Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,500
- 22,351
Jumatatu ya terehe 3 mwezi huu , meli maarufu ya uokoaji ya Italia iitwayo Dattilo iliokoa wahamiaji wapatao 1000 kwenye pwani ya Catania kwenye mji wa Sicily nchini Italia pembezoni mwa bahari maarufu ya Mediterranean.
Hivyo ilikuwa ni kazi ya uokoaji ya siku mbili kati ya kazi 72 ambazo meli hiyo imefanya na kufanikiwa kuokoa maisha ya waafrika wapatao 10,000 ambao walikuwa wakijaribu kuvuka bahari ya Mediterranean kwa kutumia meli ndogo au mitumbwi ya kujazwa upepo.
Katika shughuli hiyo ya uokoaji waokoaji waligundua miili 28 ya binadamu ambayo ilikuwa imelala sehemu ya chini ya meli hiyo ndogo ambayo ilikuwa imejaza watu wasopungua 1000.
Wahamiaji karibu wote wanahisiwa kutokea kusini mwa jangwa la Sahara hususan katika nchi za Chad, Nigeria, Mali, Niger, Sudan, Somalia, Libya, Ghana, Burkina Faso, Benin, Eritrea na Ethiopia.
Wavushaji wa wahamiaji hao au "smugglers" hulipwa kiasi kikubwa cha fedha hadi kufikia dola 5000 kwa mtu mmoja ili aweze kupata nafasi kwenye meli za kuwavusha na kuna kesi zingine kwamba baadhi ya wahamiaji hao waso na uwezo huwezwa kupelekwa kwa mkopo yaani bure na wakifika kwenye nchi husika ndugu zao hubanwa kuanza kufanya malipo kidogokidogo au kwa awamu.
Wahamiaji hawa ni mbali ya wale wahamiaji wa kutoka Syria au Iraq na Afghanistan ambao sitawazungumzia hapa lakini kwa kuangalia nchi za Afrika na idadi ya watu hawa wanaojaribu kuhatarisha maisha yao kila siku kujaribu kuvuka bahari ya Mediterannean inazidi kutisha.
Wahamiaji vijana wakiiruka miili ya waafrika wenzao ambao wamefariki na ndoto ya kwenda Ulaya.
Idadi ya waafrika wanaofariki katika majaribio ya kwenda Ulaya ni kati ya 22 na 30 kwa jaribio moja.
Boti moja ndogo ya wavusaji huweza kujaza watu wapatao 1000 kwa safari moja.
Ndoto za kwenda Ulaya ni kwa wote si kwa wanawake si kwa wanaume, vijana wa Elitrea wakijaribu bahati yao.
Kijana mdogo wa kutoka Afrika akiwa bado haamini kama ameweza kuokolewa.
Mtoto mdogo akiwa ndani ya meli ndogo ilojaza watu.
Waafika hawa wakigombea koti ya uokozi au life jacket baada ya kufikiwa na meli ya uokoaji.
Hadi sasa waafrika wapatao 132,000 ndiyo walofanikiwa kufika salama nchini Italy ambapo sharia ya sasa inataka waeombe hifadhi ya ukimbizi katika ktuo cha kwanza wanapotia mguu barani Ulaya.
Lakini lengo kuu la wahamiaji hao ni kwenda kaskazini mwa Ulaya hususan kwenye nchi za Ujerumani au Uingereza ambazo nazo sasa hivi zinarekebisha sheria zao za uhamiaji.
Ila sababu kubwa ya wimbi hili la wahamiaji hawa wa kiuchumi ni umaskini, vita, ukandamizaji wa haki za binadamu na kutafuta maisha bora.
Je, Serikali za Afrika zinapoona hali hii huwa zinafikiria nini ili kuwanusuru vijana hawa ambao ndiyo nguvu ya maendeleo katika nchi zao?
Je, Umoja wa Afrika unaona hali hii na kama ni hivyo mbona umekaa kimya?
Kipi kinaweza kufanyika?
Chanzo cha picha: AFP.