pombe kali
JF-Expert Member
- Jun 28, 2014
- 279
- 554
Salamu wana jukwaa
Nimekuwa nikijiuliza je mamlaka husika zineshindwa kabisa kusitisha matumizi ya namba za simu zisizosajiliwa?
Hizi jumbe za tuma hela kwenye namba hii zimekuwa ni nyingi sana tena hutokea kama umeweka kiasi chochote kwenye simu yako, utaona meseji inasema mfano "mimi ni baba mwenye nyumba yako tuma kodi kwenye namba hii, au mimi ni mwalimu mkuu mwanao ameanguka shuleni,
Huwa najiuliza mamlaka imeshindwa kabisa kudhibiti matumizi ya laini zisizokuwa na usajili halali, zoezi zima la usajili hufanyika kitaalamu sana ambapo kitambulisho cha taifa hutumika na alama za vidole pia ambazo ni utambulisho wa pekee sasa hizi laini za simu zinazotumiwa na hawa jamaa huwa wanazitoa wapi?
kwa nini mitandao husika isiwajibishwe kwa kukubali kuwauzia watu laini bila kufuata sheria kanuni na utaratibu hawa watu wana matusi mabaya pale wanapobaini umewagundua mbinu yao ovu
Mamlaka hapa mnafeli wapi maana wala haihitajiki teknolojia ya juu ni ku disable namba zote zisizo na usajili halali....hata mwanangu anayesoma coding anaweza