Je, mwanaume na mwanamke nani anayemuhitaji mwenzake zaidi?

mussa victor

Senior Member
Jul 12, 2015
116
162
(Writer darasa la mapenzi)

Karibuni mchangie

Ni suali moja ambalo halina majawabu ya moja kwa moja, lazima tuangalie vigezo zaidi kuliko kwa mtazamo wa kawaida. kama wewe unayo majibu usisite kutuandikia.

Mwanaume anamuhitaji mwanamke zaidi kama msaidizi wake kuliko mwanamke anavyomhitaji mwanaume na sema hivyo sio kwa kuegemea swala la ngono bali kwenye maswala mengine mengi ya kimaisha.


Inasemekana kwamba wanawake ambao hawajaolewa wanaishi zaidi ukilinganisha na wale walio ndani ya ndoa na Wanaume waliondani ya ndoa huishi maisha marefu zaidi kuliko wale walio nje ya ndoa, umewahi kujiuliza kwanini wataalamu wanadai hivo?

Wengi wetu tunazaliwa kisha kukua na kukuta baba na mama pamoja, bibi na babu pamoja, shangazi na mjomba pamoja, baba mdogo/mkubwa na mama mdogo/mkubwa pamoja na kudhani hivyo ndivyo sote tunavyotakiwa kuwa mara tunapokuwa watu wazima, na Kadhalika.

Tunapoanza kujiingiza katika mahusiano ya kimapenzi na baadae maisha ya ndoa (milele pamoja) tunakuja kuhisi kuwa hatuwezi kuishi bila wenza wetu sio kwa vile wanatulisha na kutuvisha bali tunawapenda na pengine ni kwa vile umri umeenda na unahofia kuwa "nani atanitaka na mikunjo hii".

Mwanaume ni mwindaji na uwindaji huo sio wa kupata kitoweo tu (pesa) bali kukupata wewe mwanamke pia, inasemekana kuwa wanaume wengi wanaamua kuwa “single” au wagumu ku-commit karne hii kwa vile wanawake hawawindiki tena.

Kwamba wanawake wamekuwa rahisi kupatikana (kukubali kirahisi) na hivyo wanaume hawahisi kama unawafaa kama wapenzi wao wa kudumu kwa vile hawakukuwinda bali ulijitega mwenyewe (kutokana na U-feminist a.k.a Ubeijing wa wanawake wengi wakidhani ni Usawa).

Hali hiyo inasababisha wanawake wengi kukata tamaa na wanaume ambao hawa-commit kwenye mahusiano ya kudumu.
 
Vyovyote unavyoweza kufiri lakini Mungu aliumba wanaume na wanawake kuishi pamoja. Matendo ya binadamu yanaleta athari sana katika uwiano huu mfano biashara ya utumwa iliathiri sana uwiano wa wanaume na wanawake, idadi ya wanawake ilikua kubwa kuliko ya wanawaume. Baada ya vita kuu ya I na II pia idadi ya wanaume ilishuka sana na wanawake ilibidi wafundishwe kazi ambazo zamani zilikuwa ni za wanaume; kazi kama udereva, ujenzi, kazi za viwandani. Katika simulizi pia wanadai wanawake walianza tabia ua usagaji kutokana na waume zao kuwaacha na kwenda vitani, walianza kujifariji wenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…