Je, Mwezi unazunguka dunia kwa mwendo usiobadilika 'constant speed'? Inakuwaje tunakuwa na muda tofauti wa kupatwa kwa mwezi au jua?

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,489
3,643
Wakuu habarini muda huu!

Najua JamiiForums kuna watu wenye maarifa mengi ya kila aina, hivyo naombeni msaada wenu kunielewesha jambo hili

Leo usiku hadi kuelekea kukucha kwa kesho kunatarajiwa kuwa na historia mpya kwenye hii dunia kuwa tukio la kupatwa kwa mwezi la leo litakuwa la muda mrefu zaidi kuliko yote yaliyowahi kutokea, takribani saa 6 na dakika 14

Sasa hapa nashindwa kuelewa, inakuaje muda wa kupatwa kwa mwezi au kupatwa kwa jua kuna kuwa na muda tofauti?

Je, spidi ya mwezi kuzunguka dunia inabadilika kwamba kuna saa mwezi unaongeza spid na kuna saa unapunguza spidi?

Na je, dunia kujizungusha katika muhimuli wake nayo kuna saa inapunguza na kuongeza spidi?

Naomba kuwakilisha wakuu!
 
Tazama hii video huenda ikakusaidia!
 
Attachments

  • Total Lunar Eclipse & Mars at Opposition 2018.mp4
    10.9 MB · Views: 28
Jua huwa mara kusini mwa Ikweta au kaskazini na wakati mwingine kwenye Ikweta je huu mwezi una tabia gani? Mf. Siku ya Id kwa waislamu ni siku moja dunia nzima naomba elimu kidogo kwani nilipata zero (Astronomy)
 
Tazama hii video huenda ikakusaidia!
Mkuu asante sana, ila video hii inaelezea kuhusu umbali kati ya Dunia na Sayari ya Mars zaidi, kwamba umbali wa orbit zao unatofautiana.

Hivyo, inawezekana kuwa orbit ya mwezi kuzunguka dunia sio perfect duara? Naona bado swali sijapata jibu
 
Watanzania wengi akili zetu ziko kwenye stress za maisha.. Ndo mana unaona michango kwenye hii Mada ni Haba. Au watakwambia na wao wanasubiri Majibu.

Muda Wa kupatwa kwa mwezi na kupatwa kwa Jua lazima uwe tofauti... Hata "impacts" za kupatwa kwa. Mwezi na Jua huwa ni tofauti.. Mfano kupatwa kwa mwezi Kuna impacts chache sana lakini kupatwa kwa Jua Kuna impacts nyingi ikiwemo kurefuka kwa usiku na mchana na impacts zingine.

Narudi muda mchache ujao Kuja kuingalia spid ya mwezi kama Kuna muda inaongezeka. Na muda inapungua.
 
Ipo hivi, dunia inalizunguka jua na mwezi unaizunguka dunia. Kwahiyo wakati dunia ikiwa katikati ya jua na mwezi ndio kipatwa kwa mwezi.

Sasa suala la muda kuwa mrefu ni kutokana na kuwa mwezi nao unakua hausimami nao unaendelea kuzunguka.

Tofauti na kupatwa kwa jua ambapo kutokana na jua kuwa stationary mwezi unapita tu fasta kati ya dunia na jua.

Pili kivuli cha dunia kinakua kikubwa sana kulizuia jua kutokana na mwezi kuwa mdogo kuliko dunia hivyo mwezi huchukua muda mrefu zaidi kuzunguka kivuli cha dunia

Usiponielewa basi tena
 
Last edited:
Wakuu habarini muda huu!

Najua JamiiForums kuna watu wenye maarifa mengi ya kila aina, hivyo naombeni msaada wenu kunielewesha jambo hili

Leo usiku hadi kuelekea kukucha kwa kesho kunatarajiwa kuwa na historia mpya kwenye hii dunia kuwa tukio la kupatwa kwa mwezi la leo litakuwa la muda mrefu zaidi kuliko yote yaliyowahi kutokea, takribani saa 6 na dakika 14

Sasa hapa nashindwa kuelewa, inakuaje muda wa kupatwa kwa mwezi au kupatwa kwa jua kuna kuwa na muda tofauti?

Je, spidi ya mwezi kuzunguka dunia inabadilika kwamba kuna saa mwezi unaongeza spid na kuna saa unapunguza spidi?

Na je, dunia kujizungusha katika muhimuli wake nayo kuna saa inapunguza na kuongeza spidi?

Naomba kuwakilisha wakuu!
Mwezi unazunguka duani. Na dunia inazunguka jua. Lakini angalia ''usidang'anyike'' na neno kuzunguka. Nasema ''usidanganyike'' kwa sababu mizunguko inayoongelewa iko complex. Hebu angalia hii video ya dunia inavyozunguka jua ili upate mwanga.
 
