Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 24,875
- 35,507
Siku tano zikizopita Rais wa Tsnzania alituma wasaidizi wake ambao ni Prof. Kabudi na William Lukuvi kwenda kusawazisha mambo kule Ngorongoro.
Aliagiza kurejeshwa kwa huduma zote za kibinadamu hususan haki ya kupiga kura, afya na elimu vitu ambavyo vilikuwa vimesitishwa chini ya mtutu wa bunduki na serikali yake.
Sambamba na hilo, serikali ilitoa Amri ya kufuta vijiji 25 na vitongoji 96 ndani ya Ngorongoro. Na hivyo kuhalalisha ukatili wake dhidi ya raia wanaoishi eneo hilo
Nimeona chama cha Wanasheria wakitoa kongole kwa rais kupongeza maamuzi yake ya kusitishwa utekelezaji uliokusudia kumwaga damu za wananchi kwa makusudi.
Nimejiuliza na ninauliza hapa, maagizo na uamuzi wa Rais umetengua Amri halali (haramu) ya serikali ya kufuta hivyo vijiji? Au ni style ya funika kombe ili utekelezaji ufanyike baada ya uchaguzi mwakani?
Nchi inahitaji mwelekeo.
Pia soma>> Serikali yafuta vijiji na vitongoji vyote vya wamasai wa Ngorongoro kupitia Amri ya tangazo la Serikali namba 673