Je, Muujiza gani ulishawahi kuupata?

RGforever

JF-Expert Member
Apr 3, 2011
6,878
5,431
Katika Maisha ya Kiimani Kusema Ukweli naona Watu wengi sana Katika Luninga Wakitoa Kitu kiitwacho Ushuhuda wakati wa Ibada za Maombezi..

Sometimes naona Zingine ni Changa La Macho na Watu wanaibiwa Live Live ila Kwa Mtu uliye na Akili za kawaida Unaona Kabisa Hapa hakuna Miujiza Ila ni kama Mazingaombwe tu....

Sasa basi Je Kuna Mtu Humu aliyewahi kupata Muujiza Na Akaona Katika Hali ya Kawaida Ameshazunguka Vya Kutosha Ikashindikana Ila Baada ya Kupata Maombezi Ikawezekana..

Maana Zilianza Zile za Mimba Za wanawake Wanazaa watoto mara Unashangaa Mtoto baada Ya Mwaka Kashaanza kugeuka Mara Anakuwa Nyoka Mara Anakufa Ghafla n.k n.k

Je Ushapata Muujiza ambao mpaka Leo Unadumu nao....?
 
Mshahara mdogo wa ualimu ila naishi fresh tu kuliko wanaojilipa mishahara zaidi ya 7. Kwel mtu hatoishi kwa mkate tu bali kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu
 
Pale nilipoitwa kwenye usaili wa nafasi moja nikiwa pekee yangu nikafanya huo usaili kwakujiamini sana kwakuwa vyote nilivyoulizwa vilikuwa field yangu lkn muujiza ni kuwa kazi alipatiwa mtu mwingine ambae hata kwenye usaili hakuwepo. Hii tz hii
 
Aise kama tunafanana kwenye muujiza wako na mm kiongozi kweli hii tz hii noma sana mdau duuuu mpaka nikashindwa kushangaa aise
 
kupima HIV/AIDS na majibu kuwa -VE, huku nkiwa "nimeuza mechi karbia 10*10
 
Nilikuwa nachemsha maji ya kunywa, ile nayamimina kwenye kidumu yakanimwagikia mkononi lakini kwa Muujiza wa Mwenyezi Mungu badala ya yale maji kuniunguza na kunibabua ngozi, niliyasikia yakipoa ghafla na wala sikupata jeraha lolote. Ni miaka zaidi ya kumi imepita bt huwa nalikumbuka sana tukio hilo la kutounguzwa na maji ya moto ambayo yalikuwa yamechemka mpaka yanaruka ruka...
 
Muujiza wangu mimi nilikuwa nasoma na chemli koroboi tangu form one mpaka form six na huko kote nilikuwa naburuza vibaya mno. Nilikuwa nikiwaambia washkaji hawaamini mpaka na kesho maana si kwa balaa lile. Nlikuwa natisha
 
Pale nilipoitwa kwenye usaili wa nafasi moja nikiwa pekee yangu nikafanya huo usaili kwakujiamini sana kwakuwa vyote nilivyoulizwa vilikuwa field yangu lkn muujiza ni kuwa kazi alipatiwa mtu mwingine ambae hata kwenye usaili hakuwepo. Hii tz hii
 
Nilipokuwa katika uhusiano na binti flani kwa miaka miwili na tukabahatika kupata mtoto ndio nikagundua mzazi mwenzangu ni HIV+ na mimi ni mzima wa afya na mwanangu. Hakika ni Muujiza mkubwa sitasahau.
 
Pale nilipoitwa kwenye usaili wa nafasi moja nikiwa pekee yangu nikafanya huo usaili kwakujiamini sana kwakuwa vyote nilivyoulizwa vilikuwa field yangu lkn muujiza ni kuwa kazi alipatiwa mtu mwingine ambae hata kwenye usaili hakuwepo. Hii tz hii
Huo zaidi ya muujiza,,,muujiza ni kwamba uligraduate peke yako chuo cha babaako!!!
Has haa haa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…