Je, mita za LUKU zinawasilianaje na server za TANESCO?

Paul S.S

JF-Expert Member
Aug 27, 2009
6,407
3,258
Wakuu Sote tunajua jinsi ya kununua umeme wa luku.

Swali hili liliwahi kujadiliwa sehemu sina hakika ni wapi, lakini je zile vocha unazo nunua na kwenda kuingiza kwenye LUKU inakuwaje?

Je, LUKU zinawasiliana na server za TANESCO kujua kiasi cha units ulizo nunua kama unavyoingiza vocha ya simu?
 
Wakuu Sote tunajua jinsi ya kununua umeme wa luku,
Swali hili liliwahi kujadiliwa sehemu sina hakika ni wapi, lakini je zile vocha unazo nunua na kwenda kuingiza kwenye LUKU inakuwaje?
Je LUKU zinawasiliana na server za TANESCO kujua kiasi cha units ulizo nunua kama unavyoingiza vocha ya simu?

Ni sawa uwe na chombo ambacho kina uwezo wa kuonyesha units (lita, kgs etc ) ulizoongeza sasa wewe ukinunua lita moja na kulikuwa na Nusu basi kitaonyesha kwa sasa una lita moja na nusu, hivyo ukitoa shilingi elfu kumi watakupa units za thamani hiyo na utakapoweka zile namba zitaonyesha units za thamani hiyo. Yaani ni simple logic same applies to simu.
my 2 cents
 
kaka sababu unaulizwa namba ya mita kila ukinunua vocha za luku mi naweza kusema luku haiwasiliani na tanesco.

itakua kuna mashine inagenerate key kutokana na mita yako, halafu luku ndo inatambua.

tuchukulie mfano wa software unakuta kampuni inauZA software na wanagenerate key kutokana na email basi ukieka email na key zinazoendana unaheasabika kama umenunua software ile,

huu ni muono wangu
 
mawasiliano yanapita kwenye nyaya hizo hizo za umeme.

Niliambiwa Tanesco wana uwezo wa kuwasiliana kupitia nyaya zao za umeme na ni kwa kasi na usikivu uliotulia.
 
mimi pia wazo langu kama la chief-mkwawa nahisi zile tarakimu uwa zinakuwa generated kucorrespond na namba ya mita. ndio maana ukichukua uo umeme uweke kwenye mita ingine inakataa. ndio maana mita zote zinatolewa na tanesco tu na huruhusiwi kujinunulia yako nje ya tanesco.
 
Last edited by a moderator:
kaka sababu unaulizwa namba ya mita kila ukinunua vocha za luku mi naweza kusema luku haiwasiliani na tanesco.

itakua kuna mashine inagenerate key kutokana na mita yako, halafu luku ndo inatambua.

tuchukulie mfano wa software unakuta kampuni inauZA software na wanagenerate key kutokana na email basi ukieka email na key zinazoendana unaheasabika kama umenunua software ile,

huu ni muono wangu

Mkuu upo sawa kiaina. Ila pia tanesco wanauwezo wa kukukatia umeme au mtaa flani wakiwa ofisini. Inakuaje apo.
 
HATA MIMI NAJIULIZAGA SANA KWANZA, NAMBA YAKO YA LUKU INAOPERATE KTK MITA YAKO TU,MEAN UKINUNUA HUWEZI FEED MITA YYT,TOFAUTI NA VOCHA ZA SIMU KABISA,WANA UWEZO WAKUKUKATIA UMEME WAKIWA MAOFISINI LAZIMA ZITAKUWA NA MATIRIO KAMA <EDF>THAT MEAN ILE METER INA CHIP AMBAYO INA WORK KAMA CELL MOBILE WITH SPECIFIC No.
 
Nyaya za umeme wa tanesco zina uwezo wa kusafirisha mawimbi ya umeme na data. Vipo vifaa maalumu vya ki electronic vimefungwa katika vituo vya tanesco kwa ajili ya ku separate umeme na data ndio maana tanesco sehemu nyingine hutumia nyaya zao kama nyaya za simu na hutumia kupiga simu zao za ndani badala ya TTCL.
 
So zile code unazopewa baada ya kununua units zinaenda kutafsiriwa na luku ni units ngapi, na si kwamba unapo ziingiza zile code zinatumwa Tanesco kuwa verfied
Kwamaana hiyo LUKU haiwasiliani na server za Tanesco
 
Kama ulivyoelezea kaka mkubwa ni kweli kuwa mita za LUKU huwa hazina mawasiliano na ofisi au mtambo wowote toka TANESCO.

Utaratibu wa mita hizi huwa unaitwa "Pay As You Go" ambapo sisi tumetohoa na kuita "Lipa Umeme Kadiri Unavyotumia"...ni utaratibu ambao ni "Pre Paid" na sio "Post Paid" kama zile mita za zamani.

Utaratibu huu hutumia Smartcard au Token Key.

Unapoenda kununua umeme kwenye kituo cha mauzo, kawaida huwa unapaswa utaje nambari ya mita halafu unalipia na baadaye unapewa stakabadhi yenye tarakimu kadhaa utazohitajika kuingiza kwenye mita.

Kwa mfumo wa kielektroniki, mita hizi zimetengenezwa kubadili tarakimu unazoingiza kwenda katika mita na kuzalisha tarakimu umeme "electric unit", na hapo ndipo a reverse count inapoanza kwa kadiri utavyotumia umeme.

