Je, ndege ya Air Force One, gari la the beast na ndege 6 za Boeing zinamlindaje Rais wa Marekani?

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
75,567
158,296

Je, ndege ya Air Force One, gari la the beast na ndege 6 za Boeing zinamlindaje Rais wa Marekani?​

.


Viongozi wakuu duniani watasafiri hadi India kwa Mkutano wa nchi 20 zilizoendelea kiviwanda G20, ambapo ulinzi umeimarishwa.

Rais wa Marekani Joe Biden atawasili nchini India kushiriki katika Mkutano wa G20 akiandamana na msafara mkubwa wa maafisa wake wa usalama.

Unaposkia kuhusu ulinzi unaotolewa kwao inaweza kuwa kama filamu, lakini ni ukweli.
Idara ya huduma ya Ujasusi nchini Marekani CIA ina jukumu kubwa katika kumlinda Rais.

Iliundwa mnamo 1865, lakini mnamo 1901, ilikabidhiwa jukumu la kumlinda Rais wa Marekani
Zaidi ya maafisa wa ujasusi elfu saba wanafanya kazi katika idara hiyo wakiwemo wanawake.
Mafunzo kabla ya kujiunga na idara hiyo yanachukuliwa kuwa moja ya mafunzo magumu zaidi duniani.

Maandalizi ya miezi mitatu kabla​

.

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Ijapokuwa rais wa Marekani anachukuliwa kama mtu mwenye nguvu zaidi duniani, hawezi kuchukua uamuzi wa usalama wake peke yake. Hiyo ni kazi ya idara ya Ujasusi nchini humo CIA.

Hata iwapo rais huyo atataka kubaki peke yake bila ulinzi, maafisa wa idara hiyo hawawezi kutii amri yake.

Ikiwa rais wa Marekani ataamua kuitembelea nchi yoyote, idara ya Ujasusi huanza kazi yake karibu miezi mitatu kabla ya tarehe iliyopangwa.

Rais anatembea katika aina ya ngao ya usalama ambayo ina usalama wa Matabaka tofauti . Sio tu yenye nguvu bali pia ni ghali mno.

Marekani imeshuhudia marais wake wanne wakiuawa ikiwemo Abraham Lincoln aliyeuliwa mwaka 1865, James Garfield mwaka 1881, William McKinley na John F. Kennedy mwaka wa 1901 .
Kwa hivyo kwa kawaida Marekani inazingatia sana usalama wa rais wake.

Je, Usalama huu unajumuisha nini?

Mfumo wa usalama katika ngazi tatu​

.

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Maelezo ya picha,
Gari la rais wa Marekani aina ya The Beast
Rais ana ngazi tatu za usalama. Ndani ni mawakala wa Idara ya Ulinzi wa Rais, kisha mawakala wa Idara ya Ujasusi , na kisha polisi.

Na rais huyo anapoelekea Delhi nchini India, kutakuwa na safu ya usalama ya maafisa wa usalama wa polisi ya Delhi, ambayo itakuwa safu ya usalama ya nje ya nne.

Wafanyikazi wa Idara ya Ujasusi CIA na ikulu huwasili mapema karibu miezi miwili au mitatu na kuanza kukutana na mashirika ya ulinzi katika nchi ambapo rais huyo anapanga kusafiri.

Idara hiyo huamua mahali ambapo rais ataishi. Eneo hilo linachunguzwa kwa kina. Ukaguzi wa historia yake pamoja na historia ya wafanyakazi wa hoteli pia unafanyika.

Itifaki ya Usalama​

.

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Kuna mipangilio mingine mingi. Kwa mfano, anga ya nchi hiyo inahitajika kwenye viwanja kwenye viwanja vya ndege. Kwa sababu sio tu ndege ya rais 'Air Force One' inawasili, lakini ndege sita za Boeing C17 zinapaa nayo. Pia kuna helikopta inayoruka kati ya ndege hizo.

Msafara wa rais pia unajumuisha magari aina ya limousine, vifaa vya mawasiliano, mawakala wengine wengi na wafanyikazi wa ikulu ya Marekani.

Idara ya CIA na mashirika ya usalama wa ndani huamua njia ya msafara wa rais, kwa kuzingatia wapi na jinsi gani ya kumtorosha rais iwapo kuna dharura yoyote.

Je, lipi litakuwa eneo salama iwapo kuna shambulio?

Idara hiyo ya ujasusi ina jukumu la kuhakikisha kuna hospitali ya kuangazia maswala ya dharura ambayo haitakuwa umbali wa Zaidi ya dakika 10 kutoka mahala anapolala rais.
.

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Afisa wa ujasusi huwekwa katika kila hospitali iliyo karibu ili kuwasiliana na madaktari iwapo kuna dharura.


Madaktari pia hutayarisha damu ilio sawia na aina ya kikundi cha damu ya rais ili iwapo itahitajika inaweza kupatikana kwa urahisi.
Maafisa hukagua kila kituo kwenye njia itakayotumiwa na msafara wa rais kadri tarehe ya kuwasili kwake inapokaribia.
Magari yalioeegeshwa barabarani karibu na hoteli atakapokaa rais yanaondolewa
Mazoezi pia hufanywa juu ya nini cha kufanya katika hali tofauti za hatari.