Jua ni kubwa sana mwezi hadi uzunguke na kuhamisha au kupata nafasi ya kuichabo dunia lazima utumie muda mrefu, jua ni kubwa na mwezi kuliziba jua ni muda mdogo tu jua linaichabo dunia, ukitaka kuelewa zaidi chukua goroli na white ya pool table tochi unaweza elewa vizuri sana
 
Samahani. Nimeona leo swali hili la siku nyingi miaka miwili iliyopita. Tofauti ambayo anauliza ni ile inayoweza kutambuliwa na mtu wakati anaangalia matukio hayo ya kupatwa kwa Mwezi au Jua.

Muda wa kupatwa kwa Mwezi kamilifu ni mkubwa sana kiasi saa nzima wakati muda ambao Jua linapatwa kamilifu ni kiasi dakika chache tu.

Tofauti hiyo inatokana na tofauti jinsi kupatwa kunavyotokea. Wakati wa kupatwa kwa Mwezi kikamilifu, kivuli kikubwa sana cha Dunia kinaweza kumeza Mwezi mzima mara tatu kwa hiyo mwendo wa Mwezi katika mzingo (orbit) wake hutumia zaidi ya saa kupita ndani ya kivuli cha Dunia.

Kwa upande mwingine, sababu ya kupatwa kwa Jua kikamilifu ni tofauti kabisa. Duara za Mwezi na Jua tunavyoziona kutoka hapa ardhini ni karibu sawa kabisa na zimelingana kabisa kwa bahati tu. Wakati wa kupatwa kamilifu kwa Jua, sahani ya Mwezi insogea juu ya Jua na kuweza kuifunika kabisa na kusababisha gizo totoro duniani. Haichukuwi hata dakika tatu na sahani ya Mwezi inakuwa imesogea mbele na kufichua Jua baada ya dakika tatu tu.

Kwa hiyo tofauti kati ya matukio haya mawili ni tofauti kati ya saa nzima na dakika tatu. Hii ni tofauti kubwa, ndiyo maana huwa tunashtuka tunaposikia tofauti kiasi hicho. Lakini baada ya kuelewa jinsi matukio hayo yanavyotokea utaweza kuona kwamba hakuna cha ajabu kuona tufauti kubwa kati ya kupatwa Mwezi na kupatwa Jua.

Katika matukio yote mawili muda wa matukio unatokana tu na mwendo wa Mwezi kuizunguka Dunia. Hazina husiano na mwendo wa Dunia kuizunguka Jua. Kweli ukiangalia kwa undani kuna tofauti katika kasi za mwendo lakini tofauti hiyo ni ndogo mno (sehemu ndogo sana ya sekunde) ambayo wala hatuwezi kuhisi.

eclipse-types.png

Mpito wa Mwezi ndani ya kivuli cha Dunia.png

Swali hili liliulizwa zamani miaka miwili iliyopita lakni nimeliona leo wakati ninaposti maelezo ya kupatwa kwa Mwezi. - Mwezi kupatwa mfifio kesho usiku Ijumaa Juni 05, 2020 - penumbral lunar eclipse

Swali liliulizwa hapa:
Je, Mwezi unazunguka dunia kwa mwendo usiobadilika 'constant speed'? Inakuwaje tunakuwa na muda tofauti wa kupatwa kwa mwezi au jua?

Jibu langu:

Tofauti ambayo anauliza ni ile inayoweza kutambuliwa na mtu wakati anaangalia matukio hayo ya kupatwa kwa Mwezi au Jua.

Muda wa kupatwa kwa Mwezi kamilifu ni mkubwa sana kiasi saa nzima wakati muda ambao Jua linapatwa kamilifu ni kiasi dakika chache tu.

Tofauti hiyo inatokana na tofauti jinsi kupatwa kunavyotokea. Wakati wa kupatwa kwa Mwezi kikamilifu, kivuli kikubwa sana cha Dunia kinaweza kumeza Mwezi mzima mara tatu kwa hiyo mwendo wa Mwezi katika mzingo (orbit) wake hutumia zaidi ya saa kupita ndani ya kivuli cha Dunia.

Kwa upande mwingine, sababu ya kupatwa kwa Jua kikamilifu ni tofauti kabisa. Duara za Mwezi na Jua tunavyoziona kutoka hapa ardhini ni karibu sawa kabisa na zimelingana kabisa kwa bahati tu. Wakati wa kupatwa kamilifu kwa Jua, sahani ya Mwezi insogea juu ya Jua na kuweza kuifunika kabisa na kusababisha gizo totoro duniani. Haichukuwi hata dakika tatu na sahani ya Mwezi inakuwa imesogea mbele na kufichua Jua baada ya dakika tatu tu.

Kwa hiyo tofauti kati ya matukio haya mawili ni tofauti kati ya saa nzima na dakika tatu. Hii ni tofauti kubwa, ndiyo maana huwa tunashtuka tunaposikia tofauti kiasi hicho. Lakini baada ya kuelewa jinsi matukio hayo yanavyotokea utaweza kuona kwamba hakuna cha ajabu kuona tufauti kubwa kati ya kupatwa Mwezi na kupatwa Jua.