NB:
Umuhimu wa nambari ya mita ni kwa vile hatuna kitu kama smartcard (wale wanaonunua gas huko ughaibuni wanazijua hizi au wanaopanda zile BRT's) ambapo ingetumika kwenye topping up, ndio maana tunaitaja kwa wauzaji ili ku-bind umeme tunao nunua na mita zetu.

kaka sababu unaulizwa namba ya mita kila ukinunua vocha za luku mi naweza kusema luku haiwasiliani na tanesco.

itakua kuna mashine inagenerate key kutokana na mita yako, halafu luku ndo inatambua.

tuchukulie mfano wa software unakuta kampuni inauZA software na wanagenerate key kutokana na email basi ukieka email na key zinazoendana unaheasabika kama umenunua software ile,

huu ni muono wangu
 
kaka sababu unaulizwa namba ya mita kila ukinunua vocha za luku mi naweza kusema luku haiwasiliani na tanesco.

itakua kuna mashine inagenerate key kutokana na mita yako, halafu luku ndo inatambua.

tuchukulie mfano wa software unakuta kampuni inauZA software na wanagenerate key kutokana na email basi ukieka email na key zinazoendana unaheasabika kama umenunua software ile,

huu ni muono wangu

Kama haina mawasiliano na Tanesco, vipi kuhusu ukataji wa ile asilimia ya service charge na makato mengine ya kila mwezi, inatambuaje na kuyakata?
 
...
Kwa mfumo wa kielektroniki, mita hizi zimetengenezwa kubadili tarakimu unazoingiza kwenda katika mita na kuzalisha tarakimu umeme "electric unit", na hapo ndipo a reverse count inapoanza kwa kadiri utavyotumia umeme....
Nadhani msingi wa swali upo hapo kwenye bold. Una maana kila kiasi cha units tunazonunua kina corresponding numeral arrangement?
 
kaka sababu unaulizwa namba ya mita kila ukinunua vocha za luku mi naweza kusema luku haiwasiliani na tanesco.

itakua kuna mashine inagenerate key kutokana na mita yako, halafu luku ndo inatambua.

tuchukulie mfano wa software unakuta kampuni inauZA software na wanagenerate key kutokana na email basi ukieka email na key zinazoendana unaheasabika kama umenunua software ile,

huu ni muono wangu

Spot on mkuu Mkwawa, LUKU haiwasiliani na Tanesco isipokuwa mashine za mawakala ndio zinawasiliana na servers za Tanesco kupitia Wi-Fis/Wireless link, nafikili kila mita ya luku uniyo uzwa ina specific specs zinazo saidiana na aligorithms za ku-generate specific key per meter - kwa maoni yangu. Ujanja huu tunautumia sana katika ku-generate Product Key ya OS za William Gates aaah!
 
hii sjawah kuiskia labda kuna mechanism nyengine

Logic :

Kaka hii kitu inawezekana. Kusafirisha ectric signal mbili tofauti katika transmission media moja (wire). Hii inawezakana kwa kutumia concept za filters na combiners. Lakini sharti la kuwezesha hiki kitu kitokee ni lazima signal hizo ziwe na frequency mbili tofauti. As long as sote tunajua kuwa frequency ya umeme wa majumbani kwa Tanzania ni 50 Hz, then hiyo signal nyingine unayotaka isafirisha katika waya mmoja inabidi uisafirishe kwa kutumia frequency nyingine.

Kinachofanyika :

Katika upande wa transmission signal zinakuwa combined/superimposed kwa kutumia combiner na katika reception end zinatengwa kwa kutumia filters(high pass or low pass filter) na further reconstruction processes ya data signal inafuatia.

But hiki kitu sicho kifanyikacho katika issue ya ununuaji wa LUKU. Kama ulivyosema, Katika ununuaji wa luku concept inayotumika ni kutumia meter namba kugenerate code ambayo inapoingizwa kwenye luku huenda kureset counters zilizo katika meter.

Thats it brother...!
 
Kama haina mawasiliano na Tanesco, vipi kuhusu ukataji wa ile asilimia ya service charge na makato mengine ya kila mwezi, inatambuaje na kuyakata?

Mkuu nafikiri jamaa alikuwa anauliza jinzi namba zinavyo kuwa generated, tukija kwenye mawasiliano - kila mita iliyo fungwa kwa wateja, hapo hakuna mawasiliano ya moja kwa moja kati ya mita ya LUKU na Tanesco, mawasiliano yapo kati ya wakala na Tanesco. Unapo fungiwa mita specification zake, wilaya na mji ilipofungwa, tarrif(bracket) na jina la mteja vyote hivyo vinakuwa fed kwenye database, sasa ukienda kwa wakala unapashwa kwenda na namba ya mita yako - wakala ndiye mwenye mawasiliano ya moja kwa moja na Tanesco Servers hapo ndio unapata KWhr yako kutegemea na malipo na kama kuna madeni yanakatwa; baada ya kuridhika na data integrity ndio inatoa namba za kuhingiza kwenye LUKU, kuhusu jinsi namba zinavyo zalishwa nimejaribu kueleza hapo juu, hapa naona mkuu Mkwawa anaweza kuongezea kidogo.
 
Back
Top Bottom