Je, mpangilio ukoje katika hoteli?​

.

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Katika hoteli, sio tu ghorofa nzima hutengewa rais kuishi lakini pia ghorofa ya chini na ya juu huachwa wazi kwa sababu za kiusalama.

Chumba kizima hukaguliwa kwa kina ili kuhakikisha kuwa hakuna kamera iliyofichwa au vifaa vya kurekodia.

Televisheni na simu za hoteli huondolewa. Ngao za kuzuia risasi pia zinawekwa kwenye madirisha ya chumba cha rais.
Wapishi wa rais huandamana naye na ndiyo wanaomtayarishia chakula chake.

Katika mapishi, maafisa wa Idaya ya Ujasusi pia huzingatia kwa makini ili kuhakikisha hakuna hatari kwa chakula cha rais.
.


Idara ya Ujasusi ya CIA ina jukumu lingine kubwa.
Idara hiyo pia ina jukumu la kuwalinda wanajeshi wanaoandamana na rais kila wakati. Rais ana mkoba wa kurusha kombora la nyuklia la Marekani.

Rais anasafiri kwa gari lake la aina ya limousine.
Gari hili limepewa jina maarufu 'The Beast'. Gari hili limeundwa na kuwekwa vifaa vya kila aina .
Sio tu la kivita na kuzuia risasi, pia lina vifaa vya kinga zaidi na teknolojia.

Kama vile skrini za moshi, mabomu ya machozi, teknolojia ya kuona usiku, ulinzi dhidi ya mashambulizi ya kemikali na virusha guruneti.

Madereva wamefunzwa hivi kwamba wanaweza kugeuza gari kuelekea upande mwingine, yaani digrii 180 wakati wa shambulio.

Wakati Obama aliposafiri India​

.

CHANZO CHA PICHA,EPA
Maelezo ya picha,
Mwaka 2015, aliyekuwa rais wa Marekani Barrack Obama alikuwa mgeni wa heshima katika hafla ya Siku ya Jamhuri ya India.

Mnamo 2015, Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama aliitembelea India kama mgeni wa heshima wakati wa kusherekea siku ya Jamhuri
Kulingana na mila za Wahindi, alitakiwa kuandamana na rais wa India kwenye ukumbi huo, lakini alifika mahali hapo kwa gari lake la kumlinda 'The Beast'.
Lakini itifaki ya usalama pia ilikiukwa siku hiyo.

Kulingana na miongozo ya Idara ya CIA , rais hawezi kukaa katika eneo la wazi kwa zaidi ya dakika 45. Rais Obama alikaa mahali hapa kwa saa mbili.

Taarifa hii yote sio siri. Baadhi ya watu ambao wamehudumu katika Idara hiyo wameandika hata vitabu.

Mfano ni Joseph Petro, ameandika kitabu alikuwa wakala maalum katika Idara ya Ujasusi kwa miaka 23.

Kando na yeye, Ronald Kessler aliwahoji zaidi ya maafisa 100 wa Secret Service na kuandika kitabu kiitwacho 'In the President's Secret Service'.
Kila mara Rais wa Marekani anapotembelea mahali fulani, maelfu ya watu huhudhuria.
Mwandishi wa BBC wa Ikulu ya White House aliwahi kuandika kuwa dunia inasimama wakati rais wa Marekani anaposafiri.

Chanzo: BBC SWAHILI
 
Hao walinzi wanmlinda kwasababu siku yake ya kufa haijafika lakn cku ikifika hakuna ulinzi wowote hapo atakabidhi tu faili kwa Malaika mtoa roho
Hii ni zaidi pumba uwezo wa chini sana kufikiria😳😳

Kwa hiyo ulitaka rais wa marekani mwenye maadui kila kona atembelee ist, mgambo wawili wa kumlinda, alale guest house ya uswahilini, ale kwa mamantilie kisa tu kifo hakiepukiki😳😳

Kwa akili hizo unaweza simama relini ukasema kifo hakiepukiki!!
 
Hii ni zaidi pumba uwezo wa chini sana kufikiria😳😳

Kwa hiyo ulitaka rais wa marekani mwenye maadui kila kona atembelee ist, mgambo wawili wa kumlinda, alale guest house ya uswahilini, ale kwa mamantilie kisa tu kifo hakiepukiki😳😳

Kwa akili hizo unaweza simama relini ukasema kifo hakiepukiki!!
Ww ni mbumbu Mzungu wa reli ungekuwa na chembe ya Iman ungejua nimemaanisha nn?
 
Ilikuwaje George Bush akarushiwa viatu ukumbini kwenye mkutano na waandishi wa habari?
Hao wana usalama hawakunusa hilo?
Kwanini baada ya tukio lile Bush aliendelea kukaa mkutanoni?

Event. During a 14 December 2008 press conference at the prime minister's palace in Baghdad, Iraq, Iraqi journalist Muntadhar al-Zaidi threw both of his shoes at United States president George W. Bush.


View: https://www.youtube.com/watch?v=tU0RaRvJ0PQ
 
Back
Top Bottom