Duniani

Adhabu ya Viboko inaathiri Ubongo na ukuaji wa Mtoto, anashindwa kuwa makini katika vitu, anaumia kimwili na kupata majeraha makubwa, wapo ambao wanakimbia shule kabisaAfya ya Akili pia inaweza kuathiriwa na Adhabu ya Viboko

Adhabu ya Viboko inaweza kuchangia Watoto kuwachukia Walimu waoPia, kuna Walimu ambao wanatumia Adhabu hiyo kama kufanya ukatili wa kijinsia hasa kwa wale Walimu Wanaume wanaofanya hivyo kwa Watoto wa kike waliowakataa

Ili kuondoa Adhabu ya Viboko tunatakiwa kuwa na nguvu ya kisiasa pia, kama kukiwa na mwitikio wa Wanasiasa wanaweza kusaidia kupigia kelele adhabu hiyo ikaondolewaTunatakiwa kuwaelimisha Walimu, Viongozi wa Dini jinsi ya kuripoti na kukemea masuala ya Adhabu ya Viboko

MWANAFUNZI
Viboko vimekuwa vikitutengenezea Mazingira ya hofu, ukiona Mwalimu fulani anakuja unapata hofu na kukosa umakini, pia kuna matukio ambayo yamekuwa yakisababisha majeraja kwa Wanafunzi

Pia, wapo Wanafunzi wanaoathirika kisaikolojia, Mwalimu akija darasani unashindwa hata kunyoosha mkono kujibu swali hadi Mwalimu akutaje mwenyewe ndio unazungumza au kujibu

Ni vizuri kuwa na mipango ili kuweza kupunguza au kuondoa hizi Adhabu za Viboko kwa Wanafunzi kwa kuwa zimekuwa zikichangia kutuondolea kujiamini

ANNASTAZIA RUGABA, Mkurugenzi wa Uchechemuzi Twaweza
Tumekuwa tukisema mara kwa mara kwenye tafiti zetu kuwa Adhabu ya Viboko si sahihi kwa Watoto Japokuwa masuala ambayo huwa yanagusa Mila, Desturi au Dini huwa yanakuwa na ugumu kuyabadili katika Sheria

Adhabu hii ya Viboko imekuwa ikiharibu sana Saikolojia, nina Ushahidi ambao umetokea kwa Watu ninaowajua ikiwemo hata mimi ilinitokea nikiwa nasoma

Nashauri hivi vitu ambavyo vinahusisha Mila, Desturi na Imani vinatakiwa kuwa na kampeni ya muda mrefu ili kushawishi Serikali na wenye kufanya maamuzi pamoja na kuelimisha Watanzania

Pia, Kampeni kama hizi zinaweza kusaidia, kuboresha na kuchangia mabadiliko ya ufundishaji Elimu Nchini

MWALIMU IGNATIUS JOH
Shule niliyokuwa nasoma hakukuwa na Adhabu ya Viboko, waliweka viwango vya ufaulu, ukifeli au usipofikia kiwango cha ufaulu kulichowekwa unarudishwa nyumbani, hiyo ilisaidia Wanafunzi kujituma wenyewe bila kusukumwa

Nilipoanza kazi ya Ualimu miaka minne ya kwanza sikuwahi kuchapa fimbo lakini mazingira yaliyotokea baada ya hapo yalinilazimisha kuanza kuwachapa japokuwa nilikuwa naumiaNina mifano mingi ya Watoto ambao hawawezi kukaa kwenye nafasi nzuri bila kuchapwa

KWIDO SANGA
Unapotoa adhabu kwa Mtoto unatakiwa kuangalia unatoa ukiwa katika mazingira gani ya kiakili kichwani, mfano kama una hasira au haupo vizuri kichwani kwepa kutoa adhabu kubwa kwa Mtoto

Pamoja na Kanuni nyingi zilizopo kuhusu Adhabu ya Viboko lakini lazima Walimu waelekezwe njia sahihi na waandaliwe, haya mambo ya kusema anayetakiwa kutoa Adhabu ni Mwalimu Mkuu au aelekeze kwa maandishi yote hayo yamekuwa hayazingatiwi

FILIPO LUBUA
Kuchapa Mtoto au kutoa adhabu Mwalimu anatakiwa kuzingatia mazingira na aina ya Adhabu zinazotolewa maeneo husika

Pia, ndani ya Jamii au Shule kuna tatizo la yule aliyejuu hawezi kuulizwa au kukosolewa, hiyo inafanya wale walio juu waamini wao wanaweza kufanya chochote na hakuna wa kumuuliza, hivyo ndivyo ilivyo kwa Walimu mbele ya Watoto

Sasa hivi imekuwa Walimu hawatoi Adhabu ya Viboko kama Adhabu au kuwawajibisha Wanafuzni bali wanafanya hivyo kutoa hasira zao

Kuna Mwalimu wangu mmoja nikiwa mtu mzima amewahi kuniuliza kuwa kama nisingechapwa ningefanikiwa kama nilivyofanikiwa leo? Nikamjibu kuwa kuna wanafunzi wangapi aliokuwa anawachapa na leo hii Maisha yao sio mazuri?Hivyo, Adhabu ya Viboko si nzuri na inatakiwa

IRENE FUGARA
Mwalimu na Mwanafunzi pekee hawawezi kumaliza adhabu ya Viboko, inahitaji mfumo mzima ubadilike. Walimu wengi ukiwauliza wako tayari kuacha adhabu lakini bado swali linakuwa njia gani mbadala itatumika kubadili tabia za WanafunziAdhabu ya Viboko haitoa mafundisho kwa Watoto, inakuacha na maumivu
 
Watoto wafundishwe ukakamavu mashuleni na swala la Lishe bora mashuleni Serikali iwajibike pia Michezo irudi kama zamani.

Mboko kuchimba mashimo kama kawa! Wale Walimu wavaa KOMBATI mashuleni warudishwe.

Fedha za mavietii zimwagwe Wizara ya Elimu kuongeza bajeti ya Elimu. Walimu waheshimike kama zama za Mwalimu.

Kibaha Elimu SUPPLY irudi kama zama za Mchonga.
 
Ni kweli ila kwa Kiasi, na wanaosimamia hizi adhabu wathibitike kutokuwa na matatizo ya kisaikolojia
Walimu wengi siku hizi Wana changamoto za kiakili hivyo wao wenyewe huitaji usimamizi wa karibu
 
Kuna changamoto katika uekelezaji wa utoaji wa adhabu mashuleni, kwa mfano sheria inamtaka kabla mwalimu hajatoa adhabu, lazima apate kibali kutoka kwa mkuu wa shule, lakini pia na idadi ya viboko anayotakiwa kuchapwa mwanafunzi ni viboko vinne.

Lakini kuna baadhi ya walimu wachache hawafuati taratibu hizo, naiomba Serikali itoe tamko rasmi kwa walimu wote nchini juu ya wao kufuata sheria za utoaji adhabu kwa wanafunzi
 
Back
Top Bottom