Katika matukio yote mawili muda wa matukio unatokana tu na mwendo wa Mwezi kuizunguka Dunia. Hazina husiano na mwendo wa Dunia kuizunguka Jua. Kweli ukiangalia kwa undani kuna tofauti katika kasi za mwendo lakini tofauti hiyo ni ndogo mno (sehemu ndogo sana ya sekunde) ambayo wala hatuwezi kuhisi.

eclipse-types.png

Mpito wa Mwezi ndani ya kivuli cha Dunia.png

Ni simple. Dunia inazunguka jua na mwezi nao unazunguka dunia. Kutokea kwa kupatwa kwa jua inadepend na position ya jua, dunia na mwezi ambayo inakuwa afected na mizunguko ambayo ipo tofaut.
 
Wakuu habarini muda huu!

Najua JamiiForums kuna watu wenye maarifa mengi ya kila aina, hivyo naombeni msaada wenu kunielewesha jambo hili

Leo usiku hadi kuelekea kukucha kwa kesho kunatarajiwa kuwa na historia mpya kwenye hii dunia kuwa tukio la kupatwa kwa mwezi la leo litakuwa la muda mrefu zaidi kuliko yote yaliyowahi kutokea, takribani saa 6 na dakika 14

Sasa hapa nashindwa kuelewa, inakuaje muda wa kupatwa kwa mwezi au kupatwa kwa jua kuna kuwa na muda tofauti?

Je, spidi ya mwezi kuzunguka dunia inabadilika kwamba kuna saa mwezi unaongeza spid na kuna saa unapunguza spidi?

Na je, dunia kujizungusha katika muhimuli wake nayo kuna saa inapunguza na kuongeza spidi?

Naomba kuwakilisha wakuu!

Haya matukio ni periodical, as long as Dunia na Mwezi hazihami kwenye njia za mizunguko yake, yaani ORBITS. Kwa hiyo huwa yanajirudia ila baada ya muda mrefu sana kiasi kwamba lifespan ya mwanadamu tangu kuzaliwa kwake hadi kufa, haiwezekani akayashuhudia matukio hayo
Ni kwamba njia hizi zote mbili zinazotumiwa na Mwezi kuzunguka dunia, na ile ya Dunia kulizunguka jua, yaani ORBITS, haziko mduara (orbits ---not circular) ila ziko kama mduara uliominywa ukawa na umbo kama la yai (elliptical orbits). Zaidi ni kuwa dunia nayo pia ina umbo ambalo si la mduara ulio sawia (not perfect sphere) na imekaa tenge kwenye mhimili wake ambapo huwa inajiviringisha yenyewe na kusababisha kutokea kwa na majira ya usiku na mchana. Hizi ndiyo sababu zinazosababisha mwanadamu aone KAMA matukio ya kupatwa kwa mwezi na jua huwa hayajirudii kwa sababu MAXIMUM LIFE SPAN YA MWANADAMU NI MIAKA 150, na matukio haya huwa yanajirudia katika muda ambao ni zaidi ya miaka hiyo, na pengine labda baada ya melfu ya miaka
 
Hali ya kupatwa hutokea kwa wastani mara nne kwa mwaka na siyo maelfu ya miaka. Mwezi unapatwa mara mbili na Jua linapatwa mara mbili kwa wastani kila mwaka. Hayo ya maelfu ya miaka ni mabadiliko katika muelekeo wa mhimili na kiasi cha mwinamo wa mhimili ambayo inahusiana na mabadiliko ya tabia nchi. hadi kuwa barafu dunia nzima
 
Mkuu hakuna kitu kama iko. Nataka nikupe mfano simple.

Bus la Abood no 1 linatoka mwanza saa 12 asubuh na kufika dar saa 6 usiku. Ila kuna aboid no 2 inatoka dar to dodoma. Inatoka saa 12 na kufika dar saa 8 mchana alafu inarudi hapo hapo. Tukiassume hizi bus zinafanya root on constant timetable and constant speed. maana yake, kuna point huwa zinakutana. Ila iyo point haiwezi kuwa the same point kila siku
 
Hali ya kupatwa hutokea kwa wastani mara nne kwa mwaka na siyo maelfu ya miaka. Mwezi unapatwa mara mbili na Jua linapatwa mara mbili kwa wastani kila mwaka. Hayo ya maelfu ya miaka ni mabadiliko katika muelekeo wa mhimili na kiasi cha mwinamo wa mhimili ambayo inahusiana na mabadiliko ya tabia nchi. hadi kuwa barafu dunia nzima
Hapana hujamwelewa alichokuwa anaongelea. Yeye anachosema kwa mfano ni hivi, kwa nini huwa haijirudii tuseme jua likipatwa tarehe 05/02/2000 saa 7 kamili mchana, ije ijirudie tena lipatwe kwenye tarehe hiyo hiyo na muda huo huo kwa mwaka mwingine tuseme 2040, yaani miaka 20 baadaye? Na baada ya hapo tena, lipatwe tena miaka 20 baadaye, muda huo huo na tarehe hiyo hiyo, yaani mwaka 2060, na iendelee hivyo hivyo kwa miaka inayofuata, 2080, 2100, 20120, n.k.? Mimi ndivyo nilivyomwelewa kwa kifupi
 
Back
Top Bottom