Je, kurudiana na Mwanamke mliyeachana nae miaka 13 ni vyema au ni Hatari?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
59,948
119,240
Nasubiri majibu yenu ili nijue najilipua rasmi Kurudiana nae au nisirudiane nae (tusifanye Mapenzi) ila tuwe tu Marafiki.

Katika huu Uzi nitakuwa ni Msomaji zaidi wa Comments zenu na kupitia Comments zenu ndiyo nitaamua nimrudie au nisimrudie.

Kuna Mwamba Mmoja aliniambia aliachana na Mpenzi wake waliyependana mno kwa miaka 17 ila walivyoridiana mpaka sasa wana Mahusiano mazuri kuliko hata yale waliyokuwa nayo Awali.

Na kuna Mwamba mwingime kaniambia aliachana na Mpenzi wake miaka 7 iliyopita na alivyoamua kurudiana nae anasema alipigwa Matukio (alifanyiwa Vitimbi) na Kuteswa nae hadi hata Kutamani Ardhi ipasuke aingie na apotelee mazima.

Na kuna Mwanasaikolojia Mmoja niliwahi kumsikia akisema kuwa mkiona mlikuwa Wapenzi na mkaachana kisha kuamua kurudiana basi hilo ni Jibu tosha kuwa nyie ni Wapendwa hasa ila mnagombanishwa tu na Watu wabaya wenye Wivu nanyi au Maneno ya Watu ila mkiwa Kimya kwa Mambo yenu, mkisameheana baada ya kila Mmoja Kukiri Makosa yake, mkiheshimiana na kumuobudu sana Mwenyezi Mungu na Kumtumainia Yeye mno mkirejeana Kimahusiano ndiyo mtakuwa Bora na Maradufu hata kuliko kule awali ambako kulipelekea Kuachana Kwenu.

Na wala GENTAMYCINE nisichume Dhambi kwa Mwenyezi Mungu huyu Mwanamke ninayetaka kurejeana nae kwa 95% Mimi ndiyo nilimkosea (tena pakubwa tu) na Yeye Makosa yake Kwangu nayapa tu 5% ila alinipenda kuliko Maelezo na 'Mzinguaji Tukuka' nilikuwa ni Mimi.
 
Je, sababu zilizowafanya muachane zilishatatuliwa? Je, mna watoto? Je, mmehakikisha kuweka sawa mahusiano mengine mliyoanzisha baada ya kuachana ili yasigeuke kero mnapoanza upya kurudiana? Je ndugu, watu wenu muhimu na wazazi wanasupport ninyi kurudiana?

Kama jawabu mojawapo la hayo maswali ni HAPANA, basi kuna uwezekano mkubwa mkirudiana baada ya muda mtaachana tena.
 
Ni hatari mnoooo kuliko kubeba bangi walah
si shauri na siwez kumshauri mtu kurudiana na mtu walioachana muda mrefu hvo nooo its not healthy
 
Ni hatari mnoooo kuliko kubeba bangi walah
si shauri na siwez kumshauri mtu kurudiana na mtu walioachana muda mrefu hvo nooo its not healthy
My experience has so confirmed. Siyo Kwa mtu mmoja ila Kwa wanaume zaidi ya watatu. Is absolutely unhealthy. I with my experience, I can not venture into such route.
 
Kuna kupasha viporo alafu Kuna kupasha makabichi haya ya kuachana miak kurudiana ni kupasha makabichi
 
Inawezekana Ila Lazima vitabia vyenu vilivyowatenganisha at first place mviachee,lah sivyo yatakuwa yaleyale.
 
Chuo Mipango motto wao wasemaje

Kuna mambo msingi NADHANI hili si la msingi tulipe muda bado watu twaangalia namna bajeti zinavyokaa
 
Ukitaka raha ya mahusiano usiwe serious we kula utelezi usiwaze kama mliwahi achana usiwaze kama pana feature ikisimama weka waah maisha yasonge
 
Hayanaga muongozo...


Cc: Mahondaw
 
Weee kama ndio anakupa amani ya moyo naye yuko tayari unamrudia vizuri tu
Sema Ndoivo mapenzi hayanaga fomula

Cc Smart911
 
sidhani kama mti uliokatwa unaweza pandwa tena na ukastawi/ nawiri kama mwanzo, but kama ilikuwa source ni wewe and unajua fika kama amekupenda kwa asilimia hizo nakazia tu #chekiafya
 
Nilijaribu,nikapigwa tukio takatifu.
Miaka 13 ulisahau nini kwake ambacho wengine hawakukupa.
Kama wewe ndo uliharibu basi kimepangwa kisasi kibaya sana dhidi ya Popoma.Hayo mahusiano kimbia na hakikisha mbio zinakuwa ndefu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…